Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL (Tegeta Escrow account), ni mali ya umma

Fedha zilizokuwa katika akaunti maalumu ya IPTL (Tegeta Escrow account), ni mali ya umma

acha akili za kitoto unachoshangaa nini? mfanyabiashara kugawa hela au viongozi kupewa hela, kama wamepewa kutokana na ukarimu wa mfanyabiashara kinachokuuma nini?,kama amehonga waziri mbunge sababu ni hawara yake unawashwa nini?, kama ametoa ili kujenga mahusiano mema na watu aliowapa kinakuboa nini?,acha fikra za kimasikini kiasi hicho
Hivi wewe Rebecca, toka uanze kutembea na wanaume ulishawahi kupewa milionimilioni ukihesabu ziwe 1600? Afu useme anajenga mazingira mazuri ili umpende, hii ni bongo, unapokua unatetea ufisadi sijui unataka kujenga taifa gani? Sasa unadhani hatukujui, umemegewa 0.00000000001 ya mlungula sasa unabaki kuhangaika humu kuwa divert watu na ukweli, njaa inakusumbua sana. Huwezi kueleweka kama kila siku bei za umeme zinapanda watanzania wanashindwa hata kuchemsha maji kwa umeme, afu watu wanagawana mipesa hjku watu wanalia, kwanini wasiwasaidie hata dawa basi au wapunguze gharama za umeme? Acha um..a wa kingese.
 
Acha upunguani, matusi ya nini sasa, hivi mtatumika mpaka lini? Hivi unaona bei ya umeme huu wanaotuuzia tanesco kwa bei ya kutupa, afu ukasikia watu wamegawana surlplus, unaona ni sawa kweli? Wewe unadhani hata zingekua ni za iptl kwa hiyo viongozi ndo wenye haki ya kugawana hizo pesa? Unamanisha viongozi ndo iptl? Nahata ingekua tofauti huyo rugemarilwa kiongozi wa kampuni tanzu amepata faida kiasi gani mpaka kugawia viongozi mipesa kama njugu? Hivi kama kapata faida kiasi hiko maka kugawa kiasi cha mablioni, viongozi wetu hawaoni haja sasa yakupunguza gharama za umeme ili mwananchi wakawaida aweze kumudu kuliko kumkamua mwananchi hohehahe alafu unamchapa viboko achangie maabara? Acheni ushabiki. Hii ni pesa ya uma nalazima irudi na wahusika kuchukuliwa hatua zakisheria


Acha matusi, nani anatumika sasa, kwahiyo mtu akiwa na mtazamo tofauti na wako anatumika?

Mkuu st. Kayumba kweli noma, nimepata shida sana kukuelewa :smile-big:. Sasa wewe inakuhusu nini kama kagawa mipesa kama njugu? Pesa za Rugemarila, kama kagawa sizakwake.
 
Mbona unanitukana bila sababu? Laiti ungekuja na taarifa mbadala ningekusamehe, lakini wewe unakurupuka tu na kurusha matusi. !!! Dah! Tanzania niipendayo ina njia ndefu. Sasa kama wewe si mzushi, mpuuzi usiye elimika niambie ni wapi nimesema fedha hizo ni za ccm? Kama wewe si shoga niambie kwa vigezo vipi nafanana na msalani ki hoja, jina au sura. Jikusanye kijana maisha bado hanakusubiri.Kimantiki, fedha za escrow ni mali ya IPTL
sina muda wa kushindana na mfu kama wewe

View attachment 204660View attachment 204661
 
acha akili za kitoto unachoshangaa nini? mfanyabiashara kugawa hela au viongozi kupewa hela, kama wamepewa kutokana na ukarimu wa mfanyabiashara kinachokuuma nini?,kama amehonga waziri mbunge sababu ni hawara yake unawashwa nini?, kama ametoa ili kujenga mahusiano mema na watu aliowapa kinakuboa nini?,acha fikra za kimasikini kiasi hicho
Nyie kenge madoa hamtoki halafu mko wachache sana mnao jenga nyumba kwa mchanga tupu hewani!! Rudisheni hela zetu period!!
 
kweli akanye alale anataka kujiona yeye anaujua ukweli, hajui wenzake wanalia dodoma
 
Unatumika kinyume na maumbile, sasa akili zako zinafikiria kinyume na maumbile, puru lako..!!!

