Feitoto agoma kurudi Uto, ataka review ya hukumu ya TFF

Feitoto agoma kurudi Uto, ataka review ya hukumu ya TFF

Kiungo wa kimataifa wa Tanzania Feisali Salum Abdallah “Feitoto” amewasilisha juzi maombi yake kwenye ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF akitaka Kamati ya hadhi na haki za wachezaji na wanachama ipitie upya shauri lake na irekebishe hukumu yake na kumpa haki.

Feisali alivunja mkataba na Yanga SC tarehe 22/12/2022 kwa maandishi akitumia kipengele namba 14.7 cha mkataba baina yake na Yanga ambapo ilimpasa kuilipa klabu pesa ya usajili aliyopokea pamoja na mshahara wa miezi 3 tu.

Yanga SC walipinga jambo hilo na kulalamika TFF ambako lilipelekwa kwenye Kamati husika na shauri kusikilizwa hadi hukumu kutoka ambako Kamati ilimuamuru Feisali kubaki Yanga.

Mchezaji anaona Kamati haikufanya sawasawa na haikujielekeza kwenye hoja (issues) ambazo zililetwa mezani kwa pande zote mbili badala yake ilisema yeye anapaswa kurudi Yanga kitu haukuwa hoja.

Zaidi upande wa mchezaji wanaamini pia kwamba Kamati haikuwa sahihi kusema Feisali ni mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba ambao Fei ameuvunja na Yanga pia wanajua amevunja ila wao kama partners hawakushirikishwa na ndiyo hoja yao ilipo.

Walitegemea kamati ijielekeze kama namna alivyovunja mkataba Fei ilikuwa sahihi au sio sahihi.

Kama sahihi mkataba uvunjike na kama sio sahihi mchezaji aadhibiwe na sio kumlazimisha kurudi sehemu alikoshindwa kufanya kazi kwa sababu ambazo alizisema wazi mbele yao alipohojiwa.

Wanasisitiza mchezaji sio mtumwa wa kulazimishwa kufanyakazi mahala ambapo anaona mazingira yake magumu na sio rafiki tena.

Upande wa mchezaji wanalaumu kamati kushindwa kutoa adhabu kwenye hukumu yake kitu ambacho wanakiona pia sio cha kawaida kwa mtu aliyekosea, badala ya kumpa adhabu unamlazimisha kurudi alikoshindwa kuishi.

Wanahoji au kamati inaamini kumrudisha Yanga ni kumuadhibu pia?

Wana imani Kamati ina watu weledi, wajuzi wa mambo na wabobezi ambao wanazijua sheria, kanuni, taratibu zinazitumika na FIFA Dispute resolution chamber pamoja na CAS

My Take
Hivi huyu Feitoto ameondoka na figo ya Utopolo? Acheni roho ya kimasikini
Sio kiungo wa kimataifa ni kiungo wa Kitaifa. Hajawahi kusajiliwa na timu nje ya Tanzania
 
Je kama kuomba marejeo ndiyo sehemu ya hatua za kwenda CAS? Kamati inakumbushwa kujikita kwa hoja iliyokuwepo ambayo ni Je uvunjaji wa mkataba ulifuata taratibu ama la? Na kama alivunja mkataba bila taratibu kufuatwa basi aadhibiwe kwa kosa hilo.Kumlazimisha kurudi Yanga siyo sehemu ya hoja iliyopelekwa mbele ya Kamati.
Umeiona barua ya malalamiko ya Yanga juu ya fei kwenda tff? Nan alimstaki mwenzie? Yeye fei apeleke malalamiko yake kwa kuistaki yanga then ftt wakakaa wamjadili, kesi ya kwanza ilishaisha anatakiwa arudi yanga maana bado ana mkataba hadi 2024, apeleke kesi ya kwake sasa na vifungu vya kumtetea kuvunja mkataba kingumbalu
 
... shukran kwa ufafanuzi. Changamoto nyingine za wachezaji wetu hawa ni shule na uelewa mdogo. Sina hakika kama alipokuwa anasaini huo mkataba alifahamu maana na atahri zake sembuse hata kuusoma na kuuelewa kabla ya kusaini.
Uko sahihi kabisa. Ukosefu wa elimu juu ya mikataba ni tatizo kwa wachezaji wetu. Dogo alikuwa ana uwezo wa kukaa mezani na klabu yake, na kulimaliza hili suala kwa njia rafiki.

