Acheni ujinga mchezaji hataki kuchezea timu yenu mnangangania wa nn kama sio uchawi?
Umetuchokoa na kutuchokonoa, umetuparura utopolo mpaka nimeamua nikujibu kirefu sana kama mkojo wa mwanzo asubuhi maana mikia wote nyie wote nchi nzima ni mbumbumbu.
Kaka sidhani kama we unajua boli! We itakuwa unaJua sana pool table au bao tu!
Pia nadhani una defect kwenye ubongo na unafeli kufikiri vizuri kuhusu mambo ya mpira! Nakiri Sijui uwezo wako wako wa kufikiri mambo mengine!
Mpira ni bizness kama bizness zingine kuuza mkaa, maji, unga, magari nk. Kwakuwa nadhani wewe umetoka familia ya wakulima na sio wafanyabiashara kama Mimi naamini hutaelewa kuhusu ishu ya Feitoto maana Si Kilimo ni biashara kwenye boli!! Mchezaji akipanda kiwango anapanda thamani anauzwa bei kubwa club iliyomkuza nayo Ina benefit!
Yanga haimuhitaji Tena Feitoto Wala haimng'ang'anii . Aziz Ki na Mudathir sijui Sureboy , Bigirimana, Yusuph Athumani, Clement, Morisson na Farid mara Huku Kuna Zawadi Mauya na Denis Nkane tayari wote hawa amewapa chance waoneshe viwango. Yanga imeziba pengo lake tayari si unaona unbeaten ziko pale pale na Feitoto Yuko JKU kule mchambawima ? Au umejitoa ufahamu Mkuu?
Yanga haimng'ang'anii Feitoto Bali timu inataka kupiga pesa zake tu maana Feitoto ni Mtoto wetu inapaswa auzwe kihalali mezani sio kihuni kihuni under influence ya shisha au whiskey!!
Inatakiwa tu Feitoto awe mpole alete matajiri uchwara wake mezani utopoloni tuwalipue dau lake la uhamisho ni one billion thamani yake, dogo aende!
Mkataba wake Feitoto waliuweka hapa JF nikausoma taratibu nikaona unasema akitaka kuvunja Feitoto atalipa ada ya usajili na mishahara Mitatu mkataba ukaongeza Katika hicho kifungu "Feisal avunje mkataba ikiwa tu kukiwa na sababu za maana kufanya hivyo" na bahati mbaya sababu hizo za maana kuvunja mkataba hazikutajwa kwenye mkataba. Maana yake ni kuwa
1. Kipengele alichotumia Feitoto Ili kuvunja mkataba na Yanga hakukielewa maana hatakiwi kuishia tu kuweka mzigo mezani Bali pia akae Mezani kuongea na uongozi na kuwaeleza "sababu za maana" za kuvunja mkataba na uongozi uzielewe na uzikubali!
2.Yanga na TFF Wana loophole ya kukataa sababu zote atakazosema Feitoto kwa kusema "si za maana" na watakuwa sahihi mbele ya sheria maana sababu za maana za kuvunja mkataba hazijulikani!
3. Feitoto alipiga zake shisha tu likakolea akaweka mzigo mezani akaandika barua kutuaga mashabiki wa utopolo akatimka Wala hakusema sababu za kuvunja mkataba na hakuongea na uongozi. Uhuni asilimia mia plus!
4. Feitoto Hana sababu ya maana ya kuvunja mkataba. Tukifikiria sababu hizo ni kama kutolipwa mishahara, kutotibiwa akiumia au kutopangwa!! Dogo Hana sababu ya maana ya kuvunja mkataba.
Kwa wanasimba wote habari njema ni kuwa maana yake Feitoto atasalia utopoloni mpaka apate "sababu ya maana" ya kuvunja mkataba na waliodhani Feisal ndo moyo wa Yanga wamekosea sana Yanga imejaza vipaji milioni hatufeli makombe yako pale pale hata mkimvuruga Feitoto amerudi JKU!
Mimi Zuga nilianza kubeba viatu vya wachezaji Ili kuingia uwanjani kucheki ligi kuu miaka 50 iliyopita nikiwa Mtoto mdogo sana nisikilize vizuri nimeona kwa macho yangu timu za ligi kuu zikiroga klabuni kabla ya kwenda uwanjani nakwambia laivu Ngoma ya kitoto haikeshi, Feisal Simba sijui Azam wamemrubuni kwa pesa kwa vile yeye mwenyewe ameona vipaji na vigimbi vya wenzake na ameingia baridi na kushindwa kuhimili presha ya kugombania namba , Bado ana akili za kitoto.
Utopolo tunajua mikia mnakaribia kufa kwa presha na wivu na kurubuni wachezaji wetu Ili mtuharibie sherehe kwa vile tu kinawauma sana sie utopolo tuna possess boli , tumeingia makundi shirikisho CAF kwa kuwafunga waarabu kwao, tunaongoza ligi tukisubiri Simba mpigwe mechi moja ambayo hamtapewa penati na timu pinzani kucheza pungufu!! Kombe la NBC mmeona mmelikosa mmeamua kumwaga mboga na ugali!!
Utopolo tunajua Simba mnakaribia kufa kwa kihoro kwa kuudukua mpango wa Yanga kubeba makombe yote ya bara kwa misimu mitano na utaratibu wetu wa kuhesabu unbeaten 100 maana pale tulipopanga sherehe ya kugawa keki 50 uwanjani kwa kufikisha unbeaten 50 Mikia mlienda Mbeya kabla ya mechi na mkafanikiwa kuharibu sherehe japo msichokijua ni kuwa mliongeza petrol kwenye moto Na kubadili hesabu ya unbeaten 50 kuwa unbeaten 100!
Feisal akae tu home hadi 2024 mkataba utaisha ataenda huko Azam sijui Simba. Nyie la Saba B Endeleeni kumpotosha Feitoto tu sie wenye madigirii yetu tumebukua ishu ya Feikubwa tunawafafanulia alichokosea hamuelewi!