McLaren
JF-Expert Member
- Feb 19, 2025
- 1,170
- 3,743
Wakuu,
Kesi ya Lissu inaendelea leo
Kaa karibu na uzi huu kupata updates ya kinachoendelea
Soma Pia:
===========
Part 209.
Imepigwa high Court ya kikakamavu,
Majaji wameingia wapo watatu kama kawaida yao.
Mhe. Lissu nae yupo
Karani anasoma criminal session No. 19605/ 2025 Republic v. Tundu Lissu
Mawakili wa Serikali wanajitambulisha kama kawaida yao japo leo hawajaja kama utitiri.
Wakili wa Serikali anasema, shauri linakuja kuendelea kusikilizwa na tuna shahidi wa 14 kwa ajili ya maswali ya dodoso.
Jaji Ndunguru anamuuliza Mhe. Lissu kama yupo tayari.
Mhe. Tundu Lissu anasema mimi nipo tayari.
Jaji Ndunguru anamkumbusha Shahidi kwamba yupo chini ya kiapa.
Ikumbukwe kwamba leo tunaendelea na Shahidi wa kificho P9.
Mhe. Lissu: Shahidi habari za asubuhi
Shahidi wa kificho P9 : salama.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama uliandika maelezo tarehe 22 aprill 2025
Shahidi wa kificho P9: Ndio
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama ukionyeshwa maelezo hayo utayatambua.
Shahidi wa kificho P9 : Ndio nitayatambua
SHAHIDI ANAPELEKEWA MAELEZO YAKE.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama hayo ndio maelezo yako uliyoandika polisi tarehe 22 April 2025?
Shahidi wa kificho P9 : ndio ni yenyewe
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji nataka ku-impeach credit ya huyu witness, kwahiyo nitamsomea maelezo yake, nitamuonyesha maeneo ambayo nataka kumuhoji halafu nitamuomba ayawasilishe yapokelewe kama kielelezo.
Mhe. Lissu: Shahidi nitakusomea maelezo yako halafu tutahojiana kwasababu kuna mambo hayapo sawa kwenye maelezo yako, anamsomea maelezo shahidi…
Mhe. Lissu: Sasa shahidi umesikia nilichokisoma, waeleze waheshimiwa majaji kama nilichokisoma ndicho kilichopo kwako.
Sasa nataka nikueleze maeneeo nayotaka nikuhoji;-
1. Jana ulisema wewe ni mkazi wa Mbeya mjini, nataka nikuhoji hapo
2. Kwamba wewe kazi yako ni fundi umeme na unafanya kazi ndani ya maeneo ya Jiji la Halmashauri ya Mbeya
3. 2024 ulivutiwa na sera za CHADEMA na ukaamua kuwa mfuasi na ukawa unafatilia kwa karibu mikutano, matangazo na hotuba za vipngozi wa CHADEMA.
4. Ulizungumzia matembezi ya amani yaliyofanyika Mbeya 2024 na ukasema Mbowe alianzia Songwe na Lissu Uyole na Heche Isanga.
5. April 3, 2025 ukiwa nyumbani kwako ulikua unaperuzi mitandao ya kijamii kwa simu aina Samsung 8 pro nataka nikuhoji kuhusu hiyo simu.
6. Uliingia kwenye mtandao wa instagram na ili uingie kwenye mtandao huo lazima uwe na account na simu janja na bundle ili kuweza kuangalia picha na videos.
7. Wakati unaperuzi mtandao wa instagram uliona video ya Tundu Lissu lakini umesahau ilikua ni account ya nani.
8. Huyo Lissu uliyemuona alikua amevaa kombati ya kaki za chadema na tshirt nyeusi na alikua ukimbini na kulikua na bendera ya taifa na rangi za bendera ya CHADEMA.
9. Alisema tutavuruga uchaguzi kwa kufanya vurugu na kuvuruga uchaguzi huo.
10. Lissu alisema lazima tukichafue.
11. Ulipofika kwenye Kituo cha Polisi Mwanjelwa walikwambia wanataka wakufanyie tena mahojiano.
12. Nilihojiwa na mtu mmoja na mwingine wa pili alinihoji kwenye maswali mbalimbali.
13. Wakati unamjibu huyo anae kuhoji kwa mara ya pili niliona video ya Tundu Lissu, ndio nikaanza kufanya makosa.
Mhe. Lissu: Sasa shahidi waeleze majaji kama ungependa maelezo yako yaingie kama kielelezo mahakamani?