Aidha kwa kuongeza mkataba na hivyo mshahara wake pia kuongezeka! Kusubiria mkataba wake uishe mwaka wa kesho 2024 na hivyo kuondoka kama free agent! Au timu inayomtaka kukaa mezani na Yanga jwa lengo la kumsajili.

Ila yeye aliamua kuchagua njia ya mkato na ya kihuni, ili mwisho wa siku timu na viongozi wake waendelee kudharauliwa kama ilivyotokea kwenye kesi ya Morrison.

Katika mazingira kama haya, unaona kabisa anajitesa tu yeye mwenyewe. Maana hata wale wahusika waliompa hizo pesa, wameishia tu kujificha ili kuwekeoa rungu la kufungiwa/kupigwa faini na TFF.
 
Utopolo ni kikundi cha wachawi ndo kilicho sababisha mpaka sasa ngasa ni masikini baada ya kuharibu dili ambalo linge mpatia milion 300
Watu tunajadili mambo ya msingi, wewe unaleta story za uchawi! Huku ukisahau ni mwaka wa jana tu timu yako ya simba ilipigwa faini ya dola elfu 10 na CAF kutokana na vitendo vyake vya kishirikina uwanjani kule Afrika ya Kusini.

Halafu aliyekuambia Mrisho Ngasa ni maskini ni nani? Na kuna uhusiano gani wa huo umaskini wake na hilo dili la milioni 300?

Yaani mtu achezee Kagera Sugar, Yanga, Azam, simba, Afrika ya Kusini, Ndanda, nk tangu 2004 huko! Halafu from nowhere tu awe maskini kwa sababu alibaniwa dili la milioni 300!

Kweli Rage alikuwa sahihi kuwaita mbumbumbu.
 
Sio kwamba anapoteza muda ila Wanasheria wake ni Mbumbumbu mno, Huwezi kukata rufaa au kuomba review kwenye mamlaka iliyotoa uamuzi. Ilitakiwa aombe mwenendo wa shauri ili aende kukata rufaa kwenye ngazi inayofuata yaani CAS. Halafu hata sababu ambazo Wanasheria wake wanazitumia katika ku-justify review ni za kilimbukeni zaidi. Huwezi kusema mchezaji hapendi tena kuchezea timu fulani, wanatakiwa wajikite kwenye masuala yaliyovunjwa kwenye Mkataba kati ya Yanga na Feisal.
Wewe Mwanasheria kama Mimi utayaona hayo lakini waliofeli hawawezi kujua hayo. Sababu ya rufaa "Ni Kwa nini Kamati haikumwadhibu Feisal kama ilimkuta na kosa?" Kweli kabisa Huyo unasema ni Mwanasheria? Wapi Yanga iliomba Kamati iangalie kama Feisal kavunja sheria? Yanga walisema mchezaji wao haonekani na bado ana mkataba nao, na Kamati ikamuita mwajiriwa kumuuliza Kwa nini huendi kazini? Akasema Mimi nilishaacha kazi. Kamati ikaangalia ushahidi wa pande zote ikasema Rudi Kwa mwajiri wako kazi haiachwi kihuni namna hiyo. Hivyo mwenye jukumu la kumwadhibu Feisal ni Yanga siyo Kamati.
 
Hivi kwann mnaendeshwa na mahaba hata sehemu zisizostahiki.

Yaani unakubali kuwa hakuvunja mkataba kihalali hivyo aadhibiwe lakini unasahau kuwa mkataba usiovunjwa kihalali Ni mkataba usiovunjwa.

Unakubali kabisa FEI anastahili kuadhibiwa ila unalazimisha kuwa mkataba umevunjwa. Sasa kama kavunja mkataba kwa hivyo vifungu vyako unavyotaka kwann unataka aadhibiwe?

We unajua mambo ya mikataba hivi kweli?