Baada ya kusikia kelel nyingi juu ya suala la ESCROW, Nimepitia taarifa mbalimbali zinazohusu suala la fedha za account hii ya EScrow kwa upole, utulivu, unyenyekevu na bila ushabiki. Katika taarifa hizo nimepata kuelewa kuwa fedha za Escow si za umma, wala hazijaibiwa ka namna yoyote. Bali fedha hizi ni mali ya kampuniya IPTL kupitia kampuni tanzu mbili yaani Menchmar na VIP.

Kwa muda wa zaidi ya miaka miwili kumekuwapo na mgogoro wa waziwazi wa kimaslahi kati ya wamiliki wa IPTL ambao ni kampuni ya VIP na kampuni ya Mechmar kutoka Malaysia. Tuliokuwa tunafuatilia habari, hili si jambo geni

Cha ajabi kwangu, watu wengi wanashabikia bila kujua wala kujali kufuatilia kuwa account ya escrow ilianzishwaje. Taarifa zilizowazi zinaonyesha kwamba Mahakama Kuu, kufuatia mgogoro uliokuwepo, iliamua pande zote mbili yaani VIP na Mechmar zisaini hati ya makubaliano juu ya kutunza fedha za malipo ya kila mwezi ya umemeyatokanayo na umeme unaozalishwa na IPTL na kuiuzia TANESCO. Mpaka hapo nadhani wenzangu mmeanza kupata picha ya hili suala sumbufu.

Taarifa zinaonyesha kuwa, mahakama ilielekeza malipo hayo yahifadhiwe katika akaunti hiyo mpya ya ESCROW iliyofunguliwa Benki kuu hadi mgogoro kati ya wabia hawa wawili utakapoamriwa.
Mpaka hapo ndugu zangu, ikiwa taarifa hizi ni za kweli, mtakubaliana nami kuwa fedha za ESCROW ni mali ya IPTL. Yaani MENCHMAR na VIP. Zaidi ni majungu na wivu.

Sasa tujiulize mgogoro upo wapi? walalamikaji ni akina nani? fedha ambazo TANESCO imeridhia kulipia huduma inayotolewa kwa kazi ambayo imeshafanywa zinakuwaje fedha za umma?Ijulikane kuwa malipo yoyote ya taasisi nyeti kama TANESO hufanywa kwa kufuata taratibu na kuzingatia kanuni. maana yake malipo yale ni malipo halali kwa kazi halisiiliyofanywa.

Mwenzenu nimeona kuwa yawezekana jambo hili ni zaidi ya haya yanayotaarifiwa kwa uwazi.Pengine kuna nguvu inayoendesha mambo nyuma ya pazia. Suala lenyewe hapa lipo katika swali la kwanini baadhi ya viongozi wa umma wamepata mgao (Kama kweli wamepata, mimi hainihusu wala sina muda wa kuwaonea wivu). Hata hivyo bado hakuna sababu dhahiri ya kuziita fedha za ESCROW kuwa ni za umma. Zinabaki kuwa ni malipo ya umeme ambao TANESCO imeridhia kuwa umezalishwa na IPTL

Najua ni rahisi kuzusha mambo na kuyafanya yawe ni mjadala mkubwa katika jamii ya watu waliokosa mweleke na kukata tamaa. Wengi wetu tuna madeni, mipango yetu na njozi zetu zimevurugika... katika hali hii ni rahisi kupenda habari za uzushi zaidi kuliko za kweli na zenye tija. Lakini katika suala hili la fedha za Escrow...pesa hizo ni za IPTL.

Nahisi kuna mvutano wa makundi ya kisiasa. Lakini, ndugu zangu, kwa wanasiasa, muda huu ni muda wa kujipambanua. wale ambao watashindwa katika medani za ushindani katika mchezo huu rahisi, yamkini hata kuwa viongozi wa umma hawafai. Mimi niweke wazi, kama ningekuwa ni PM au AG nisingekubali kujiudhuru kwajambo lisilonihusu mimi wala kuuhusu umma, hata kama nimepokea fedha za ESCROW kwa maendeleo ya umma.

