Feisal penalty/fidia ya kutokutumikia mkataba inamsubiria

Nakuchukulia kama genius siku zote kwa michango yako humu jamvini lakini leo nashangaa comment yako hii uliyoandika! Aisee kweli ushabiki wa hizi timu zinawatoa watu akili duh!

Yanga hawalazimishi Feisal abaki suala lipo wazi na hata TFF wameshaliweka wazi kwamba kilichobaki ni maongezi kati ya mwajiri(yanga) na mwajiriwa(Fei) kwa hili yanga yupo tayri kukaa chini na Fei kudiscuss kuhusu kuvunja mkataba wameshatoa wito sana kwa Fei aende mezani waongee,Fei hataki anataka kuvunja mkataba kienyeji kana kwamba yanga sio professional team ni kijiwe cha kahawa tu..Mpaka hapo utasemaje yanga wanamng'ang'ania?

Maamuzi ya TFF sio unfairly na hayajakaa kishabiki maana kwenye mkataba TFF ni third party tu kutoa maamuzi inategemea na maelewano kati ya pande mbili za kwanza..yangekuwa unfairly kamanYanga wangekuwa hawataki kukaa mezani kuvunja mkataba na Fei halafu wao wakasema mchezaji aende akamalizane na timu yake lakini kwa hili yanga yupo tayari kumalizana na Fei,Unfair iko wapi hapa? Ulitaka TFF ndio wavunje mkataba kati ya mwajiri na mwajiriwa? Ingekuwa hivi team zingebaki na wachezaji!? Yaan mtu aamke tu from abajalo fc let's say atake kuvunja mkataba ghafla kwa kulazimisha mkataba uvunjwe TFF bila kuwashirikisha abajalo Fc,wewe umeona wapi hii!? Kutakuwa na mpira kweli nchi hii?
Msimpotoshe dogo aisee aendelee kuliwa hela zake na wanasheria akae chini amalizane na Yanga ataachiwa kwa amani
Hizi timu zinafanyaga watu wawe matahira
Mfano madrid wanamtaka jude bellingham basi wamwambie ingia mitini alafu ukiwa ukiwa mitini nenda kwenye shirikisho la ujeruman la mpira waambie wavunje mkataba wako na dortmund sababu huipendi dortmund alafu chama cha mpira wavunje mkataba wake aende atakapo ambapo ni madrid kirahis hivyo

Ukinga ni tatizo kubwa sana Tanzania nyerere hakukosea
 
Weka ushabiki pembeni,mkataba unavunjwa kwa makubaliano ya waliongia mkataba tena kwa kufuata vipengele vya kuuvunja vilivyopo kwenye mkataba,fei mkataba alisaini na Yanga how aiombe tff ivunje mkataba ambao wao awakuwepo wakati unasainiwa,ok kwa mfano sasa tff ndio inavunvja mkataba kwa sababu zipi inauvunja,fei hajalipwa mshahara miezi 3,yan ni kitu gani fei alikosa kwenye mkataba wake ambacho kitasababisha mkataba uvunjwe,hapo ndio tff ilipomuambia arudi kwa aliongia nao mkataba au lah aende juu zaidi (CAS) kama anaona anaonewa
Mikataba kupelekwa katika mahakama ili ivunjwe inatokea pindi pande mbili zikakosa mahusiano mazuri.

TFF ni chombo ambacho kinawakutanisha mchezaji na Club kisha Club itaangalia demand yake kama fidia kwasababu sio upande ambao umetaka kuvunja mkataba

Nani kakuambia kutolipwa mshahara wa miezi mitatu ndio sababu pekee ya kumfanya mchezaji avunje mkataba?

Mchezaji sio mtumwa, nimekuwekea hapo vifungu vya sheria ambavyo vinampa idhini mchezaji kuondoka muda wowote eidha kwasababu au bila sababu

Kinachofanyika ni kwamba inapotokea utaratibu imekiukwa basi lazima kuwe na faini au adhabu ya kufungiwa kwa muda lakini kivyovyote vile mkataba hautaendelea
 
Yani kama hajafuata utaratibu basi ndio inafanya zoezi la kuvunjika mkataba liwe lepesi zaidi.

Na faini juu, ambapo kama Club inaweza kujipatia pesa kupitia makosa ya mchezaji.

Lakini hata baada ya maneno mengi kusemwa kuwa amevunja utaratibu na kuamua kufata utaratibu kuvunja mkataba bado maamuzi yaliotolewa yameonesha tatizo halikuwa kutofuata utaratibu

Bali tatizo ni Yanga hawataki mkataba uvunjwe, hivyo kwasababu yeyote ile huwezi kupatiwa unachokitaka
Umetanguliza maslahi na ushabiki zaidi.
Unazungumza kienyeji sana mkuu.
Hujawahi kufanya kazi ya mkataba?

