Feisal penalty/fidia ya kutokutumikia mkataba inamsubiria

Sijachanganya. Fei alitanguliza utovu wa nidhamu kwa kuondoka kambini kihuni...huo si utovu wa nidhamu?
Au kibongobongo ni sawa?
Feisali aliamza kuvunja mkataba kwa kurudisha pesa ya mishahara mitatu na hela ya usajili. Aliambatanisha na kifungu cha mkataba kinachompa authority ya kuvunja mkataba

Na alitoa na statement ya kuwaaga mashabiki.

Hata Club ilikiri kupokea hizo pesa.

Kwa hiyo kusema aliondoka kambini naweza kukubali, kwasababu aliondoka akiwa sio mchezaji wa Yanga.
 
Kwa hiyo TFF wanamuonea?
 
Ili uvunje makataba lazima Yanga wawe hawajamlipa mshahara na hawajamchezesha mechi kumi ndo angeweka hio milion 100 kama fidia ya kuvunja mkataba

Kama ameshavunja mkataba kwanin hana timu mpaka sahivi
Sikujua una upeo mdogo hivi
 
Kwa hiyo TFF wanamuonea?
Ndio 100% jana Fei na mawakili wake walikuwa wakitaka idhini ya kuvunja mkataba kwasababu, kwa TZ ili mkataba uvunjwe lazima chombo husika kihusishwe, sasa majibu waliyopewa leo haya lingani na lile ombi lao
 
TFF ni chombo kinachosimamia maswala yote ya mpira hapa kwetu.

Kunapotokea migogoro ndio chombo cha kwanza kuanzia kabla mbeleni hujafika.

Kwanini Feisali kapeleka ombi la kuvunja mkataba TFF na sio kwenye Club yake?

Jibu ni kuwa, Yanga na Feisali kwa hatua hii wamepoteza mahusiano mazuri hivyo wao kwa wao hawawezi kuelewana.

TFF inakazi ya kuwakutanisha na kuhakikisha zoezi linafanyika na kutoa faida kwa pande zote mbili.

Yanga wao kama waajiri wataangalia ni kitu gani wanahitaji in return kwa mchezaji ambaye ameamua kuvunja mkataba. Kama ni kurudishiwa pesa ya usajili sawa, ila kivyovyote itakavyokuwa mkataba lazima uvunjike.
Swali la msingi , Je ni lini Feisal ameenda yanga kama timu anavyomtaka, ili aje na majibu ya wapi wameshindwa kufikia mwafaka ,ya kwamba nilienda kukaa mezani na yanga ila ugumu ukaja hapa?
 
Umeongea vizuri sana.
Bila shaka hadi sasa hakuna club wala mchezaji aliyemtetea Faisal kwani ukweli ni kwamba alikosea kutaka kuvunja mkataba kienyeji.

Hata aende FIFA hii kesi hawezi kushinda.
Ni vyema tukaweka ushabiki pembeni tuongee ukweli.

Watanzania ni watu wa mihemko na blablaa tu, dunia iliyostaarabika inaheshimu mikataba.

Pili kama ulivyosema wachezaji wajitahidi wanaposaini mikataba waweke njaa kando, wasisaini mikataba kwa mkumbo au kama daftari la mahudhurio bali wasome waelewe au wawaajiri wanasheria watafsiri mikataba kabla hawajasaini.

Fei aweza kushitakiwa kwa kukiuka mkataba.
Angalia mawakili alioanza nao walimuacha sasa yuko na mawakili wa kutaka sympathetic public badala ya miongozo ya kisheria,then tufikirie tu sasa ni miezi 5 na toka tff na Yanga imuombe dogo aende kukaa nao ni miezi karibia 4 sasa lakini dogo anashindwa kupeleka barua ya kuomba kuvunja mkataba,shida iko wapi!hiyo barua si lzm aipeleke mwenyewe anaweza kumtuma hata boda boda aipeleke klabu pale
 
Kuna kikao chochote cha kuvunja mkataba kilichokaliwa kati ya yanga na Fei toto kinachoonyesha kwamba baada ya kukaa walikosa maelewano mazuri? Maana kwa hili suala hili third part ihusike mahakama/TFF ni lazima ijiridhishe kwamba hawa watu walikaa kwanza ila wakakosa maelewano mazuri kwenye hii ishu pamoja na kufuatwa kwa taratibu zote za kuvunja mkataba hapo sasa ndio inatoka notice ya Privy to contract kuendelea mbele zaidi,sasa kama Fei hataki kukaa na Yanga TFF itapata Validity gani ya kuamua kuingilia kuvunja mkataba!? Utaratibu ungekuwa hivyo ingekuwa vichekesho aisee
Haya mambo tuliyajadii sana hapa miezi ya katikati mwa hili sakata.

Kwanza unatakiwa ujue kuwa hakuna mkataba ambao hauvujiki.

Sheria zipo wazi sana, mkataba unaweza ukavunjwa kwa upande wowote iwe kwa sababu au bila sababu (whether the termination was with just cause or without just cause).

