Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
23,683
Reaction score
55,898
Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg. Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa.

Amesema bwawa hilo ni kubwa sana hivyo usalama wake unapaswa kuzingatiwa ktk hatua zote za ujenzi wake.

Ametolea mfano kuwa mabwawa ya Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ukubwa wake kila moja ni madogo mara kumi ya lile la Nyerere yalijegwa kwa miaka 5 kila moja.

Ameongeza kuwa bwawa la Nyumba ya Mungu lilijengwa kwa zaidi ya miaka 5.

Source: ITV (Kipindi Maalum).

Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa...
We CHAWA ropoka kuhusu vingine vyote lakini kuhusu miundombinu ya akili kwa masilahi mapana zaidi ya Taifa letu la leo na kesho ebu ficha upumbavu wako kwanza....[emoji19]
 
Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa....
Segere zimeanza. Tuliwaambia tukajibiwa sisi Chadema hatuna jema.

Kwa mujibu wa Tundu Lissu lile bwawa litakuwa na athari kubwa kiuchumi hadi likamilike. Linakadiriwa kujengwa kwa Trilioni 8 hadi 15 ili likamilike.

Hizo dana dana ni sababu ya pesa wala sio ukubwa wa Bwawa.

Kidatu miaka ya 70 huko na leo teknolojia tofauti sana.
 
Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa.

Amesema bwawa hilo ni kubwa sana hivyo usalama wake unapswa kuzingatiwa ktk hatua zote za ujenzi wake.

Ametolea mfano kuwa mabwawa ya Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ukubwa wake kila moja ni madogo mara kumi ya lile la Nyerere yalijegwa kwa miaka 5 kila moja.

Ameongeza kuwa bwawa la Nyumba ya Mungu lilijengwa kwa zaidi ya miaka 5.

Source: ITV (Kipindi Maalum).

View attachment 2243918

29 May 2022

Mubashara / Live Mafanikio ya Sekta ya Nishati, Mei 29, 2022

Source : ITV Tanzania
 
Miradi mikubwa ya awamu ya 5 changamoto kubwa sana :

MRADI WA SGR RELI MPYA NAO KUMALIZIKA NJIA ZOTE ITACHUKUA WALAU SI CHINI YA MIAKA 15 KAMA RASILIMALI FEDHA ZITAKUWEPO YAKUTOSHA

Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa...
Bwawa la mtera linaingia mara kumi? Mzee unalifahamu bwawa la mtera lakini??
 
Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa...
Huyu ni Katibu Mkuu wa Wizara husika.

Maana ya lugha hiyo ni kuwaandaa watu wakubali mipango ya kifisadi inayoandaliwa kwenye wizara hiyo.

Kesho utasikia habari za mipango ya dharura inayohitajika kufanywa ili nchi isiwe gizani.

Hawa watu ni wapuuzi sana, wanafikiri waTanzania ni wajinga.

Kabla ya ujenzi kuanza, mkandarasi na wataalam huko Tanesco hawakujua kuwa itahitaji muda mrefu kukamilisha ujenzi huo? Hii miradi inafanywa tu kwa kubahatisha bila ya kuwa na upambanuzi juu yake kuhusu muda utakaohitajika kuikamilisha?

Hayo mabwawa anayotolea mifano yake, yalijengwa kwa muda huo wakitumia teknologia gani? Leo hii hapajakuwepo na maendeleo/mabadiliko yoyote katika ujenzi wa mabawa haya?

Huku kuwadharau waTanzania kiasi hiki kunatokana hasa na nini?

Hawa watu inatakiwa kuwatafutia njia za kuwatia adabu, kwa sababu sasa wamevuka mipaka kabisa katika kuwaona waTanzania kuwa mabwege.
 
Huwezi kuanzisha miradi mingi ya matrilioni kwa wakati mmoja. Hii ndiyo hasara yake sasa

Sasa nimeelewa sababu za kihistoria marais wengine kutokuwa na uthubutu wa kupitiliza sana kuanzisha miradi mikubwa kwa mkupuo mmoja ambayo bajeti ya ndani Tanzania hata ikichanganywa na mikopo ya mabenki makubwa za nje ingekuwa hatari sana kwa usalama wa nchi na kuwepo tishio la wasiwasi ya nchi kupigwa mnada kama alivyotoa angalizo spika aliyepita.
 
Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa...
Hongera sana Bw. Felchesmi Mramba... Kumbe wenye akili kubwa bado wapo.

Kujenga a mega project kama JNHP kwa kasi waitakayo wananchi na wanasiasa ni kujitegea time bombs.

Sijui wengine akili wanaziweka wapi wanapojadili masuala nyeti, muhimu na hatari kwa maendeleo na uhai. Ndiyo tunahitaji umeme wa uhakika lakini tujue kuwa miradi ya mabwawa ya umeme ni hatarishi. Inahitaji muda na umakini!

Pamoja na mambo mengine... nchini Ethiopia Grand Ethiopian Renaissance Dam ujenzi ulianza 2011 na kukamilika 2020. GERD imeanza kazi 2022.

Tujiandae kisaikolojia. JNHP itachukua muda mrefu zaidi.
 
Yule boss wa awamu ya 5 alikuwa na nia njema lakini uwezo wake wa kupangilia mambo ulikuwa mdogo Sana. Aliendeshwa na mihemko ya kutaka sifa.

Huwezi kuanzisha miradi mingi ya matrilioni kwa wakati mmoja. Hii ndiyo hasara yake sasa
Ye angeweza. Ni uthubutu tu. Kwani mangapi yameanzishwa na yamefanyika. Kuna lecturer mmoja aliniambia wakati serikali inaanza mchakato wa makao makuu dom kuwa hautafanikiwa kabisa. Baadae ye nae akawa mpiga tarumbeta. Nadhani hakuamini kilichotokea.
 
Back
Top Bottom