Messi ameomba radhi kwa kuondoka kambini na kusafiri, sembuse huyu kijana kutoroka kwenda Dubai unataka aachiwe kienyeji?
 
Kwamba Yanga ashindwe gharama halafu Fei ndio atoe hela alipe😃,Fei ailipie yanga!?,mkuu umetumia nini leo
Sijasema Yanga hana uwezo wa kulipa.

Nimesema Yanga hana maslahi kupeleka kesi CAS hivyo hawezi kukubali kutoa hiyo hela.

Kwenye kesi ya Morrison Yanga ndio waliotoa hela kule CAS baada ya Simba kuona kesi hiyo kwao haina maslahi kwasababu hapa walikuwa wameshinda.

Sijui kama umeelewa
 
Mikataba kupelekwa katika mahakama ili ivunjwe inatokea pindi pande mbili zikakosa mahusiano mazuri.

TFF ni chombo ambacho kinawakutanisha mchezaji na Club kisha Club itaangalia demand yake kama fidia kwasababu sio upande ambao umetaka kuvunja mkataba

Nani kakuambia kutolipwa mshahara wa miezi mitatu ndio sababu pekee ya kumfanya mchezaji avunje mkataba?

Mchezaji sio mtumwa, nimekuwekea hapo vifungu vya sheria ambavyo vinampa idhini mchezaji kuondoka muda wowote eidha kwasababu au bila sababu

Kinachofanyika ni kwamba inapotokea utaratibu imekiukwa basi lazima kuwe na faini au adhabu ya kufungiwa kwa muda lakini kivyovyote vile mkataba hautaendelea
Ukisign mkataba wewe ni mtumwa kama ulikua hujui ndo ujue leo ndo ukiingia mkataba na kampuni yeyote ile wanakupangia hadi mda wa kuja na kuondoka kazin hujiaamulii wewe
Hata ruhusa unawaomba
 
Weka ushabiki pembeni,mkataba unavunjwa kwa makubaliano ya waliongia mkataba tena kwa kufuata vipengele vya kuuvunja vilivyopo kwenye mkataba,fei mkataba alisaini na Yanga how aiombe tff ivunje mkataba ambao wao awakuwepo wakati unasainiwa,ok kwa mfano sasa tff ndio inavunvja mkataba kwa sababu zipi inauvunja,fei hajalipwa mshahara miezi 3,yan ni kitu gani fei alikosa kwenye mkataba wake ambacho kitasababisha mkataba uvunjwe,hapo ndio tff ilipomuambia arudi kwa aliongia nao mkataba au lah aende juu zaidi (CAS) kama anaona anaonewa
Mkuu, mkataba sio lazima mukae chini mkubaliane muuvunje, pande moja tu inaweza amua bila pande nyingine kuridhia lakini kuna consequences zake kama fidia.

Pili unaposema kwanini ameenda TFF, pale mwanzo alipovunja mkataba TFF ilisema kuwa wao hawakushirikishwa hivyo hajafuata utaratibu maana kwa Tz mkataba utavunjika ikiwa chombo husika kitahusishwa. Rejea kanuni ya 74 ya TFF

Hivyo akaamua aombe idhini TFF kama ambavyo sheria zinasema lakini cha ajabu duhh
 
Umetanguliza maslahi na ushabiki zaidi.
Unazungumza kienyeji sana mkuu.
Hujawahi kufanya kazi ya mkataba?

Messi ameomba radhi kwa kuondoka kambini na kusafiri, sembuse huyu kijana kutoroka kwenda Dubai unataka aachiwe kienyeji?
Jamaa ushabiki mbele lakini hajui maslahi ambayo tff inatengeneza kwenye hii issue iwe fundisho kwa wachezaji wote wawe makini kipindi wakisaini mikataba yao maana kama fei angefanikiwa uhuni wake huu basi hata huko simba ingeweza kutokea,maana mikataba ingewezekana kuvunjwa wakati wowote ule mchezaji anapotaka pasipo kuzingatia kanuni za kimkataba
 
Sijasema Yanga hana uwezo wa kulipa.

Nimesema Yanga hana maslahi kupeleka kesi CAS hivyo hawezi kukubali kutoa hiyo hela.

Kwenye kesi ya Morrison Yanga ndio waliotoa hela kule CAS baada ya Simba kuona kesi hiyo kwao haina maslahi kwasababu hapa walikuwa wameshinda.