Shahidi wa kificho P9: haina shida.
Upande wa Serikali : hatuna pingamizi
Mahakama: Yamepokelewa kama kielelezo D13
================
PART 210
Anaendelea Mhe. Lissu na Cross Examination.
Mhe. Lissu: Waheshimiwa Majaji naomba shahidi apewe kielelezo D13
Mhe Lissu: Jana kwenye ushahidi wako uliulizwa unaishi wapi na ukasema unaishi katika Halmashauri ya Mbeya, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli.
Mhe. Lissu: Naomba uangalie maelezo yako, nenda palipo andikwa makazi usome pameandikwa makazi yako wapi?
Shahidi wa kificho P9: Pameandiwa Mwakibete.
Mhe. Lissu: Kwenye mstari wa kwanza kabisa sema palivoandikwa hapo? Kwamba unaishi?
Shahidi wa kificho P9 : Pameandikwa Mwakibete lakin nilihojiwa Mbeya.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama unafahamu kwamba haya maeneo huwa yanatangazwa kwenye gazeti la serikali na waziri wa TAMISEMI
Shahidi wa kificho P9 : sifahamu
Mhe. Lissu: Umeonyesha gazeti la Serikali linaloonyesha Mwakibete ni Mbeya,?
Shahidi wa kificho P9; Hapana.
Mhe. Lissu: unafikri unaandika andika tu unaingizwa chaka na mapolisi na wewe unaandika tu.
Mhe. Lissu: Uliulizwa unafanya shughuli gani na ulisema unafanya kazi ya fundi umeme na kazi zako unafanya katika Halmashauri ya Mbeya, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Angalia maelezo yako unafanya kazi gani?
Shahidi wa kificho P9 : Mkulima
Mhe. Lissu: Kazi ni mkulima hapa unajifanya fundi umeme, lugha gongana.
Watu wanacheka: 😂😂😂😂
Mhe. Lissu: nyie Waha wa kigoma wajanja sana nyie na mimi napenda watu wajanja kama wewe.
Mhe. Lissu: Uliulizwa unakumbuka kitu gani kilikukuta 2024, ukasema nilivutiwa na sera za CHADEMA na nikawanafatilia matangazo, mikutano n.k haya sasa soma maelezo yako mjanja wa Jiji la Mbeya…😁
Mhe. Lissu: Waeleze waheshimiwa majaji hayo maelezo uliyosoma hapo kama yapo na ulivyosema jana
Shahidi wa kificho P9 : Hayapo
Mhe. Lissu : Uliandika kwa mapolisi wakakupuuza wakaandika ya kwao.
Mhe. Lissu: Katika matukio mengi uliyofatilia ulitaja matembezi ya yaliyoongozwa na Lissu yalianzia Uyole, na Heche Isanga, mwambie jaji kama Mhe. Heche yupo katika maelezo kayo
Shahidi wa kificho P9: Nilieleza ni Mnyika sio Heche.
Mhe. Lissu: Jana ulisema Heche alianzia Isanga, unataka niwasumbue majaji wakusomee ulichokisema??
Shahidi wa kificho P9: inawezekana nilikosea
Mhe. Lissu: Kazi yangu ni kukamata watu waongo kama wewe.
Shahidi wa kificho P9 : Hiyo unasema ww
Mhe. Lissu: ndio nasema.
Mhe. Lissu: Ulisema mnamo tarehe 3 April 2025 ukiwa nyumbani kwako wakati unaperuzi mitandao kupitia simu yako aina ya Samsung 8 pro, kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : kweli
Mhe. Lissu: Angalia maelezo yako waeleze majaji kama kuna mahala popote ulikua unaangalia mitandao kupitia aina ya Samsung 8 pro.
Shahidi wa kificho P9: hayajaandikwa.
Mhe. Lissu: Asante, mmeuzwa na mapolisi.
Mhe. Lissu: Ulisema kwamba uliingia kwenye mtandao wa instagram na ili uweze kuimgia instagram lazima uwe na simu janja, account na bundle, hayo maneno yapo au hayapo.
Shahidi wa kificho P9 : hayapo.
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako jana ulisema wakati unaingia kwenye instagram uliona video ya Tundu lissu na ukasema huo mtandao umeusahau.
Shahidi wa kificho P9 : Ndio nimeusahau.
Mhe. Lissu: Kama umesahau inamaana, kwenye maelezo yako utakua umeandika.