Mwenye taarifa tofauti atuletee hapa.... uzushi uwekwe pembeni, matatizo binafsi yawekwe pembeni...ebu tupeni raha ya kusoma vigezo na ukweli, si uzushi na kejeli. Suala hili limenipotezea muda kulifuatilia ili nione uhalisia ulipo...kumbe twajadili mipasho na uzushi. jambo hili si jema kwa ustawi wa jamii inayoheshimu utu, sheria na misingi ya utawala bora.






 
Now it is easy as pie, jamani ID ya informer ni ya Zitto Kabwe.

1.Anapenda kujitambulisha kuwa ni informer
2.Ametoa taarifa ambazo kwa namna yoyote chanzo ni chake yeye mwenyewe
3.sasa popote penye ID ya Informer ni zitto


Ok, sina kinyongo na maoni ya informer. Yeye ni mwanasiasa mwenye ushawishi. Kwasasa sitajibu hapa. Ingawa naona kabisa taarifa hizi zinajaribu kufunika hoja kuu ya msingi. Yaani kimantiki na kiuhalisia fedha za escrow ni za umma kwa sababu ipi? au ni za IPTL kwasababu zipi?

Naahidi kurudi na kutoa maoni yangu yasiyo na ushabiki

Kwa mara nyingine serikali kupitia viongozi na watendaji wake akiwamo Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wamedai kwamba kiasi cha Dola za Marekani milioni 250 zilizopaswa kuendelea kuwapo katika ‘Tegeta Escrow Account’ si mali ya serikali na hivyo si mali ya umma. Akaunti hiyo ilifunguliwa na serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) pamoja na kampuni ya Independent Power Limited (IPTL).

Kwa bahati mbaya sana viongozi wa serikali wamekuwa wakiendelea kurudia kuueneza huo uongo kwamba fedha hizo si mali ya umma. Inasikitisha pia kwamba vyombo vya habari vimekuwa navyo vikibeba na kusambaza huo uongo bila kuhoji na kuchunguza. Inashangaza sana pia asasi za kiraia nazo zimekaa kimya. Inatisha na kushangaa tena kuona wapinzani wakimwachia suala hili Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila, pekee wakati mapambano dhidi ya rushwa ni ajenda kuu ya wapinzani. Kafulila amekuwa akiendelea kuhoji suala hilo bungeni peke yake bila kupata kuungwa mkono na kupewa msaada wa aina yoyote kutoka kwa wenzake wa kambi ya upinzani bungeni.

Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) ilielekeza kuwapo kwa ukaguzi maalumu kwenye akaunti hiyo ya Tegeta escrow account iliyokuwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kwa kuwa ndani yake kulikuwapo fedha za umma. PAC haina sababu yoyote ya kufuatilia fedha za watu binafsi. Mwaka 2009 iliyokuwa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma (POAC) ilitoa maelekezo kwa BoT kutothubutu kutoa fedha hizo. Agizo hilo la POAC lilitokana na sababu kwamba fedha hizo zilikuwa ndani ya hesabu za Tanesco.

Akaunti ya ‘Tegeta escrow’ ilifunguliwa kutokana na kuwapo kutoelewana kuhusiana na gharama halisi na halali za umeme unaozalishwa na IPTL na kuuzwa kwa TANESCO. Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID) katika uamuzi wake wa Februari, 2014 ilitoa hukumu kuonyesha kwamba Tanesco walitozwa kiwango cha juu zaidi ya kilichopaswa kulipwa kwa IPTL. Kwa uamuzi huo ni dhahiri kwamba fedha zilizokuwa zimehifadiwa kwenye akaunti hiyo maalumu ya escrow zilipaswa kugawanywa kwa IPTL na Tanesco baada ya hesabu kufanyiwa marekebisho upya kwa viwango halali.

Hesabu za mwaka wa fedha ulioishia Disemba 2012 za Tanesco zinaonyesha wazi kwamba fedha hizo ni mali ya shirika hilo la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia mia moja. Fedha za kampuni ni suala la kisheria kama inavyobainishwa katika sheria ya kampuni ya mwaka 2002.