Sijui kama umeelewa
Kesi ya morrison mkataba wake na Yanga uliku una mapungufu ni vitu viwil tofauti
 
Hakuna kitu kama hicho kwenye mpira
 
Umetanguliza maslahi na ushabiki zaidi.
Unazungumza kienyeji sana mkuu.
Hujawahi kufanya kazi ya mkataba?

Messi ameomba radhi kwa kuondoka kambini na kusafiri, sembuse huyu kijana kutoroka kwenda Dubai unataka aachiwe kienyeji?
Usichanganye habari mbili ambazo hazina uhusiano.

Ishu ya Messi sio ya kimkataba ni kinidhamu.

Ishu ya kinidhamu wala usiende mbali mpaka Ufaransa wakati Azizi Ki na Morrison wametoka kwenye adhabu za kinidhamu mpaka kocha Nabi alishindwa kujizuia
 
Kesi ya morrison mkataba wake na Yanga uliku una mapungufu ni vitu viwil tofauti
Sijauhuisha mkataba wa Morrison na mkataba wa Feisali

Nimejaribu kumuelekeza circumstances ya Feisali kulipa hela CAS na kikwazo cha gharama ambacho kinaweza kumkwamisha kutokana na Yanga kutokuwa interested na hii kesi
 
Sijasema Yanga hana uwezo wa kulipa.

Nimesema Yanga hana maslahi kupeleka kesi CAS hivyo hawezi kukubali kutoa hiyo hela.

Kwenye kesi ya Morrison Yanga ndio waliotoa hela kule CAS baada ya Simba kuona kesi hiyo kwao haina maslahi kwasababu hapa walikuwa wameshinda.

Sijui kama umeelewa
Hapo nimekuelewa..

Tukija kwenye suala la kiini cha thread hii kwanini unaamin Fei anaonewa na wakat utaratibu upo wazi kwamba mkataba unaotaka kuvunjwa wahusika ni Yanga na Fei, ndio wanauwezo wa kuvunja mkataba, TFF sio wahusika wa mkataba huo hivo hawana uwezo wa kisheria kuvunja mkataba wakati wahusika hawajakaa kutaka kuvunja mkataba na kushindwana "Privy to contract".!? Maana suala lipo wazi Yanga anamtaka Fei aje wavunje mkataba Fei hataki sasa hapo anaonewaje?
 
Jamaa ushabiki mbele lakini hajui maslahi ambayo tff inatengeneza kwenye hii issue iwe fundisho kwa wachezaji wote wawe makini kipindi wakisaini mikataba yao maana kama fei angefanikiwa uhuni wake huu basi hata huko simba ingeweza kutokea,maana mikataba ingewezekana kuvunjwa wakati wowote ule mchezaji anapotaka pasipo kuzingatia kanuni za kimkataba
Umeongea vizuri sana.
Bila shaka hadi sasa hakuna club wala mchezaji aliyemtetea Faisal kwani ukweli ni kwamba alikosea kutaka kuvunja mkataba kienyeji.

Hata aende FIFA hii kesi hawezi kushinda.
Ni vyema tukaweka ushabiki pembeni tuongee ukweli.

Watanzania ni watu wa mihemko na blablaa tu, dunia iliyostaarabika inaheshimu mikataba.

Pili kama ulivyosema wachezaji wajitahidi wanaposaini mikataba waweke njaa kando, wasisaini mikataba kwa mkumbo au kama daftari la mahudhurio bali wasome waelewe au wawaajiri wanasheria watafsiri mikataba kabla hawajasaini.

Fei aweza kushitakiwa kwa kukiuka mkataba.
 
Hizi timu zinafanyaga watu wawe matahira
Mfano madrid wanamtaka jude bellingham basi wamwambie ingia mitini alafu ukiwa ukiwa mitini nenda kwenye shirikisho la ujeruman la mpira waambie wavunje mkataba wako na dortmund sababu huipendi dortmund alafu chama cha mpira wavunje mkataba wake aende atakapo ambapo ni madrid kirahis hivyo

Ukinga ni tatizo kubwa sana Tanzania nyerere hakukosea
Nashangaa sana aisee,halafu mashabiki wa Simba ndio wanajitoa ufahamu kuhusu suala hili utakuta wengine wanaelewa vizuri tu hili atajitahid apindishepindishe hili ionekana Yanga haifanyi Fair mpaka unajiuliza kwani hawa wana maslahi gani na hili suala!? Mwisho wa siku unakuja kutambua kwamba furaha yao ni kuona tu Yanga haina mchezaji mzuri kariba ya Feisali basiii hakuna lingine la maana

Suala ni moja kwamba pande mbili za kwanza zote zipo tyr kuvunja mkataba ila mmoja tu ndio kwa sababu ya ujinga wake anachelewesha mambo,sasa hapo third part(TFF) anaingiliaje hili suala na hakuna barua inayoonyesha kwamba pande mbili za kwanza wamekaa mezani ila wameshindwa kuvunja mkataba! Yaani privy to contract!?
 
