Kinachoamua uwiano wa bajeti iegemee wapi zaidi ni mapato yanayokusanywa nchini kwako kwanza. Mara nyingi matumizi ya kawaida kama kulipa madeni (ya ndani na nje), mishahara, posho, ununuzi wa magari, mafuta, ruzuku, n.k huwa vinakuwa na ongezeko ambalo haliendani na kasi ya ukusanyaji mapato, hivyo hupelekea kiasi kikubwa kutumika ktk upande huo na kiasi kidogo kinachosalia huenda ktk maendeleo. (Revenue-driven budget)
Kwa sehemu kubwa ya deni la taifa hukopwa ili kuongeza kiwango cha bajeti ya maendeleo na kiasi kingine huwa tunachangiwa na wahisani. Ila njia ya kutoboa kupitia bajeti ndogo ni kuhakikisa tunakuwa na miradi michache ila inapata uwekezaji mkubwa na kupunguza miradi isiyo na tija sana na yenye uchocheo mdogo ktk uchumi. Pia, serikali ijikite ktk kutoa huduma zaidi haya mashirika ya kibiashara kama ATCL ingetafutwa namna tuyamiliki kwa asilimia 25 tu, ili tupunguze gharama za uendeshaji. Mengi yanaendeshwa kwa pesa za umma.