Kwa maelezo hayo na hoja hizo, inakuaje serikali ianze kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma? Hivi inawezekanaje kwa fedha za mtu binafsi zikaingizwa katika hesabu za shirika la umma linalomilikiwa na serikali kwa asilimia 100? Ni lini fedha hizo zimekoma kuwa za umma? Je ni baada ya baadhi ya watendaji wa serikali kula njama za kuzichukua fedha hizo kwa kushirikiana na ‘mwekezaji’ aliyechafuka kwa ufisadi duniani?

Serikali inadanganya waziwazi kudai kwamba fedha hizo si mali ya umma. Umma una haki ya kukumbushwa kwamba madai hayo yalitolewa pia katika lile sakata la ufisadi maarufu wa EPA unaofanana kwa kila hali na huu wa sasa wa ‘Tegeta Escrow’.

Hoja nyingine ni kwamba, Mbunge Kafulila alisema kwamba Jaji Utamwa wa Mahakama Kuu ya Tanzania hakutoa uamuzi wa kuchukuliwa fedha kutoka akaunti ya ‘Tegeta Escrow’. Nimepitia kwa makini hukumu ya Jaji Utamwa na kubaini kwamba hakuna popote alipotaja akaunti ya ‘Escrow’. Hata hivyo, nilipopitia muhstasari wa kikao kati ya TANESCO, IPTL na Wizara ya Nishati na Madini, ndipo kwa mara ya kwanza nikakuta wametafsiri uamuzi wa mahakama wakidai kwamba fedha zote za ‘Tegeta Escrow’ zipewe kampuni ya PAP (inamilikiwa kwa asilimia 50 na Harbinder Singh na 50% na Simba Trust iliyosajiliwa Australia). Hiki ndicho kikao kilichofanya maamuzi ya kuiba na kugawana wenyewe fedha hizo (Hukumu ya Jaji Utamwa na muhstasari wa kikao vinaambatanishwa).

Wote waliohudhuria kikao hicho kilichojipa mamlaka ya kutafsiri hukumu ya Mahakama Kuu, wanapaswa kuchunguzwa na kufikishwa mahakamani kwa mujibu wa sheria zilizopo. Inawezekana vipi uamuzi wa mahakama ukatafsiriwa na kikao cha Wizara? Muhstasari wa kikao hicho ndio uliowasilishwa Benki Kuu (BoT) kuhalalisha madai kwamba fedha hizo lazima zitolewa kutoka akaunti ya Escrow.

Fedha zinazohusiana na akaunti ya Escrow ni Dola za Marekani milioni 250, katia ya hizo Dola milioni 122 zilizokuwa BoT zimeshatolewa na kiasi kilichosalia Dola milioni 128 zitalipwa na Tanesco kutokana na fedha zake kwa madai ya kushindwa kulipa kwa wakati. Fedha zilizolipwa ni zile ambazo zimetoka Wizara ya Nishati na Madini ambayo kisheria ndio walipaswa kulipia gharama za uzalishaji umeme (capacity charge) fedha zilizotoka kwa walipa kodi.

Ikumbukwe kwamba uhamishaji wa asilimia 70 ya hisa za IPTL kwenda PAP umeambatana na nyaraka za kughushi kutokana na kutokuwepo kabisa kwa uthibitisho wa cheti halisi cha hisa (share certificate) kutoka kampuni ya Mechmar kwenda kampuni ya Piperlink. Nyaraka za TRA zinaonyesha kwamba hisa hizo (70%) ziliuzwa kwa Shilingi za Kitanzania milioni sita (6) tu. Na bado hakuna ushahidi kuonyesha kwamba uhamishaji huo wa hisa ulipata baraka za mamlaka husika kama inavyotakiwa na sheria za nchi.

Wakati huyo anayejiita mmiliki mpya wa IPTL aliposaini mkataba wa kuchukua fedha kutoka akaunti ya Escrow zilizokuwapo BoT, hakuwa mmiliki halali kisheria kwani kodi ililipwa siku moja baada ya wao kupokea fedha kutoka BoT. Sheria inataka kutolewa kwa cheti na Kamishna wa TRA kama uthibitisho kwamba kodi yote imelipwa ipasavyo (Sheria ya Fedha ya 2012 kifungu cha 29).

Ni nani wamiliki wengine wa kampuni ya PAP? Uchunguzi ni muhimu ukawalenga vigogo na wanasiasa wakubwa wakiwamo watendaji waandamizi wa Wizara ya Nishati na Madini.

Inapaswa tutafakari kuona kwamba Harbinder Singh aliyechukua fedha za Escrow, anamiliki vitalu vya mafuta na gesi kupitia kampuni iitwayo HydroTanz ambayo nayo imesajiliwa nchini Australia, ikiwa na anwani sawa na ya kampuni ya Simba Trust. Kitalu hicho cha mafuta kinaitwa ‘Mnazi Bay North’, jirani kabisa na ugunduzi mkubwa wa hivi karibuni mkoani Mtwara.

Tunatarajia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG), atafichua ukweli wa sakata hili na TAKUKURU itawafikisha mahakamani wahusika bila kujali nyadhifa zao serikalini.

Kauli ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kwamba kuna watu waliokula rushwa na kwamba nyaraka zinazotajwa ni karatasi za kuuzia vitumbua, ni kauli zenye kuonyesha kutapatapa kwa watendaji serikalini. Hakuna hata mahali pamoja ambapo nimemtaja mtu kuwa ni mwizi zaidi ya kuwasilisha hoja zinazohitaji majibu mwafaka na si matusi, vitisho na tuhuma za kuzusha. Nyaraka za TRA haziwezi kuwa za kufungua maandazi kama ambavyo hukumu ya Jaji wa Mahakama Kuu haiwezi kuwa karatasi za kufungia maandazi na badala yake ni nyaraka halali zinazohitaji maelezo kutoka kwa viongozi na watendaji wa serikali badala ya kuropoka na kuporomosha matusi.

Hali kadhalika, Bunge lina kila sababu kupitia sheria yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kulinda hadhi yake kutoka kwa watendaji kama Maswi ambao wanatoa matamshi ya kuonyesha kwamba chombo hicho ni chombo cha watu wasiofaa na kwamba watu wanaofaa wanazungumza nje ya Bunge. Maswi na wengine kama wana ushahidi wa rushwa dhidi ya mbunge ama yeyote hawapaswi kupayuka ovyo bali kwa nafasi zao wanaweza kuwasiliana na vyombo vya dola kama TAKUKURU na polisi ili wachunguze na kuchukua hatua kama ambavyo vinawachunguza wao.

Kauli ya Maswi kwamba “wanaume” hawazungumzi ndani ya Bunge si tu udhalilishaji wa chombo hicho bali pia inaashiria ugonjwa wa mfumo dume uliotawala miongoni mwa viongozi wetu kwa maana kwamba wanaume ndio wenye hadhi, uwezo na heshima na wanawake ni dhaifu na wasiostahili heshima. Tufumbue macho tuone na tuondoe hisia binafsi zenye kubebwa na itikadi, chuki na misimamo yetu ya kisiasa. Tuwe wazalendo ili tuweze kusimamia utaifa.


Zitto Kabwe




 
your money with who?,dai pesa za kwenu kwanza,ur money uliwasaidia kuzalisha umeme?

Leo jumapili nisingependa kuharibu siku yangu na either mtoto wa Chenge,Werema,Muhongo au Fisadi wa aina yoyote.

Ni pesa zetu zinatokana na bei kubwa ya umeme tunayotozwa na nyie manyang'au,majangili,wahujumu uchumi,wauaji wa uchumi wa taifa letu.

Soma alama za nyakati siyo wakati wake huu.Mlikulwa sana sasa ifike mwisho muadhibiwe.
 
1.Hon. A. Change 1.617bil
2.Wierina Investment Co 404Mil
3.Prof.Eudes Ruhangisa 404Mil
4.Mutabuzi & Advocates 404Mil
5.Rugonzibwa Theophil 404Mil
6.Dr.Enos Bukuku 161Mil
7.Placida Luoga 121Mil
8.Joyce Kyoba 80.8Mil
9.Hassan A.Matunga 80.8Mil
10.Eustadius Rutabingwa 80.8Mil
11.Shaban Gurumo 80.8Mil
12.Dr. James Diu 80.8Mil
13.Limbanga M Kinyero 40.2Mil
14.Hon.J.A.K. Mujulizi 40.4Mil
15.Fr.Romuald Rutagerekwa 40.4Mil
16.Philip Gerald Saliboko 40.4Mil
17.Miss Evelyin J. Rugemalira 808.5Mil
18.Alice Kemirembe Marco 80.8Mil
19.Rashid Abdallah Kupyasa 80.8Mil
20.Prof. Anna Tibaijuka 1,617Bil
21.Daniel A.N.Yona 40.4
22.Theophil Bwakea 161.7Mil
23.Steven Roman Urassa 161.7Mil
24.Paul Peter Kimiti 40.4Mil
25.Rev.Alphonce Twimaninn Ye Simon 40.4Mil
26.Bishop Method Kilaini 80.8Mil
27.Bishop Eusebius A. Nzigirwa 40.4Mil
28.Emmanuel Daniel Ole Naiko 40.4Mil
29.Fr.Hubert Rutashumururwa Rewabangira 40.Mil

Aisee List ni Ndefu nimechoka kuandika atleast hapo mtapata picha what type of People waliokula hii pesa.Jambo la kushangaza ni kwanini amount zao wengi zinaendana endana?
 
1.Hon. A. Change 1.617bil
2.Wierina Investment Co 404Mil
3.Prof.Eudes Ruhangisa 404Mil
4.Mutabuzi & Advocates 404Mil
5.Rugonzibwa Theophil 404Mil
6.Dr.Enos Bukuku 161Mil
7.Placida Luoga 121Mil
8.Joyce Kyoba 80.8Mil
9.Hassan A.Matunga 80.8Mil
10.Eustadius Rutabingwa 80.8Mil
11.Shaban Gurumo 80.8Mil
12.Dr. James Diu 80.8Mil
13.Limbanga M Kinyero 40.2Mil
14.Hon.J.A.K. Mujulizi 40.4Mil
15.Fr.Romuald Rutagerekwa 40.4Mil
16.Philip Gerald Saliboko 40.4Mil
17.Miss Evelyin J. Rugemalira 808.5Mil
18.Alice Kemirembe Marco 80.8Mil
19.Rashid Abdallah Kupyasa 80.8Mil
20.Prof. Anna Tibaijuka 1,617Bil
21.Daniel A.N.Yona 40.4
22.Theophil Bwakea 161.7Mil
23.Steven Roman Urassa 161.7Mil
24.Paul Peter Kimiti 40.4Mil
25.Rev.Alphonce Twimaninn Ye Simon 40.4Mil
26.Bishop Method Kilaini 80.8Mil
27.Bishop Eusebius A. Nzigirwa 40.4Mil
28.Emmanuel Daniel Ole Naiko 40.4Mil
29.Fr.Hubert Rutashumururwa Rewabangira 40.Mil

Aisee List ni Ndefu nimechoka kuandika atleast hapo mtapata picha what type of People waliokula hii pesa.Jambo la kushangaza ni kwanini amount zao wengi zinaendana endana?
Mbona hii ni kama bado ni orodha ya Mkombozi Bank tu. Tunataka na ile ya Stanbink
 
1. Pesa za Akaunti ya ESCROW ni za umma au watu binafsi?
Duru zilizoarifiwa zina maoni tofauti. Na hivi ndivyo wanavyosema.
Kutoka Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali (CAG) kwenda kwa Waziri Mkuu kuhusu ukaguzi wa Akaunti ya Escrow. “Pesa zilizomo katika Akaunti ya Escrow zaweza kuwa za umma au zaweza zisiwe za umma”.

2. Jaji Warioba: Katika mahojiano na gazeti la Raia Tanzania
“Fedha hizo ni za tozo za gharama ya uwekezaji. Hawakufika mahali ni kiasi gani, lakini kwa kuwa sasa wanakwenda kuchunguza, nina hakika mwisho itaonekana, sehemu kubwa ya fedha hizo zilikuwa ni za tozo za gharama za uwekezaji”.
“Hata hivyo wananchi wamefanywa waamini kwamba fedha zote zilikuwa za umma, huo ni mwelekeo wa kisiasa………”

3. Mwigulu Nchemba katika gazeti la Jambo Leo, Jumapili Desemba 7, 2014 amenukuliwa akisema “Bunge lilimwonea Maige” na anaendelea kusema kwamba, “hata kwa Prof. Muhongo, Tibaijuka lazima serikali iwe makini”. Mwigulu Nchemba ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, alikuwa mstari wa mbele akitaka waliohusika na kashfa ya akaunti ya Escrow wakiwemo mawaziri na wabunge wawajibishwe. Mwigulu anasema kulikuwepo na mvutano kati ya Bunge na Serikali kwani Serikali ilikuwa haiko tayari kufanya makosa kama ilivyokwisha kufanya makosa ya kuwatimua mawaziri katika sakata la Richmond na operesheni Tokomeza. Mwigulu anasema na tunamnukuu, “Hatutaki kufanya makosa tena kwa kufanya uamuzi kwa kufuata upepo badala ya uhalisia, kwani kule nyuma tumewahi kufanya hivyo na kuwawajibisha baadhi ya mawaziri bila ushahidi wala ukweli kuhusu tuhuma na kashfa zilizotokea kwenye wizara zao”.
Kwa maelezo hayo juu ni wazi kwamba suala la Escrow Akaunti lilichukuliwa kwa pupa na ndiyo maana wahusika wameanza kuhamisha nguzo za magoli.

4. David Kafulila: Maaskofu – kuhusu viongozi wa dini waliopata mgao wa fedha kutoka kwa Mkurugenzi wa VIP Engineering and Marketing, James Rugemalira alisema anaona hawana tatizo kwa kuwa , mamlaka zao haziwezi kushinikiza au kusaidia fedha hizo zitoke. Rushwa lazima iwe na vishawishi ambavyo vinasababisha mtu/watu wafanye kitu fulani, watu wa mamlaka kwa sababu mamlaka zao kwa namna moja au nyingine zilihusika kwa mfano Jaji, waziri, viongozi wa dini hakuna sheria ambayo wao wanaweza kuipindisha ili fedha ziweze kutoka alisema.

5. Wachimbaji wadogo:walioko karibu na Buhemba wamekerwa na mpango wa baadhi ya wabunge na wanaharakati kwa kumshinikiza Rais Jakaya Kikwete amfukuze kazi Waziri Muhongo.
Wachimbaji hao baadhi yao waliojitambulisha kwa majina ya Alez Nyamenda, Mabula Miloga (mwanza), Kinapo Mtazama, Peter Haule (Ruvuma), Mwaitenda Simon (Mbeya na Liwola Mpole (Morogoro) wamesema kwamba Waziri Muhongo ni mmoja kati ya Mawaziri ‘Majembe’ katika serikali ya Rais Kikwete.

6. Muluga: Anasema kwamba Waziri Muhongo ni hodari sana wa kazi ingawa amekuwa na tabia ya kusema ukweli, hivyo kujitengenezea maadui wengi. Maneno haya ya Maluga yaliungwa mkono na baadhi ya wadau ambao walisema kwamba, Rais Kikwete asikubali kuburuzwa na baadhi ya wabunge ambao wana ajenda zao za chuki, hasira na visasi dhidi ya Waziri huyo makini.
 
Kwa nini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ameshindwa kueleza iwapo fedha hizo ni za umma au za watu binafsi? Majibu sahihi yatasaidia kupunguza jazba miongoni mwa wananchi.
 
CAG yupo sahihi. Ni mpaka wafikie muafaka kuhusu ku over charge TANESCO ndiyo ijulikane kiasi gani zinaenda kwa matepeli na kiasi gani ni za umma. Kabla ya hilo ni za umma tu.
 
Siyo za umma, ndio maana walizisomba kwenye viroba, maboksi na sandarusi pale stanbinc bank. MOFO!!
 
Kwa nini Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali ameshindwa kueleza iwapo fedha hizo ni za umma au za watu binafsi? Majibu sahihi yatasaidia kupunguza jazba miongoni mwa wananchi.
Mna kazi ya kujisafisha, mama Tiba nae anapitapita huko kujisafisha. Once a traitor, always a traitor.
 
Back
Top Bottom