Feitoto ni mtoro, kwanini TFF haikumuadhibu kwa kosa la utoro?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Kwenye sakata la Fei toto TFF imedhibitisha kuwa FEI ni mchezaji halali wa Yanga. Pamoja na maamuzi hayo ya TFF lakini Fei hajaonekana kazini kwa mwajili wake. Hii ina maana kuwa Fei ameikosea Yanga, TFF na wadau wa mpira. Maswali ni mengi sana kuhusu huyu mchezaji, lakini maswali muhimu kuliko yote ni

1. Kwanini TFF haimpi mchezaji adhabu kwa mujibu wa kanuni za TFF, CAF na FIFA kwa mchezaji aliyetenda kosa la aina hii?

2. Ni nani yuko nyuma ya TFF ambaye pia TFF inaogopa kumpa adhabu kwa munjibu wa kanuni za TFF, CAF na FIFA kwa mtu anaefanya kosa la aina hii?

Kama TFF ilitoa hukumu kuwa FEi ni mchezaji halali wa yanga na Fei amekaidi maamuzi ya TFF hadi inafika leo hii maana yake ni nini?

Inafikirisha sana juu ya mustakabi wa soka letu.
 
Hata Yanga nao wanashindwa kuamua juu ya mwajiriwa wao.

Haonekaniki kazini na hajulikani alipo.

Je Yanga wanaendelea kumlipa?

Naona huu mkataba unaenda kuwa void. [emoji1][emoji1][emoji1]
 
Kuna wachezaji walichelewa ama kutoroka kambini wakala adhabu.

Iweje kwa fei inakuwa shida.

Hivi Morrison yupo kambini?
 
Kwenye sakata la Fei toto TFF imedhibitisha kuwa FEI ni mchezaji halali wa Yanga. Pamoja na maamuzi hayo ya TFF lakini Fei hajaonekana kazini kwa mwajili wake...
TFF haihusiki na kutoa adhabu hiyo ila ipo kamati maalumu inayohusika na kutoa adhabu na hii ni pale yanga itakapomoa adhabu
 
Kabla hujailaumu TFF jiulize kwanza, je, Yanga ambao ni waajiri wa Fei waliisharudi TFF kutoa taarifa kuwa Fei hajarudi kazini tangu baada ya hukumu? Kama mwajiri wake hajalalamika, TFF wanatoa wapi kiherehere cha kumwadhibu Fei?

Halafu, unakumbuka kabla ya mechi na TP Mazembe akihojiwa na chombo fulani cha habari Msemaji wa Yanga Ally Kamwe alisema "Wachezaji wote was Yanga wapo kambini na siku ya mechi wote watakuwepo uwanjani". Kwa kauli hiyo, unataka TFF wafanyeje?
 
Wametoa hukumu kulingana na shauri lililowaailishwa
 
1. Kwanini TFF haimpi mchezaji adhabu kwa mujibu wa kanuni za TFF, CAF na FIFA kwa mchezaji aliyetenda kosa la aina hii?
Ondoa ujinga, tangu lini shirikisho la soka likashughulikia malalamiko ambayo haijafikishiwa? Kamati hii ilipewa jukumu la kufanya review. Tukisema muende shule mnasema tunaleta dharau
 
Fei arud yanga Ila Kama anataka kuondoka toka moyon Basi atengeneze mazingira ya kufukuzwa full utovu wa nidhamu full kutoroka kambini had yanga yenyewe imfukuze kazi.

Simple Sana km yanga hawana ajenda ya kukomaa na mchezaji au kimkomoa maana tumeona wengine walifukuzwa kwa utovu wa nidhamu so nae atembee mule mule maana ngoma ishakua ngumu hii
 
TFF haihusiki na kutoa adhabu hiyo ila ipo kamati maalumu inayohusika na kutoa adhabu na hii ni pale yanga itakapomoa adhabu
Tff mbona inatoa maamuzi, kutoa adhabu na kusimia utekelezwaji wa adhabu kwa wadau wengine?
 
