Fedha ya matumizi ya kawaida kuwa kubwa kuliko ya matumizi ya maendeleo ina maana gani?

Fedha ya matumizi ya kawaida kuwa kubwa kuliko ya matumizi ya maendeleo ina maana gani?

Wizara ya fedha ndio inalipa mishahara na ruzuku ya Chadema usishangae matumizi ya kawaida kuwa makubwa hivyo bwashee!
pls kuwa unakuywa maziwa baada ya kuvuta ile kitu , chadema wanapata ruzuku wapi, wewe itaungua pressure high blood kwa chuki zako dhidi ya cdm
 
Hii matumizi ya kawaida kuzidi maendeleo ni kila wizara serikalini
 
Kabla ya kukurupuka ungeingia tovuti ya bunge au wizara ya fedha utaikuta hotuba nzima na mchanganuo wake

Were mjinga recurrent expenditure ya namna hiyo kama ilivyoanishwa kwenye tovuti yao ni matumizi ya hovyo ambayo hayapaswi kubarikiwa na sisi walipa kodi!!!
 
Hii ni abajeti ya mwaka 2020/21

, Wizara ya Fedha na Mipango inaomba kuidhinishiwa jumla ya shilingi trilioni 12.39 kwa mafungu yote saba (7) kwa ajili ya matumizi ya kawaida na maendeleo. Kati ya kiasi hicho, shilingi trilioni 11.73 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na shilingi bilioni 659 kwa ajili ya matumizi ya maendeleo. Kati ya matumizi ya kawaida, shilingi trilioni 10.48 kwa ajili ya deni la Serikali, shilingi bilioni 750.29 matumizi mengineyo na shilingi bilioni 510 kwa ajili ya mishahara na marekebisho ya mishahara. Aidha, matumizi ya maendeleo yanajumuisha shilingi bilioni 624.7 fedha za ndani na shilingi bilioni 34.61 fedha za nje.

Sh. Trillion 10.48 kwaajiri ya deni la serikali/taifa... Hizi pesa ni nyingi Sana kulinganisha na ujumla wa bajeti kuu ya wizara zote....

Kama pesa zote hizo zinalipa deni ingekuwa deni linapungua kuliko sasa kuongezeka... Miaka mitatu tu ingepunguza nusu ya deni la taifa...

Hizi bajeti ni tarakimu tu tofauti na uhalisia...
 
Nenda kajifunze public finance utapata picha kubwa kuhusu hilo unaloongea, iko hivi kila mwaka serikali inakopa fresh debts ili kulipa deni la nyuma, kwa mantiki hiyo deni haliwezi kupungua zaidi ya kuongezeka babu, yaani unadaiwa shing 100 unaenda kukopa 50+riba ili ukapunguze deni la shing 100 je ktk mtririko huo deni litapungua au litazidi kupanuka.
 
Matumizi ya kawaida ni lazima yawe juu sababu kuna mishahara, running cost mbalimbali na mambo kibao hapo sishangai sn, tatizo lipo hapo kuwa fedha za maendeleo hata hiyo kidogo hazitolewi zote
 
jamani si humu ndani tulisema tunataka maendeleo ya watu na si vitu.sasa hii ni bajeti ya watu na si vitu.hahahahaaaaa!
Ni bajeti mbinuko, halafu bajeti mbonyeo ndio onayosaipport maendeleao kwa asilimia lubwa, sema safari hii naona imekua kinyume kidogo
 
View attachment 1812485
BAJETI ina matumizi mengi ya kawaida kuliko Matumizi ya maendeleo ya nchi?

Hivyo kweli tutaendelea
nchi yetu kiuchumi? Bajeti aliyotoa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu ili ipitishwe na Wabunge ni bajeti mbaya haifai kupitishwa Wabunge.

Tunamuomba Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu atueleze Shilingi Trilioni 11.93 zitatumika kwa ajili ya Matumizi yapi ya kawaida? Wakati pesa aliyoweka ya Maendeleo ni ndogo sana Shilingi Trilioni 1.02.

Maendeleo gani yatakayoweza kuifanikisha Tanzania kwa Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02.? Hebu atufafanulie zaidi Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu.
Mkuu sikuelewi!
 
1622442542208.jpg
 
Wizara ya fedha ndio inalipa mishahara na ruzuku ya Chadema usishangae matumizi ya kawaida kuwa makubwa hivyo bwashee!
Wewe mbona una akili ya panzi sana, kwako chama ni Chadema tu hujui kwamba hii nchi ina vyama zaidi ya ishirini. You're very useless in this forum.
 
Nawaelewesha LA saba wenzangu mana coment za [emoji115][emoji115] hamtazielewa zp kisomi ni kwamb wale wabunge waliyeomba hy bajet /fedha wapo sahh coz mle bungen kuna wabunge ambao wamepewa vyeo vya uwaziri wa kitu husika mfano wazir wa kilimo nk kwhy hiyo bajet kubwa kuliko zote ndani yake ndio kuna hizo secta husika

Sent from my VFD 200 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo bajeti ni ya wizara ya fedha peke yake. Kuna pesa nyingi za maendeleo kwenye wizara nyingine haswa wizara ya ujenzi na uchukuzi. Na hapo kwenye matumizi ya kawaida sehemu kubwa, zaidi ya tsh 10 trillions, ni kwa ajili ya kulipa madeni.
 
Hiyo ni kawaida, chukulia mfano nyumbani kwako ... pesa ya maendeleo vs matumizi ya kawaida. By the way I think there is a very thin line between the two ...
 
View attachment 1812485
BAJETI ina matumizi mengi ya kawaida kuliko Matumizi ya maendeleo ya nchi?

Hivyo kweli tutaendelea
nchi yetu kiuchumi? Bajeti aliyotoa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu ili ipitishwe na Wabunge ni bajeti mbaya haifai kupitishwa Wabunge.

Tunamuomba Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu atueleze Shilingi Trilioni 11.93 zitatumika kwa ajili ya Matumizi yapi ya kawaida? Wakati pesa aliyoweka ya Maendeleo ni ndogo sana Shilingi Trilioni 1.02.

Maendeleo gani yatakayoweza kuifanikisha Tanzania kwa Pesa ya Shilingi Trilioni 1.02.? Hebu atufafanulie zaidi Mheshimiwa Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Mwigulu.
Maendeleo mtaysikia kwa majirani
 
Back
Top Bottom