Kinachokuja kuleta utofauti ni consequences, kwa mtu aliyevunja kiholela kunakuwa na adhabu ya faini pamoja na kifungo. Lakini mkataba lazima uvunjike
 
Angalia mawakili alioanza nao walimuacha sasa yuko na mawakili wa kutaka sympathetic public badala ya miongozo ya kisheria,then tufikirie tu sasa ni miezi 5 na toka tff na Yanga imuombe dogo aende kukaa nao ni miezi karibia 4 sasa lakini dogo anashindwa kupeleka barua ya kuomba kuvunja mkataba,shida iko wapi!hiyo barua si lzm aipeleke mwenyewe anaweza kumtuma hata boda boda aipeleke klabu pale
Karume alijiondoa kumtetea naona ameombwa kurudi kumtetea.
Yule dada alivyo na mdomo kama dogo kaonewa angeongea sana
 
Ili uvunje makataba lazima Yanga wawe hawajamlipa mshahara na hawajamchezesha mechi kumi ndo angeweka hio milion 100 kama fidia ya kuvunja mkataba

Kama ameshavunja mkataba kwanin hana timu mpaka sahivi
Sikujua una upeo mdogo hivi
Hiyo ni termination with just cause kuna nyingine termination without just cause
 
Haya mambo tuliyajadii sana hapa miezi ya katikati mwa hili sakata.

Kwanza unatakiwa ujue kuwa hakuna mkataba ambao hauvujiki.

Sheria zipo wazi sana, mkataba unaweza ukavunjwa kwa upande wowote iwe kwa sababu au bila sababu (whether the termination was with just cause or without just cause).

Kinachokuja kuleta utofauti ni consequences, kwa mtu aliyevunja kiholela kunakuwa na adhabu ya faini pamoja na kifungo. Lakini mkataba lazima uvunjike
Mkuu unajaribu kuwaelewesha lakini ndio hvyo tena wamekaza mafuvu
 
TFF ni chombo kinachosimamia maswala yote ya mpira hapa kwetu.

Kunapotokea migogoro ndio chombo cha kwanza kuanzia kabla mbeleni hujafika.

Kwanini Feisali kapeleka ombi la kuvunja mkataba TFF na sio kwenye Club yake?

Jibu ni kuwa, Yanga na Feisali kwa hatua hii wamepoteza mahusiano mazuri hivyo wao kwa wao hawawezi kuelewana.

TFF inakazi ya kuwakutanisha na kuhakikisha zoezi linafanyika na kutoa faida kwa pande zote mbili.

Yanga wao kama waajiri wataangalia ni kitu gani wanahitaji in return kwa mchezaji ambaye ameamua kuvunja mkataba. Kama ni kurudishiwa pesa ya usajili sawa, ila kivyovyote itakavyokuwa mkataba lazima uvunjike.
Feisal kupeleka ombi la kuvunja mkataba TFF ndio tunarudi palepale ni kutokana na ufinyu wake wa kutokuelewa procedures maana TFF hawawezi kutoa maamuzi ya kuvunja mkataba wa First and second part ikiwa hakuna notice yoyote ya kushindwana ktk uvunjwaji wa mkataba husika kwa kufuata sheria..

Kilichofanyika ni kwamba Fei aliingiza hela kwenye account za Yanga na akawa analazimisha kuondoka alipokuwa anaitwa wakae wayaongee akakimbilia TFF,TFF ikasikiliza hoja zake ikawaita na yanga ambao wakatoa hoja zao wakaonekana wao wana hoja hukumu ikatoka kwamba Yanga ni mchezaji wao halali..

Yanga haikuwa na kinyongo ikamuita mezani akakimbilia tena TFF badala ya kukaa wayamalize na yanga wakati hadi kufikia hapo kamati haina Jurisdiction ya kusikiliza kesi husika kwakuwa hukumu ilishatoka "Functus officio" kilichobaki ni yeye amalizane na team yake mtu hataki kukutana na waajiri wake halafu unasema yanga wanamng'annia,unahitimisha kwa kusema wanamng'ang'ania wewe ulishawaona wamekaa kuvunja mkataba yanga ikawa haitaki chochote hata hiyo fidia ya kuvunja mkataba ikawa inamng'ang'ania tu!?

Cha muhimu aende kukutana nayanga tuone kama wanamng'ang'ania au vipi na kama watamng'ang'ania hapo sasa nitaungana na ww kukemea hili
 
Mkuu mkataba sio lazima mkubaliane ndio mvunje.

Hyo ipo mutual agreement lakini ipo pia unilateral termination ambayo inawezekana kukawa na sababu au isiwepo na kama hakuna sababu fidia itahusika
Sawa hiyo ya kutokukubaliana ipo,je unaweza kuvunja mkataba bila kukubaliana pasipo kufuata procedures sahihi?yaan ukurupuke tu bila kufuata taratibu wewe hii umeiona wapi!? Kazini kwako!? Kanisani? Kwenye taasisi gani!? Kwamba hufuati hatua sahihi unajiamulia tu kuvunja kihuni mkataba kisa sio lazima mkubaliane kuvunja?
 
Swali la msingi , Je ni lini Feisal ameenda yanga kama timu anavyomtaka, ili aje na majibu ya wapi wameshindwa kufikia mwafaka ,ya kwamba nilienda kukaa mezani na yanga ila ugumu ukaja hapa?
Palipo na mahusiano pana maelewano, hatua waliyofikia Yanga na Feisal hakuna tena hayo mahusiano mazuri.

Jaribio la Feisali kuvunja mkataba kwa kurudisha pesa ambapo alipewa mamlaka na mkataba wake wenyewe ndio sababu iliyopelekea mahusiano mazuri kati yake na Yanga kuvurugika
 
Sawa hiyo ya kutokukubaliana ipo,je unaweza kuvunja mkataba bila kukubaliana pasipo kufuata procedures sahihi?yaan ukurupuke tu bila kufuata taratibu wewe hii umeiona wapi!? Kazini kwako!? Kanisani? Kwenye taasisi gani!? Kwamba hufuati hatua sahihi unajiamulia tu kuvunja kihuni mkataba kisa sio lazima mkubaliane kuvunja?
Ngoja tuanze hizo procedure ni zipi ?
 
Back
Top Bottom