Kwenye sakata la Fei toto TFF imedhibitisha kuwa FEI ni mchezaji halali wa Yanga. Pamoja na maamuzi hayo ya TFF lakini Fei hajaonekana kazini kwa mwajili wake. Hii ina maana kuwa Fei ameikosea Yanga, TFF na wadau wa mpira. Maswali ni mengi sana kuhusu huyu mchezaji, lakini maswali muhimu kuliko yote ni

1. Kwanini TFF haimpi mchezaji adhabu kwa mujibu wa kanuni za TFF, CAF na FIFA kwa mchezaji aliyetenda kosa la aina hii?

2. Ni nani yuko nyuma ya TFF ambaye pia TFF inaogopa kumpa adhabu kwa munjibu wa kanuni za TFF, CAF na FIFA kwa mtu anaefanya kosa la aina hii?

Kama TFF ilitoa hukumu kuwa FEi ni mchezaji halali wa yanga na Fei amekaidi maamuzi ya TFF hadi inafika leo hii maana yake ni nini?

Inafikirisha sana juu ya mustakabi wa soka letu.
Wewe tuliza matako usifikiri una akili sana kuwazidi wengine, ujui uyo fei kawekewa mtego gani ambao tiyali keshajichanganya pakubwa na itamcost,
 
Anaogopa mwisho km huu
IMG_7853.jpg
 
Yanga hawajashtaki TFF Haiwausu kwa Sasa.
Yanga itamwaacha abaki na urojo mpaka mwisho wa mkataba
 
Kabla hujailaumu TFF jiulize kwanza, je, Yanga ambao ni waajiri wa Fei waliisharudi TFF kutoa taarifa kuwa Fei hajarudi kazini tangu baada ya hukumu? Kama mwajiri wake hajalalamika, TFF wanatoa wapi kiherehere cha kumwadhibu Fei?

Halafu, unakumbuka kabla ya mechi na TP Mazembe akihojiwa na chombo fulani cha habari Msemaji wa Yanga Ally Kamwe alisema "Wachezaji wote was Yanga wapo kambini na siku ya mechi wote watakuwepo uwanjani". Kwa kauli hiyo, unataka TFF wafanyeje?
Ni dhahiri kuwa kuna timu ilifanya mawasiliano na mchezaji mwenye mkataba kinyume na kanuni, hata hili linahitaji microscope TFF kuliona?
 
Ondoa ujinga, tangu lini shirikisho la soka likashughulikia malalamiko ambayo haijafikishiwa? Kamati hii ilipewa jukumu la kufanya review. Tukisema muende shule mnasema tunaleta dharau
Kwahiyo TFF haiwezi kuadhibu mpaka ipelekewe shitaka? Yaani kama nikimtukana Karia sihukumiwi mpaka Karia apeleke mashitaka? Mbona Karia alimsamehe Manara lakini Kamati ikamhukumu Manara?
 
Wanaosikiliza mashauri na kuhukumu ni Kamati mbalimbali za TFF. Mfano, suala la Feitoto, aliyeshtaki ni Feitoto na iliyosikiliza na kutoa hukumu ni Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji. Kuhusu Manara, aliyeshtaki ni Sekretarieti ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na iliyosikiliza na kutoa hukumu ni Kamati ya Maadili. Kumbuka wajumbe wengine wa hizo kamati wanatoka katika vilabu ikiwemo Yanga.
 
Sasa hilo swali waulize viongozi wako wa utopolo, TFF haiwezi kutolea maamuzi suala ambalo halijalalamikiwa.
 
Yanga Kuna watu wenye weledi wewe. Kama wakienda TFF kushitaki maana yake mkataba wa Fei utavunjika na adhabu yake ingekuwa kulipa fidia fulani hivi kisha mchezaji ataondoka na kwenda alikotongozwa. Yanga hawaendi TFF ng'o kudai Fei haonekani kambini. Wachezaji wetu wote tunao, wapo kambini na hatuna shida nao. Mwenye swali aje, tunachotaka CCM ni adhabu kwa wanaowattongoza wachezaji wetu wenye mikataba halali.
 
Back
Top Bottom