Feisal Salum (Fei Toto) na Yanga kimeeleweka, kutambulishwa Azam muda wowote

Feisal Salum (Fei Toto) na Yanga kimeeleweka, kutambulishwa Azam muda wowote

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
MWANASPOTI linajua kabla ya jua kuzama leo Jumatano Juni 7, Feisal Salum 'Fei Toto' atatambulishwa rasmi ndani ya Azam.

Licha ya Azam kufanya siri, lakini Mwanaspoti linajua klabu hiyo ilimalizana na Yanga jana jijini Dar es Salaam baada ya kikao kizito cha pande zote mbili.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwaomba Yanga kumaliza mgogoro na kiungo huyo Mzanzibari, ili mambo mengine yaendelee.

Fei aliingia kwenye mgogoro huo, baada ya kuvunja mkataba bila kuzingatia kanuni, hadi kesi kupelekwa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) bado Yanga ikawa kwenye upande wa haki.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia kwenye mitandao yetu na Gazeti la Mwanaspoti kesho Alhamisi Juni 8.

Chanzo: Mwanaspoti
 
Kuna msemo unasema "Ongea kwa upole ila beba fimbo kubwa". Yanga wameongeleshwa kwa upole tena wakapewa na ubwabwa ila wanajua kilichowasukuma kufanya maamuzi tena ya haraka ni fimbo kubwa.
 
Fei akienda Azam ntamshangaa sana, yaani atakua amekubali kuua career yake kwasababu ya maslahi ya muda mfupi let say miaka kama mitatu ivi

Unatoka Yanga unaenda Azam? Bora angetafuta club ya nje...
Tuchukulie Azam wampe mshahara wa milioni 8 kwa mwezi. Hiyo ni tofauti ya milioni 4 kwa mwezi kulingana na aliyokuwa anapata. Hiyo ni ziada ya milioni 48 kwa mwaka. Hiyo ni ziada ya milioni 100 ndani ya miaka 3. Na hapo nimeweka kiwango cha chini cha milioni 8 tu na pia sijaangalia mazagazaga mengine mengi tu atakayoweza kupewa na Azam.

Kwenda Azam au Simba bado ni upgrade kwa Feisal kimaslahi na hata kimpira.
 
Back
Top Bottom