Feisal Salum (Fei Toto) na Yanga kimeeleweka, kutambulishwa Azam muda wowote

Feisal Salum (Fei Toto) na Yanga kimeeleweka, kutambulishwa Azam muda wowote

Niliandika hapa jana kuhusu hili.
 
MWANASPOTI linajua kabla ya jua kuzama leo Jumatano Juni 7, Feisal Salum 'Fei Toto' atatambulishwa rasmi ndani ya Azam.

Licha ya Azam kufanya siri, lakini Mwanaspoti linajua klabu hiyo ilimalizana na Yanga jana jijini Dar es Salaam baada ya kikao kizito cha pande zote mbili.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuwaomba Yanga kumaliza mgogoro na kiungo huyo Mzanzibari, ili mambo mengine yaendelee.

Fei aliingia kwenye mgogoro huo, baada ya kuvunja mkataba bila kuzingatia kanuni, hadi kesi kupelekwa kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) bado Yanga ikawa kwenye upande wa haki.

Kwa habari zaidi endelea kufuatilia kwenye mitandao yetu na Gazeti la Mwanaspoti kesho Alhamisi Juni 8.

Chanzo: Mwanaspoti
All the best kwake
 
Fei hakuna timu ya kumfanya akuze career yake bongo unless aongeze mshahara tu. Dogo mwenzie yule pale Sakho kaja na moto sana. Na Kila siku Simba ukiskia wameshinda bhas atatajwa kama mtu aliyenyunyiza. Yani ilikuwa mwendo wa minyunyizo tu... Sasa hivi hata wakimuacha pale Azam hawamachukui yule pimbi pamoja na kuwa na goli Bora afrika nzima mwaka ule... Hajifunzi tu?
 
Fei akienda Azam ntamshangaa sana, yaani atakua amekubali kuua career yake kwasababu ya maslahi ya muda mfupi let say miaka kama mitatu ivi

Unatoka Yanga unaenda Azam? Bora angetafuta club ya nje...
Ataenda nje akitokea hapo.

Subiri tuone mjataba wake utakuwaje, maana Azam ni wafanya biashara na wanawekeza fedha nyingi kwenye mpira.

Tusitegemee huruma kwenye biashara.
 
Fei akienda Azam ntamshangaa sana, yaani atakua amekubali kuua career yake kwasababu ya maslahi ya muda mfupi let say miaka kama mitatu ivi

Unatoka Yanga unaenda Azam? Bora angetafuta club ya nje...

huwa mnanishangaza sana huu mtazamo wenu. Yaani abaki yanga kwenye maslahi madogo kisa nini labda? Carrier?
 
Ataenda nje akitokea hapo.

Subiri tuone mjataba wake utakuwaje, maana Azam ni wafanya biashara na wanawekeza fedha nyingi kwenye mpira.

Tusitegemee huruma kwenye biashara.
Bibi unafeli wapi

Andika vizuri
 
Tuchukulie Azam wampe mshahara wa milioni 8 kwa mwezi. Hiyo ni tofauti ya milioni 4 kwa mwezi kulingana na aliyokuwa anapata. Hiyo ni ziada ya milioni 48 kwa mwaka. Hiyo ni ziada ya milioni 100 ndani ya miaka 3. Na hapo nimeweka kiwango cha chini cha milioni 8 tu na pia sijaangalia mazagazaga mengine mengi tu atakayoweza kupewa na Azam.

Kwenda Azam au Simba bado ni upgrade kwa Feisal kimaslahi na hata kimpira.
Kimaslahi sawa, kimpira ?
 
huwa mnanishangaza sana huu mtazamo wenu. Yaani abaki yanga kwenye maslahi madogo kisa nini labda? Carrier?
Sijasema abaki Yanga, angepata timu ya nje ingesaidia career yake, sasa unatoka Yanga unaenda Azam?
 
Watu wanaongea tu kishabik we mwenyewe kampun nyingine ikikutaka ikasema inakupa mpunga mara2/3 zaid ya unachopewa kwenye kampuni unayofanyia kazi utabaki??? Au mnamsema tu Fei mwache aende Ronaldo mwenyew yupo Arabun huko kwasababu ya mpunga mrefu,,,!
 
Back
Top Bottom