Sijauhuisha mkataba wa Morrison na mkataba wa Feisali

Nimejaribu kumuelekeza circumstances ya Feisali kulipa hela CAS na kikwazo cha gharama ambacho kinaweza kumkwamisha kutokana na Yanga kutokuwa interested na hii kesi
Sijachanganya. Fei alitanguliza utovu wa nidhamu kwa kuondoka kambini kihuni...huo si utovu wa nidhamu?
Au kibongobongo ni sawa?
 
Hapo nimekuelewa..

Tukija kwenye suala la kiini cha thread hii kwanini unaamin Fei anaonewa na wakat utaratibu upo wazi kwamba mkataba unaotaka kuvunjwa wahusika ni Yanga na Fei, ndio wanauwezo wa kuvunja mkataba, TFF sio wahusika wa mkataba huo hivo hawana uwezo wa kisheria kuvunja mkataba wakati wahusika hawajakaa kutaka kuvunja mkataba na kushindwana "Privy to contract".!? Maana suala lipo wazi Yanga anamtaka Fei aje wavunje mkataba Fei hataki sasa hapo anaonewaje?
TFF ni chombo kinachosimamia maswala yote ya mpira hapa kwetu.

Kunapotokea migogoro ndio chombo cha kwanza kuanzia kabla mbeleni hujafika.

Kwanini Feisali kapeleka ombi la kuvunja mkataba TFF na sio kwenye Club yake?

Jibu ni kuwa, Yanga na Feisali kwa hatua hii wamepoteza mahusiano mazuri hivyo wao kwa wao hawawezi kuelewana.

TFF inakazi ya kuwakutanisha na kuhakikisha zoezi linafanyika na kutoa faida kwa pande zote mbili.

Yanga wao kama waajiri wataangalia ni kitu gani wanahitaji in return kwa mchezaji ambaye ameamua kuvunja mkataba. Kama ni kurudishiwa pesa ya usajili sawa, ila kivyovyote itakavyokuwa mkataba lazima uvunjike.
 
Nashangaa sana aisee,halafu mashabiki wa Simba ndio wanajitoa ufahamu kuhusu suala hili utakuta wengine wanaelewa vizuri tu hili atajitahid apindishepindishe hili ionekana Yanga haifanyi Fair mpaka unajiuliza kwani hawa wana maslahi gani na hili suala!? Mwisho wa siku unakuja kutambua kwamba furaha yao ni kuona tu Yanga haina mchezaji mzuri kariba ya Feisali basiii hakuna lingine la maana

Suala ni moja kwamba pande mbili za kwanza zote zipo tyr kuvunja mkataba ila mmoja tu ndio kwa sababu ya ujinga wake anachelewesha mambo,sasa hapo third part(TFF) anaingiliaje hili suala na hakuna barua inayoonyesha kwamba pande mbili za kwanza wamekaa mezani ila wameshindwa kuvunja mkataba! Yaani privy to contract!?
Mkuu mkataba sio lazima mkubaliane ndio mvunje.

Hyo ipo mutual agreement lakini ipo pia unilateral termination ambayo inawezekana kukawa na sababu au isiwepo na kama hakuna sababu fidia itahusika
 
Mikataba kupelekwa katika mahakama ili ivunjwe inatokea pindi pande mbili zikakosa mahusiano mazuri.
Kuna kikao chochote cha kuvunja mkataba kilichokaliwa kati ya yanga na Fei toto kinachoonyesha kwamba baada ya kukaa walikosa maelewano mazuri? Maana kwa hili suala hili third part ihusike mahakama/TFF ni lazima ijiridhishe kwamba hawa watu walikaa kwanza ila wakakosa maelewano mazuri kwenye hii ishu pamoja na kufuatwa kwa taratibu zote za kuvunja mkataba hapo sasa ndio inatoka notice ya Privy to contract kuendelea mbele zaidi,sasa kama Fei hataki kukaa na Yanga TFF itapata Validity gani ya kuamua kuingilia kuvunja mkataba!? Utaratibu ungekuwa hivyo ingekuwa vichekesho aisee
 
Back
Top Bottom