Shahidi wa kificho P9: Sasa wewe unaniuliza mambo waliyoniuliza mawakili.
Mhe. Lissu: Jibu swali langu. Unanifundisha namna ya kukuhoji?
Shahidi wa kificho P9 : Ndio hakuna
Mhe. Lissu: Uliulizwa muonekano wa Tundu Lissu, ukasema alikua ukumbini alivaa kombati za kaki za chadema na tshirt nyeusi na bendera ya taifa na rangi za CHADEMA, kweli si kwei?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Sasa waeleze waheshimiwa majaji kama yapo katika maelezo yako.
Shahidi wa kificho P9 : Hakuna
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako jana uliulizwa alisema atauzuiaje ukasema tutafanya vurugu na kuuvuruga uchaguzi huo.
Shahidi wa kificho P9: Kweli
==========
Part 211
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia Cross examination Shahidi wa kificho P9
Mhe. Lissu: Waambie majaji kama tutafanya vurugu na kuuvuruga uchaguzi huo kama yapo kwenye maelezo yako…nasubiri jibu shahidi!
Shahidi wa kificho P9: Hayapo
Mhe. Lissu: Uliendelea kusema, alisema lazima tukichafue, kweli si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : kweli.
Mhe. Lissu: hayo maneno yapo au hapo.
Shahidi wa kificho P9 : sasa mbona unarudia maswali. hayapo.
Mhe. Lissu: Twende kwa yaliyotokea 22 April 2025, ulisema siku hiyo ulipigiwa simu na polisi kwenda Kituo cha Polisi Mwanjelwa.
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Sasa soma pale palipoanzia na leo Tarehe 22 April 2025 mpaka nitakapokwambia basi…
Shahidi wa kificho P9 Anasoma…
Mhe. Lissu: Kwenye hiyo sehemu kuna sehemu kumeandikwa kituo cha polisi Mwanjelwa.?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli haijaandikwa
Mhe. Lissu: Na ukasema ulipofika walisema wanataka kukuhoji tena kwa matukio yaliyokuleta hapa.
Shahidi wa kificho P9: Kweli.
Mhe.Lissu : Waambie kama hayo maneno yapo kwa tukio lililokuleta hapa.
Shahidi wa kificho P9 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Kwenye ushahidi wako jana, ulisema nilihojiwa na mtu mmoja na mwingine alichangia kwa kuniuliza maswali mbalimbali, waeleze majaji kama hayo maneno yapo katika maelezo yako?
Shahidi wa kificho P9 : Hayapo.
Mhe. Lissu: Niliona clip ya Tundu Lissu ndio nikaanza, waeleze hayo maneno kama yapo katika maelezo yako.
Shahidi wa kificho P9 : hayapo.
Mhe. Lissu: Sijamalizana na wewe, nataka ukitoka hapa ukawaeleze Mapolisi kwamba kule hakufai!
Watu wanacheka: 😂😂😂😁
Mhe. Lissu: Ulisema mimi kama mwananchama wa CHADEMA nilishawishika na kwamba nitafanya uasi, hayo maneno yapo au hayapo?
Shahidi wa kificho P9: Yapo.
Mhe. Lissu: Sasa nataka uwaambie majaji kwamba wewe ni Mwanachama wa CHADEMA au sio?
Shahidi wa kificho P9 : Mimi sio mwanachama wa CHADEMA.
Mhe. Lissu: Kwenye maelezo yako na ushahidi wako wa jana, ulisema mwaka 2024 ulivutiwa na sera na kuamua kuwa mwanachama wa CHADEMA, kweli au sio kweli?
Shahidi wa kificho P9 :Kweli.
Mhe. Lissu: waambie majaji wafuasi wa CHADEMA huwa wanaandikishwa wapi.
Shahidi wa kificho P9: sifahamu.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama wafuasi huwa wanatambulishwa wapi.
Shahidi wa kificho P9: Sijui
Mhe. Lissu: Waeleze kama huwa wanaalama usoni?
Shahidi wa kificho P9: Hapana
Mhe. Lissu: Na ulisema baada ya kuwa mfuasi ulishiriki katika matembezi ya amani, kweli au sio kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli
Mhe. Lissu: Waambie waheshimiwa kama ulijiandikisha sehemu yoyote?
Shahidi wa kificho P9 : Hapana
Mhe. Lissu: Sasa shahidi hukuwahi kujiandikisha popote, huna alama yoyote kuwa ni mfuasi wa CHADEMA, waeleze majaji wataamini vipi kwamba wewe ni mfuasi wa CHADEMA?