Umewahi kupanga nyumba? Kwahiyo mwenye nyumba anaweza kuamka asubuhi tu akakutolea vitu nje na Kisha kusema kavunja mkataba alafu serekali ya mtaa au ukienda mahalamani waseme ni kweli mwenye nyumba alikosea hakuvunja mkataba vizuri kwa hiyo anaadhibiwa kulipa fine ila wewe utajijua huko uliko kama vitu viko barabarani au chini ya mti haijalishi mradi ameshaadhibiwa kulipa fine

Hebu eleweni kitu kimoja aisee MKATABA USIOVUNJWA KIHALALI NI MKATABA USIOVUNJWA NA UNAENDELEA VILE VILE ULIVYOKUWA.

Mnamdanganya huyu mtoto, mtaharibu future yake. Nyie mko makwenu na makazini kwenu mnamdanganya huyu dogo wakati mpira ndio kazi yake
Jambo la Kisheria unaongea na Wafamasia? Kuna Waandisi wa barabara humu wanalazimisha kuwa wanasheria.
 
Je kama kuomba marejeo ndiyo sehemu ya hatua za kwenda CAS? Kamati inakumbushwa kujikita kwa hoja iliyokuwepo ambayo ni Je uvunjaji wa mkataba ulifuata taratibu ama la? Na kama alivunja mkataba bila taratibu kufuatwa basi aadhibiwe kwa kosa hilo.Kumlazimisha kurudi Yanga siyo sehemu ya hoja iliyopelekwa mbele ya Kamati.
Waliopeleka shitaka TFF ni Feisal au Yanga? Mbona mnajitoa ufahamu? Yaani Kamati imekubaliana na hoja ya mpeleka shitaka halafu mnataka ihukumu ambacho haijaombwa kwenye madai?
 
Kiungo wa kimataifa wa Tanzania Feisali Salum Abdallah “Feitoto” amewasilisha juzi maombi yake kwenye ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF akitaka Kamati ya hadhi na haki za wachezaji na wanachama ipitie upya shauri lake na irekebishe hukumu yake na kumpa haki.

Feisali alivunja mkataba na Yanga SC tarehe 22/12/2022 kwa maandishi akitumia kipengele namba 14.7 cha mkataba baina yake na Yanga ambapo ilimpasa kuilipa klabu pesa ya usajili aliyopokea pamoja na mshahara wa miezi 3 tu.

Yanga SC walipinga jambo hilo na kulalamika TFF ambako lilipelekwa kwenye Kamati husika na shauri kusikilizwa hadi hukumu kutoka ambako Kamati ilimuamuru Feisali kubaki Yanga.

Mchezaji anaona Kamati haikufanya sawasawa na haikujielekeza kwenye hoja (issues) ambazo zililetwa mezani kwa pande zote mbili badala yake ilisema yeye anapaswa kurudi Yanga kitu haukuwa hoja.

Zaidi upande wa mchezaji wanaamini pia kwamba Kamati haikuwa sahihi kusema Feisali ni mchezaji wa Yanga kwa mujibu wa mkataba ambao Fei ameuvunja na Yanga pia wanajua amevunja ila wao kama partners hawakushirikishwa na ndiyo hoja yao ilipo.

Walitegemea kamati ijielekeze kama namna alivyovunja mkataba Fei ilikuwa sahihi au sio sahihi.

Kama sahihi mkataba uvunjike na kama sio sahihi mchezaji aadhibiwe na sio kumlazimisha kurudi sehemu alikoshindwa kufanya kazi kwa sababu ambazo alizisema wazi mbele yao alipohojiwa.

Wanasisitiza mchezaji sio mtumwa wa kulazimishwa kufanyakazi mahala ambapo anaona mazingira yake magumu na sio rafiki tena.

Upande wa mchezaji wanalaumu kamati kushindwa kutoa adhabu kwenye hukumu yake kitu ambacho wanakiona pia sio cha kawaida kwa mtu aliyekosea, badala ya kumpa adhabu unamlazimisha kurudi alikoshindwa kuishi.

Wanahoji au kamati inaamini kumrudisha Yanga ni kumuadhibu pia?

Wana imani Kamati ina watu weledi, wajuzi wa mambo na wabobezi ambao wanazijua sheria, kanuni, taratibu zinazitumika na FIFA Dispute resolution chamber pamoja na CAS

My Take
Hivi huyu Feitoto ameondoka na figo ya Utopolo? Acheni roho ya kimasikini
Wewe una matatizo unabehave Kike! Wewe ni mnazi wa simba, iweje ufuatilie masuala ya Yanga? Kwa Mwanaume hii ni hatari.

