Fedha za Plea-Bargain aulizwe Balozi Mbelwa Kairuki, anajua vizuri sana

Mama ameongezewa mke mwenza lini, acha uzushi. Kwani Jiwe wakati anamsema Kikwete, wakati naye alikuwa waziri, kwanini asingeachia huo uwaziri. Acha unafiki
 
Viongozi hawa wakuu wana tabia ya kulindiana madhaifu yao na hii ndiyo mara ya kwanza tunaona kiongozi aliyeko madarakani akimshambulia mtangulizi wake non stop; na kujisahaulisha kuwa naye alikuwa ndiye second in command wa serikali hiyo hiyo anayoishambulia; na kwamba hawezi kukwepa madhaifu ya wakati ule kwa asilimia 100%

Ni kama vile amepewa masharti na watoa pesa za kampeni yake ya urais 2025 kwamba ili ubakie madarakani ni lazima ufanye hiki na kile. Ngoja tuone itakavyokuwa lakini sidhani kama hii ni strategy nzuri.

Kwenda 2025 hapa angejaribu tu kupunguza ukali wa maisha kwa mtu wa kawaida kama anavyofanya mwenzake huko Zanzibar. Labda anajiamini kuwa CCM kama kawa itashinda tu kwa gharama yo yote ile. Ambacho hajui ni kwamba akijichanganya akaruhusu katiba mpya na tume huru ya uchaguzi asije kushangaa akiangukia pua hiyo 2025 maana bila kuiba kura CCM hii ya sasa ni nyepesi sana japo nadhani pia ni kama kaichezea CHADEMA kwa kuwaasalisha baadhi ya makamanda wake.

Time will tell!
 
Haya maneno ni mazito mno.
 

Kwa kukukumbusha tu second in command wa ukweli alikua ni BASHITE ALBERT na third in command ni yule MDAIWA GHALI ZAIDI ndani ya Tanzania, huyu mama na PM walikuwa mapazia tu wasitwishwe lawama .
 
Sitetei mh Rais, wanaosema kuwa Samia alikuwa anajua kinacho endelea nadhani hawakuwahi kuwa viongozi au kuwa na nyadhifa za usaidizi ktk uongozi, point yangu ni kwamba unaweza kuwa sehemu ya uongozi lakini usijue chochote kinachoendelea Kwa mkubwa wako
 
Naunga hoja mkono
 
CCM wote ni majizi, wa zamani, wa sasa na wajao
 
Kwamba YOTE "mabaya" aliyokuwa akiyafanya Jiwe yeye hakuyaona wala kuyasikia hata kwenye nyaraka za siri zilizokuwa zinavuja kwenda kwa Kigogo na Kimambi zikiwa za moto; na zikakoma mara moja alipoingia madarakani? Kama aliyasikia, alichukua hatua gani?

Yawezekana lakini hawezi kujitenga kwa asilimia 100 na makosa ya mtangulizi wake; na tungekuwa na demokrasia ya kweli na investigative journalists ambao siyo waoga ingekuwa rahisi tu kuonyesha kuwa hata yeye alihusika katika baadhi ya maamuzi haya haya anayoyapigia kelele.

Mimi namuona ni kama mtu mwoga tu asiyejiamini na ambaye anashinikizwa na kikundi fulani cha watu wenye nguvu na wenye malengo yao binafsi. Au anajaribu tu kuficha madhaifu yake mengine (mf. Upigaji wa wazi wazi unaoendelea), kupanda sana kwa maisha ya mwananchi wa kawaida huku yeye akiangalia tu wakati mwenzake wa Zanzibar akichukua hatua,...na mengineyo.

Mama ni mwanasiasa na mwanadiplomasia mzuri sana na kuna mazuri mengi amefanya katika uwanja huo lakini pia kuna mengi ya msingi ambayo ama yamemshinda kutokana na mfumo alioukuta au hataki tu kuhangaika nayo; na badala yake anaishia tu kulalamika.

Ngoja tuone atakachowafanya akina Biswalo, Dotto James na wengine ambao ni wahusika wakuu wa hili sakata alilolianzisha...

Siasa!

Sihasa!
 
Umejuaje yote haya brother kama si story zs kutunga. Huu ndiyo muda sahihi wa yeye kuachia ngazi. Madudu kila mahali na wananchi tumemchoka. Nchi imemshinda hii anabak kuimpress msoga.
 
Aliwahi kuhoji mahali, "Kuna hela zimeletwa hapa kwangu na nimeambiwa nizilinde ila sijui ni za nini japo zimetoka nyumbani". Samia anzia hapo.
Kuna watu wamejitajirisha kwa hizi hela za makubaliano kati ya DPP na washitakiwa feki.
 
Hata ukitoa mishipa yote ya shingo Magufuli alivunja rekodi ya wizi tangu taifa letu liasisiwe. Kama vipi mfuate sasa huko kuzimu umsaidie kukusanya kuni.
 
Pamoja na hayo yote our late beloved president alipendwa na kila Mtanzania mwenye akili timamu. Mnaomchukia na kumwita mwovu mpimwe uwezo wenu wa kufikiri. Huyuhuyu mnaemwabudu anaupiga mwingi si ndiye aliyetuaminisha uwepo wa gaidi hapa Tanzania. Au nae mnasubiri Mungu aamue ugomvi waramba asali nao wapate pigo sawa na hali ilivyo kwa wanyonge hivi sasa, ndipo muanze kumkejeli?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…