Shahidi wa kificho P9 : Mimi sijui hilo ni suala la amani.
Mhe. Lissu: Unasema tulihamasishwa kushiriki kongamano la vijana lililopangwa kufanyika Mbeya, waambie kama uliwahi kupewa mualiko wowote hata wa simu?
Shahidi wa kificho P9 ; hapana sikupewa mualiko wowote.
Mhe. Lissu: kama kiongozi wa chama aliwahi kukufata ili kukupa taarifa ya kongamano.
Shahidi wa kificho P9 : hawakunifata.
Mhe. Lissu: Kama hawakukufata inamaana hawakujui.
Shahidi wa kificho P9 : Sio lazima wanijue wote.
Mhe. Lissu: Kwa maelezo yako ya ushahidi ya jana, umesema ulisoma VETA Mbeya kati ya 2008-2010 ulipohitimu, kweli au sio kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli.
Mhe. Lissu: waeleze majaji kama umewasilisha cheti cha kuhitimu?
Shahidi wa kificho P9 : sijawasilisha kwasababu hakina umuhimu.
Mhe. Lissu: wataaminije? Kwasababu maneno matupu hayavunji mfupa.
Mhe. Lissu: Umesajiliwa kama fundi umeme wa majumbani na viwandani.
Shahidi wa kificho P9 : Ndio nimesjiliwa.
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama umeleta hati ya kusajiliwa?
Shahidi wa kificho P9: Hapana
================
Part 212
Mhe. Lissu anaendelea kumfanyia cross examination Shahidi wa kificho P9
Mhe. Lissu: Shahidi umesema tarehe 4 april 2024 ukiwa na jamaa zako nyumbani kwako, “Tukawa tunajadili kauli ya Mwenyekiti kwamba tukichafue, ni kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Ni kweli.
Mhe. Lissu: Umewataja hao jamaa zako wakati unatoa ushahidi?
Shahidi wa kificho P9 : Hapana.
Mhe. Lissu: Wakati tunazungumza jamaa yangu akaniomba namba yangu ya simu, jamaa ambaye simfahamu, unakumbuka hayo maneno?
Shahidi wa kificho P9 : Ndio nakumbuka.
Mhe. Lissu: inawezekana mtu usiyemfahamu kuwa jamaa yako, hiyo inaingia akilini!
Shahidi wa kificho P9: Inawezekana.
Mhe. Lissu; Na jamaa yako ambaye humfahamu akakuomba namba yako ya simu na ukampatia? Inaingia akilini?
Shahidi wa kificho P9 : ndio inaingia akilini.
Mhe. Lissu: ndivyo ulivyofundishwa na mapolisi.
Mhe. Lissu: Kwa vile unafanya kazi ya fundi umeme kwa malipo, una leseni ya biashara?
Shahidi wa kificho P9: Sina leseni ya biashara kwasababu sina ofisi
Mhe. Lissu: Una TIN number?
Shahidi wa kificho P9: Ndio
Mhe. Lissu: Umeionyesha?
Shahidi wa kificho P9 : hapana kwasabb haijahitajika.
Mhe. Lissu: Tarehe 5 April 2024 siku ambayo unakamatwa, unasema ulipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha kuwa ni mteja, na ukasema tulipoonana akajitambulisha kuwa ni afisa wa polisi na akanionyesha kitambulisho chake, waambie waheshimiwa majaji kama unakumbuka jina la icho kitambulisho?
Shahidi wa kificho P9: Nakumbuka ni Vicent
Mhe. Lissu: Waeleze majaji kama hilo jina lipo kwenye maelezo yako.
Shahidi wa kificho P9: Halipo.
Mhe. Lissu: Hiyo tarehe 5 April 2024 uliandika maelezo kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P9 : Kweli.
Mhe. Lissu: Na maelezo ya siku hiyo yalihusu uchochezi na kuzuia uchaguzi, kweli au si kweli?
Shahidi wa kificho P9: Kweli
Mhe. Lissu: Waambie majaji hiyo tuhuma ya uchochezi na kuzuia uchaguzi imeishia wapi?
Shahidi wa kificho P9 : Sijui
Mhe. Lissu: Waeleze majaji tangu tarehe 5 april 2024 umepelekwa Mahakamani kwa tuhuma hizo?