Nikusadie, mfano ukiachana na mke Acha kumfuatilia la sivyo utapata Msongo wa mawazo mwisho uuee! Kama wewe ni mshabiki wa simba, fuatilia ya simba na ya Yanga waachie wana yanga!
 
Roho mbaya ya viongozi iliyomfikisha hapo Feisal.

Morrison naskia anapokea 23M halafu kwa mwezi anacheza mechi mbili nazo hizo anatokea sub hachezi dakika 60

Aziz Ki inadaiwa anapokea 26M ila at least huyu anacheza mechi nyingi japokuwa kihalisia yeye na Feisal kwenye ubora sioni utofauti.

Hao wote wamemzidi Feisal mara 7 mshahara, is that fair?
Kama feisal aliona anacholipwa ni kidogo kulingana na thamani yake alitakiwa kufuata njia sahihi sio kwa alichokifanya.. pale liverpool chamberlain alikua analipwa mshahara mkubwa kuliko mane ila ushawahi kusikia mane kagomea mazoezi? Si walikaa mezani wakayamaliza
 
Kuomba review ni sawa kabisa na hizo hoja watatumia cas pale wakishindwa review Yao.
Kilichofanyika mwanzoni ni uhuni TU na mawakili wa Feitoto wanataka kuonyesha huo ni uhuni wao
 
... hivi Yanga wamemkosea nini huyu kijana? Mbona alikuwa anawabeba sana; nini kimetokea ghafla wameshindwana?
Amekula hela ya watu huko ukoloni Kwa sharti la kumtukana bake wenyewe wanaitaka wanamuendesha wanavyotaka wao. Makolo walidhani wataitoa yanga kwenye reli, kumbe sasa ndio wameitia hasira yanga. Sasa hivi tunasajiri yeyote, Juni tunamleta adabayor

Sent from my M10_Max using JamiiForums mobile app
 
Mashabiki wa simba mchukueni tu Feitoto maana mmeshupalia sana.

Nyie simba na ndugu yenu azam fuateni taratibu mumchukue fei wenu...Mkileta figisu figisu mtamuumiza dogo maana hajielewi mmeshamrubuni na mijihela kwahiyo kawa mwehu.
 
Acheni ujinga mchezaji hataki kuchezea timu yenu mnangangania wa nn kama sio uchawi?
Umetuchokoa na kutuchokonoa, umetuparura utopolo mpaka nimeamua nikujibu kirefu sana kama mkojo wa mwanzo asubuhi maana mikia wote nyie wote nchi nzima ni mbumbumbu.

Kaka sidhani kama we unajua boli! We itakuwa unaJua sana pool table au bao tu!

Pia nadhani una defect kwenye ubongo na unafeli kufikiri vizuri kuhusu mambo ya mpira! Nakiri Sijui uwezo wako wako wa kufikiri mambo mengine!

Mpira ni bizness kama bizness zingine kuuza mkaa, maji, unga, magari nk. Kwakuwa nadhani wewe umetoka familia ya wakulima na sio wafanyabiashara kama Mimi naamini hutaelewa kuhusu ishu ya Feitoto maana Si Kilimo ni biashara kwenye boli!! Mchezaji akipanda kiwango anapanda thamani anauzwa bei kubwa club iliyomkuza nayo Ina benefit!

Yanga haimuhitaji Tena Feitoto Wala haimng'ang'anii . Aziz Ki na Mudathir sijui Sureboy , Bigirimana, Yusuph Athumani, Clement, Morisson na Farid mara Huku Kuna Zawadi Mauya na Denis Nkane tayari wote hawa amewapa chance waoneshe viwango. Yanga imeziba pengo lake tayari si unaona unbeaten ziko pale pale na Feitoto Yuko JKU kule mchambawima ? Au umejitoa ufahamu Mkuu?

Yanga haimng'ang'anii Feitoto Bali timu inataka kupiga pesa zake tu maana Feitoto ni Mtoto wetu inapaswa auzwe kihalali mezani sio kihuni kihuni under influence ya shisha au whiskey!!

