Fedha za bima kwa wote kukatwa kwenye line za simu, mpango wenu Serikali ni Watanzania tuache kabisa kuwasiliana?

Idea nzuri sana ila tunataka huo mfuko usiwe tied na serikali maana utageuzwa shamba la kufisadi.
 
badala ya kuishauri serikali kutafuta na kutengeneza vyanzo vipya vya mapato yeye amefikiria akaunti binafsi za watanzania ndio chanzo cha mapato, kweli kuwa na hela sio kuwa na akili kuna wadangaji hadi kwenye siasa.
 
Kama watanzania wangekuwa wakimsikia daktari anasema kitu wanaelewa na kupokea basi bima ingetufaa.

Lakini kama Prof. Janabi akisema kitu watu wanabeza. Ni wazi bora mzigo wa afya ubakie kuwa kitu cha maamuzi binafsi tu
 
Ipo siku Tanzania haitakalika kama Haiti,CCM washenzi sana,wanadhani Watanzania ni wale wale siku zote
 
Utakatwa huo mpunga na wakati wa matumizi ya hiyo pesa ujiko atapewa Rais wa CCM atayekuwa madarakani kwamba "Tunamshukuru Rais XXX kwa kutoa fedha za matumizi YYY"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…