Shahidi wa kificho P9 : sijawahi kupelekwa
Mhe. Lissu: Waeleze majaji ulipoitwa polisi kwa mara ya pili 22 april 2025 kama ulielezwa tuhuma za uchochezi na kuzuia uchaguzi?
Shahidi wa kificho P9: Ndio nilielezwa.
Mhe. Lissu: Angalia maelezo yako shahidi halafu tuonyeshe wapi uliuzwa juu ya tuhuma hizo
Shahidi wa kificho P9: Mimi nilieleza lakini wao hawakuandika.
Mhe. Lissu: Imekula kwako kwasababu wanasema haya ni maelezo yako.
Mhe. Lissu: Wewe ni shahidi kwenye kesi dhidi yangu, kweli si kweli.?
Shahidi wa kificho P9 : kweli
Mhe. Lissu: Na ndio maana umekuja kutoa ushahhidi jana na leo, kweli si kweli.
Shahidi wa kificho P9 : kweli.
Mhe. Lissu: Nikisema walikukamata tu ili uje kutia ushahidi dhidi yangu nitakua nakosea??
Shahidi wa kificho P9 : Mimi sifahamu.
Mhe. Lissu: Waambie waheshimiwa majaji kama unajua kuwa hakuna kosa la kuzuia uchaguzi?
Shahidi wa kificho P9 : ni kosa.
Mhe. Lissu: waambie majaji ni kwa mujibu wa sheria gani?
Shahidi wa kificho P9 : mimi sio mwanasheria.
Mhe. Lissu: ni sheria gani.
Shahidi wa kificho P9 ; Mimi najua kuzuia uchaguz kwa njia ya vurugu ni kosa lakini sheria gani sijui
Mhe. Lissu: Kama hujui sema sijui, sio kuleta ujuaji tu.
Mhe. Lissu: Kwani mimi nimeshatakiwa kwa kosa la vurugu.
Shahidi wa kificho P9 : umeshtakiwa kwa uhaini.
Mhe.Lissu: Shahidi ulikujaje Dar es salaam
Shahidi wa kificho P9: Nilipanda bus
Mhe. Lissu: Nani alikwambia uje kutoa ushahidi
Shahidi wa kificho P9 : Nililetewa wito
Mhe. Lissu: nani alikuletea?
Shahidi wa kificho P9 : aliniletea Mwenyekiti wa serikali za mtaa.
Mhe. Lissu: anaitwa nani?
Shahidi wa kificho P9 : Siwezi kukutajia kwasababu za kiusalama.
Katuga: sisi tunapinga hilo swali kwasababu za kiusalama. Kwahyo tunaomba hilo swali asiulizwe.
===================
Part 213

Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji hilo pingamizi la Wakili la Serikali halina maana yoyote, kwasababu shahidi mwenyewe amesema kwamba summons alipelekewa summons na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa na Mwenyekiti ni ofisa wa serikali, lakini vilevile Mahakama haitaweza kujua kama huyu shahidi ni mkweli au ni muongo kwahiyo swali langu ni halali na ninaomba pingamizi lao litupitiliwe mbali, lakini huyo Mwenyekiti sio mtu ambaye amelindwa na sheria.
Katuga: Sisi tunaomba swali hilo shahidi asiulizwa kwasababu swali hilo litapelekea utambuzi wa shahidi huyu na kama tunavyojua humu ndani kuna wafuasi wake, researchers wake wanaweza wakaenda kumtafuta ili kumtambua shahidi huyu.
Mhe. Lissu: naomba ondoa hiyo kauli yako mimi sijazungumzia kuhusu wafuasi wangu humu.
Katuga: Naondoa hiyo ilikua ni by the way lakini msimamo wetu ni kwamba swali hilo shahidi asiulizwe
Mahakama: tunadhani uendelee na x-examination bila hilo jina.
Mhe.Lissu: Lakin waheshimiwa majaji mnaweza kuona namna cross examination yangu inavyokua limited lakini naomba niendelee.
Mhe. Lissu: shahidi umekujaje hapa
Shahidi wa kificho P9: nimependa bus
Mhe. Lissu: nani amekulipia nauli
Shahidi wa kificho P9 : nimejilipia mwenyewe
Mhe. Lissu: Umefikia wapi
Shahidi wa kificho P9 : Kwa ndugu yangu.