Inatakiwa tu Feitoto awe mpole alete matajiri uchwara wake mezani utopoloni tuwalipue dau lake la uhamisho ni one billion thamani yake, dogo aende!

Mkataba wake Feitoto waliuweka hapa JF nikausoma taratibu nikaona unasema akitaka kuvunja Feitoto atalipa ada ya usajili na mishahara Mitatu mkataba ukaongeza Katika hicho kifungu "Feisal avunje mkataba ikiwa tu kukiwa na sababu za maana kufanya hivyo" na bahati mbaya sababu hizo za maana kuvunja mkataba hazikutajwa kwenye mkataba. Maana yake ni kuwa

1. Kipengele alichotumia Feitoto Ili kuvunja mkataba na Yanga hakukielewa maana hatakiwi kuishia tu kuweka mzigo mezani Bali pia akae Mezani kuongea na uongozi na kuwaeleza "sababu za maana" za kuvunja mkataba na uongozi uzielewe na uzikubali!

2.Yanga na TFF Wana loophole ya kukataa sababu zote atakazosema Feitoto kwa kusema "si za maana" na watakuwa sahihi mbele ya sheria maana sababu za maana za kuvunja mkataba hazijulikani!

3. Feitoto alipiga zake shisha tu likakolea akaweka mzigo mezani akaandika barua kutuaga mashabiki wa utopolo akatimka Wala hakusema sababu za kuvunja mkataba na hakuongea na uongozi. Uhuni asilimia mia plus!

4. Feitoto Hana sababu ya maana ya kuvunja mkataba. Tukifikiria sababu hizo ni kama kutolipwa mishahara, kutotibiwa akiumia au kutopangwa!! Dogo Hana sababu ya maana ya kuvunja mkataba.

Kwa wanasimba wote habari njema ni kuwa maana yake Feitoto atasalia utopoloni mpaka apate "sababu ya maana" ya kuvunja mkataba na waliodhani Feisal ndo moyo wa Yanga wamekosea sana Yanga imejaza vipaji milioni hatufeli makombe yako pale pale hata mkimvuruga Feitoto amerudi JKU!

Mimi Zuga nilianza kubeba viatu vya wachezaji Ili kuingia uwanjani kucheki ligi kuu miaka 50 iliyopita nikiwa Mtoto mdogo sana nisikilize vizuri nimeona kwa macho yangu timu za ligi kuu zikiroga klabuni kabla ya kwenda uwanjani nakwambia laivu Ngoma ya kitoto haikeshi, Feisal Simba sijui Azam wamemrubuni kwa pesa kwa vile yeye mwenyewe ameona vipaji na vigimbi vya wenzake na ameingia baridi na kushindwa kuhimili presha ya kugombania namba , Bado ana akili za kitoto.

Utopolo tunajua mikia mnakaribia kufa kwa presha na wivu na kurubuni wachezaji wetu Ili mtuharibie sherehe kwa vile tu kinawauma sana sie utopolo tuna possess boli , tumeingia makundi shirikisho CAF kwa kuwafunga waarabu kwao, tunaongoza ligi tukisubiri Simba mpigwe mechi moja ambayo hamtapewa penati na timu pinzani kucheza pungufu!! Kombe la NBC mmeona mmelikosa mmeamua kumwaga mboga na ugali!!

Utopolo tunajua Simba mnakaribia kufa kwa kihoro kwa kuudukua mpango wa Yanga kubeba makombe yote ya bara kwa misimu mitano na utaratibu wetu wa kuhesabu unbeaten 100 maana pale tulipopanga sherehe ya kugawa keki 50 uwanjani kwa kufikisha unbeaten 50 Mikia mlienda Mbeya kabla ya mechi na mkafanikiwa kuharibu sherehe japo msichokijua ni kuwa mliongeza petrol kwenye moto Na kubadili hesabu ya unbeaten 50 kuwa unbeaten 100!

Feisal akae tu home hadi 2024 mkataba utaisha ataenda huko Azam sijui Simba. Nyie la Saba B Endeleeni kumpotosha Feitoto tu sie wenye madigirii yetu tumebukua ishu ya Feikubwa tunawafafanulia alichokosea hamuelewi!
 
Back
Top Bottom