Feisal Salum (Fei Toto) na Yanga kimeeleweka, kutambulishwa Azam muda wowote

Feisal Salum (Fei Toto) na Yanga kimeeleweka, kutambulishwa Azam muda wowote

Sijasema abaki Yanga, angepata timu ya nje ingesaidia career yake, sasa unatoka Yanga unaenda Azam?

Carrier ipi hapa bongo mzee? Kama nani labda? Hapa angalia pesa tu. Ang'ang'anie yanga kwenye maslahi madogo kwa lipi?
 
MWANASPOTI linajua kabla ya jua kuzama leo Jumatano Juni 7, Feisal Salum 'Fei Toto' atatambulishwa rasmi ndani ya Azam.

Licha ya Azam kufanya siri, lakini Mwanaspoti linajua klabu hiyo ilimalizana na Yanga jana jijini Dar es Salaam baada ya kikao kizito cha pande zote mbili.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwaomba Yanga kumaliza mgogoro na kiungo huyo Mzanzibari, ili mambo mengine yaendelee.

Fei aliingia kwenye mgogoro huo, baada ya kuvunja mkataba bila kuzingatia kanuni, hadi kesi kupelekwa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) bado Yanga ikawa kwenye upande wa haki.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia kwenye mitandao yetu na Gazeti la Mwanaspoti kesho Alhamisi Juni 8.

Chanzo: Mwanaspoti
Fei ashukiru Mama ni WA kwao vinginevyo
 
Sijasema abaki Yanga, angepata timu ya nje ingesaidia career yake, sasa unatoka Yanga unaenda Azam?
Nje ya nchi ni Kwa wachache na ndio maana mayele hato ondoka yanga..........

Unakumbuka MAKAMBO? Kibongo bongo..... Nje ni Kwa wachache sana tena DEDICATED PLAYER...
 
Kimaslahi sawa, kimpira ?
Kimpira pia. Hakuna mchezaji asiyetamani kuchezea Simba. Tukiweka ushabiki pembeni kihadhi tu Simba iko juu zaidi ya Yanga, huo ndiyo UKWERII.

Malengo ya Simba msimu ujao ni kuendelea kupambana kutoboa kwenye Champions League wakati uwezekano mkubwa malengo ya Yanga yakawa kuendelea kupambania Kombe la Shirikisho maana wameona kuna urahisi zaidi (kupanga ni kuchagua), kwa hiyo kimpira pia Simba ni option bora zaidi kwake.
 
Kauli ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan inaonekana kutoa matunda baada ya tetesi zinazoeleza kuwa Azam Fc na Yanga Sc wamemalizana juu ya usajili wa kiungo, Feisal Salum Abdallah (Fei Toto).Ni muda wa takribani miezi sita kiungo huyo amekuwa na mgogoro na klabu yake ya sasa ya Yanga juu ya kuvunja mkataba wake hatua iliyopelekea mshauri kadhaa kujadiliwa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Yanga kuwa upande wa haki juu ya madai ya mchezaji huyo.

D4FE0294-C82A-4BE7-A9DF-535C00606908.jpeg
 
Fei akienda Azam ntamshangaa sana, yaani atakua amekubali kuua career yake kwasababu ya maslahi ya muda mfupi let say miaka kama mitatu ivi

Unatoka Yanga unaenda Azam? Bora angetafuta club ya nje...
kama ulikua hujui hii balaa yote wameileta azam
 
Hii italeta viburi kwa wachezaji wengi kutokuheshimu mikataba
 
Back
Top Bottom