Fedha za bima kwa wote kukatwa kwenye line za simu, mpango wenu Serikali ni Watanzania tuache kabisa kuwasiliana?

Fedha za bima kwa wote kukatwa kwenye line za simu, mpango wenu Serikali ni Watanzania tuache kabisa kuwasiliana?

Idea nzuri sana ila tunataka huo mfuko usiwe tied na serikali maana utageuzwa shamba la kufisadi.
 
badala ya kuishauri serikali kutafuta na kutengeneza vyanzo vipya vya mapato yeye amefikiria akaunti binafsi za watanzania ndio chanzo cha mapato, kweli kuwa na hela sio kuwa na akili kuna wadangaji hadi kwenye siasa.
 
Kama watanzania wangekuwa wakimsikia daktari anasema kitu wanaelewa na kupokea basi bima ingetufaa.

Lakini kama Prof. Janabi akisema kitu watu wanabeza. Ni wazi bora mzigo wa afya ubakie kuwa kitu cha maamuzi binafsi tu
 
Wakuu,

Kuna watu mpaka unafikiria mtu kama huyu kafikaje bungeni, maana ni zaidi ya weupe kichwani, watupu kabisa!

Kodi zote hizi mnazotuumiza nazo wananchi bado unataka ziongezwe nyingine kwenye line za simu?

Hii siyo ya kukalia kimya!

Dunia inapiga kasi kwenye digidali lakini Viongozi wetu ndio kwanza wapo mstari wa mbele kuturudisha nyuma!

Mbunge unajua hali za wananchi wako, gharama za maisha zinapanda kila kukicha, baada ya kutafuta njia ya kupunguza mzigo unataka umuongezee tena kodi?

Ndio mmeona hii ndio itakuwa njia rahisi ya kuwafanya watu wasipate taarifa, mpite bila kupingwa na kuendesha serikali kama vile mnaendesha ng'ombe?

Wale wa kukaa kimya na kuona matatizo yanawagusa watu fulani, hii inaenda kukugusa hata wewe! Piga kelele, embu tuache kuwa wajinga na kukubali upuuzi kama huu kuendelea kufanyika!

Raia wa Gairo, Mbunge wenu Ahmed Shabiby kapendekeza takataka huko bungeni, endeleeni kuwa chawa tuendelee kusaga meno mpaka kiama!

Kwa nafasi yako piga kelele, hata wewe unayetoa povu hapa unafanya kwa nafasi yako, usikae kimya wakati una uwezo wa kusema, kama Rais huwa anapita amini na wale wengine wanapita kuchungulia kama mmekubali au lah, huwezi kwenda kuandamana piga spana JF dawa iwaingie huko huko walipo!


====

Pia soma Mbunge wa Gairo, Shabiby ataka fedha za bima kwa wote zikatwe kwenye laini za simu
Ipo siku Tanzania haitakalika kama Haiti,CCM washenzi sana,wanadhani Watanzania ni wale wale siku zote
 
Utakatwa huo mpunga na wakati wa matumizi ya hiyo pesa ujiko atapewa Rais wa CCM atayekuwa madarakani kwamba "Tunamshukuru Rais XXX kwa kutoa fedha za matumizi YYY"
 
Back
Top Bottom