Mhe. Lissu: Waambie waheshimiwa majaji kama kuna kiongozi au mfuasi anajua kama unakuja kutoa ushahidi
Shahidi wa kificho P9: Ndio wapo baadhi
Mhe. Lissu: waliwahi kukutishia
Shahidi wa kificho P9 : ndio
Mhe. Lissu: unajua hilo ni kosa
Shahidi wa kificho P9 : hilo ni kosa la jinai
Mhe. Lissu: umewataja,
Shahidi wa kificho P9 : siwezi kuwataja kwa usalama
Mhe.Lissu: waeleze majaji kama ulitoa taarifa kituo cha polis
Shahidi wa kificho P9 : ndio
Mhe. Lissu: Kituo cha polisi kipi?
Shahidi wa kificho P9: Sasa nikitoa taarifa hiyo hapa si itakua navunja usalama?
Mhe. Lissu: Hebu jibu swali bwana tusisumbuane
Mahakama: Shahidi hebu jibu hilo swali
Shahidi wa kificho P9: Nilitoa kituo cha polisi Ilomba
Mhe. Lissu: Ulipewa RB
Shahidi wa kificho P9: ndio
Mhe. Lissu: umeitoa hapa mahakamani?
Shahidi wa kificho P9 : hapana
Mhe. Lissu: Polisi walichukua hatua gani?
Shahidi wa kificho P9: Walisema watafatilia
Mhe. Lissu: waambie waheshimiwa majaji kama kuna mtu yoyote amekamatwa
Shahidi wa kificho P9 : hapana
Mhe. Lissu: Waambie kama kuna mtu yoyote amepelekwa mahakamani:
Shahidi wa kificho P9 : hakuna
Mhe. Lissu: Waheshimiwa majaji sina swali lingine kwa shahidi huyu.
Wakili wa Serikali: Leo tunashahidi mmoja, tunaomba break kidogo halafu tuje na shahidi mmoja aliyebaki, kwasababu jana hatukupumzika.
Mahakama: Mshitakiwa unasemaje
Mhe. Lissu: Tukienda kwa utaratibu huu tutachukua mida mrefu sana, Mahakama ilisema upande wa serikali ulete mashahidi wasiopungua watatu, kwanin hawajaleta hao mashahidi wengine.
Upande wa mashtaka wanatakiwa wawe na mshahidi wengine kama walivyotakiwa na Mahakama.
Katuga: Jana tulisema tutakuja na shahidi mmoja then twende kuargue application yetu, hatujaweza kuja na mashahidi wengi ili tupate muda wa kutosha kwasababu yeye alisema ana-objection.
Mahakama: Nadhani twende break fupi kwanza ili tukirudi tuendelee na huyo shahidi halafu tukimalizana nae mambo mengine yatafata.

- Shahidi wa Kesi ya Lissu (P7): Nauli ya kuja mahakamani leo nimepewa na mwanamke wangu. Ndiye ananiweka mjini
- Kesi ya Tundu Lissu kuendelea leo Februari 17, 2026, mashahidi wa Jamhuri wasiopungua watatu wangojewa
- Kesi ya uhaini dhidi ya Lissu: Shahidi wa saba kati ya 30 wa Jamhuri kuanza kutoa ushahidi
- Kesi ya Lissu | Shahidi wa Siri (P6): Lissu alisema tunakwenda kuvuruga uchaguzi na kukinukisha
- Kesi ya Lissu: Hiki ndicho Kizimba cha mashahidi wa kificho, kilichosababisha Kesi kuahirishwa
- Baada ya takribani miezi mitatu, kesi ya Tundu Lissu kuendelea leo Februari 9, 2026
- Kesi ya Lissu: Mahakama yaagiza Kizimba cha Mashahidi wa siri kirekebishwe Majaji wawaone. Kesi kuendelea Feb 12, 2026
- Kesi ya uhaini ya Lissu, mahakama kutoa uamuzi wa mapingamizi leo Feb 11, 2026
- Kesi ya uhaini ya Tundu Lissu kuendelea Februari 9 hadi Machi 6, 2026
- Shahidi wa kesi ya Lissu (P7) anasema alikamatwa mara tu baada ya kuangalia video ya Lissu iliyokuwa Jambo TV
- Kesi ya Lissu | Shahidi wa siri (P5): Niliona video ya Lissu akisema atakinukisha, uchaguzi mkuu hautafanyika
- Mama wa CHADEMA azimia mahakamani baada ya Lissu kudai kunyimwa chakula
- Mahakama kuu, Kanda ya Dar es salaam Tarehe 11 Februari, 2026 kutoa uamuzi mdogo katika kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu