Tetesi: Fei Toto apokea Ofa ya Tsh Milioni 600 kutoka Simba SC kwa Mkataba wa miaka Mitatu

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Kiungo fundi wa Azam FC, Feisal 'Fei Toto' Salum inadaiwa amepokea ofa ya Tsh milioni 600 kutoka kwa miamba ya Soka, Simba SC, ikiwa ni malipo ya kusaini mkataba wa miaka mitatu. Simba wapo tayari kulipa kwa mafungu ya Tsh milioni 200 kila mwaka.

Soma: Mwigulu: Feisal ukishatoka Simba uje Singida

Fei Toto amekubali kujiunga na Simba akiona ni hatua kubwa katika safari yake ya kusakata Soka.
IMG_2335.jpeg
 
Kwa kiwango Cha Fei niseme TU hiyo hela ni ndogo sana labda kama Kuna kingine hatukioni ila ml 600 kwa Fei hapana
Fei ni Yaya Toure wa ligi yetu ni alama ya mpira wa tz move ya kwenda Simba ni nzuri sana kwa kiwango chake kuliko kuwa chamazi pasipokuwa na ndoto yoyote ila sio kwa hiyo hela Simba waweke angalau bill 1 na ilipwe haraka na kwa utulivu
 
Kama inshu ingekua kumshawishi mzee bakhresa isingekua kazi hadi ya kuhusisha viongozi wa serikali kwa sababu huyo mzee ni mwana Simba kindaki kindaki na aliwahi hadi kua muhasibu wa simba kama sijakosea, sidhani kama hiyo dili iko namna hiyo
 
Fei ni fundi wa boli anastahili kuweka rekodi ya mauzo kwa wachezaji wa ndani kwa sasa, 600m sio kiasi kidogo cha fedha ila kinaweza kupanda kupitia hata makubaliano kwenye baadhi ya vifungu kwenye mkataba mfano akiisaidia timu yake kufikia hatua fulani ya mafanikio (Ubingwa Ligi Kuu, Ubingwa michuano ya CAF) n.k
 
Hapo nadhani jambo litakuwa ni biashara tu ilivyokaa na masharti ya mkataba waliyoweka Yanga kuhusu Fei kuuzwa kwenye vilabu vya ndani, hayo mengine ni kuzunguka tu.
 
Fei ni fundi wa boli anastahili kuweka rekodi ya mauzo kwa wachezaji wa ndani kwa sasa, 600m sio kiasi kidogo cha fedha ila kinaweza kupanda kupitia hata makubaliano kwenye baadhi ya vifungu kwenye mkataba mfano akiisaidia timu yake kufikia hatua fulani ya mafanikio (Ubingwa Ligi Kuu, Ubingwa michuano ya CAF) n.k
Yah vyovyote vile anatakiwa kuweka statement kwenye uhamisho wake ili kuamsha hali ya michezo kwa vijana wenye ndoto hiyo hela ni ya Mzize sio Fei
 
Kiungo fundi wa Azam FC, Feisal 'Fei Toto' Salum inadaiwa amepokea ofa ya Tsh milioni 600 kutoka kwa miamba ya Soka, Simba SC, ikiwa ni malipo ya kusaini mkataba wa miaka mitatu. Simba wapo tayari kulipa kwa mafungu ya Tsh milioni 200 kila mwaka.

Soma: Mwigulu: Feisal ukishatoka Simba uje Singida

Fei Toto amekubali kujiunga na Simba akiona ni hatua kubwa katika safari yake ya kusakata Soka.
View attachment 3195088
Kitu ambacho amkijui ni mkataba wa fei ulivyo, ni ngumu sana kwa Azam kumuuza fei kwa sasa labda mpaka amalize mkataba wake ama avunje mkataba wake jambo ambalo ni gumu kwakuwa Azam anatakiwa ailipe yanga bilioni Moja kama itamuuza ndani ya nchi kwa timu yoyote Ile ama endapo itamtoa kwa mkopo kwa timu yoyote Ile ndani ya nchi, kwa maana iyo itawalazimu Azam wamuuze si chini ya bilioni Moja na nusu ili na wao wapate faida yao kwa kuwa bilioni Moja itaenda yanga,,sasa ni timu Gani bongo hapa itatoa iyo pesa kwaajili ya feitoto? Yanga wanajua kilichopo ndio maana wametulia tuli wanajua Kuna watu wanafurahisha genge tu na propaganda uchwara za milioni 600
 
Unatuletea story za vijiweni. Wewe uko Sikonge ndanindani huko, mkataba wa Feisal umeuonea wapi?
 
Fei ni fundi wa boli anastahili kuweka rekodi ya mauzo kwa wachezaji wa ndani kwa sasa, 600m sio kiasi kidogo cha fedha ila kinaweza kupanda kupitia hata makubaliano kwenye baadhi ya vifungu kwenye mkataba mfano akiisaidia timu yake kufikia hatua fulani ya mafanikio (Ubingwa Ligi Kuu, Ubingwa michuano ya CAF) n.k
Jamaa ni fundi kweli. Ila nashindwa kuelewa kwa nini akiwa timu fulani, timu hiyo haipati mafanikio.
 
Mil 600 - kwa mil 200 kila mwaka sindiki nzurinkwa fei.

Wampe 500mil cash mkononi - wamshawishi zingine zitakazobakia majaliwa ya muumba atakutana nazo mbele.
 
huyu fei ana kiwango gani mpaka alipwe million mia sita ! Naona simba wanataka kuchezea hela bure . kwa upande wangu naona mchezaji wa kawaida ndio maana hata timu za nje hazijatuma ofa
 
Back
Top Bottom