Kwanza nawapa hongera AC Milan kwa kutufunza adabu jana,sawa nimekubali matokeo,ila kocha hatuna,kikosi kilekile hadi wamekariri,sikati chenga twawala lakini tulifungwa,ila goli la kwanza refa aliwasaidia mkono walikuwa 12,maana aliunawa kabla Prince kufunga goli,sawa sikatai,ila mimi namlaumu kocha hakuwa na mbinu,mechi ya jana Xavi ilitakiwa asingemaliza angewapa nafasi Thiago na hata Song maana AC Milan walijaza waafrika wengi so Song angesaidia,maana ukichunguza listi ya jana ndio ileile aliweka vs Granada yaani hata AC Milan walijua kabisa listi itakuwa hivi na hata Gang Chomba akapanga utadhani nae alikuwa na wana La Masia,hata mechi ya marudiano siwezi kusema lolote maana wapo frustrated na listi kocha hana mbinu kama Mourinho na Fergie,binafsi Milan wamenifunga ila siwakubali kiukweli hata kama watatutoa,imeniuma tumefungwa na timu mbovu yaani afadhali ningefungwa na Arsenal kuliko AC Milan maana kocha hata angeamua kuwasurprise angewaweka watoto kina Tello,Cuenca,Montoya,Adriano,Thiago nk AC Milan walikuwa wanafungwa palepale kwao kikosi cha jana walikisomea mwezi mzima na ukichunguza sawa kocha inabidi ubadilishe,ndio maana hata Mourinho sasa anaanza kuijua Barca maana kashasoma wachezaji wanaocheza ni walewale,Xavi namuheshimu ni mzuri ila kwa sasa hatakiwi kumaliza 90 zote kama Guardiola alivyokuwa anafanya na hata Del Bosque La Furia Roja timu ya taifa,haya mambo ya kukariri kikosi kila siku wachezaji hao hao mechi za kila kombe kama timu zote za bongo asipocheza fulani basi kocha anaingiliwa ndio inamponza huyu msaidizi Jordi Roura,nimemkumbuka Tito Francesc Vilanova i Bayo,binafsi nasema tena nimekubali nimefungwa ila hata kama tutatolewa kombe natabiri mshindi wa mechi ya Man UTD vs Real Madrid ndio anabeba maana makocha wana mbinu,zaidi ya yote Gang Chomba hongera najua ni party ya kufa mtu kwenu kumfunga mbabe wa soka duniani,ila yote 9 msijisahau sana lakini ni half time ila zaidi sasa tunasubiria mbinu za huyu mimi namuita msimamia mazoezi hana mbinu,wewe utaona tena ktk ligi kikosi kitakuwa hicho hicho,inabidi achanganya kumfanya mpinzani wako asikujue,binafsi imeniuma sana kufungwa na AC MIlan ni bora hata Arsenal ingenifunga kuliko vibonde Milan.Nimemkumbuka sana Josep Guardiola i Sala,yaani in the words of broken heart is just emotion taing me over!