Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg. Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa.

Amesema bwawa hilo ni kubwa sana hivyo usalama wake unapaswa kuzingatiwa ktk hatua zote za ujenzi wake.

Ametolea mfano kuwa mabwawa ya Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ukubwa wake kila moja ni madogo mara kumi ya lile la Nyerere yalijegwa kwa miaka 5 kila moja.

Ameongeza kuwa bwawa la Nyumba ya Mungu lilijengwa kwa zaidi ya miaka 5.

Source: ITV (Kipindi Maalum).

View attachment 2244046
Huyu naye ni walewale
 
Huyu ni Katibu Mkuu wa Wizara husika.

Maana ya lugha hiyo ni kuwaandaa watu wakubali mipango ya kifisadi inayoandaliwa kwenye wizara hiyo.

Kesho utasikia habari za mipango ya dharura inayohitajika kufanywa ili nchi isiwe gizani.

Hawa watu ni wapuuzi sana, wanafikiri waTanzania ni wajinga.

Kabla ya ujenzi kuanza, mkandarasi na wataalam huko Tanesco hawakujua kuwa itahitaji muda mrefu kukamilisha ujenzi huo? Hii miradi inafanywa tu kwa kubahatisha bila ya kuwa na upambanuzi juu yake kuhusu muda utakaohitajika kuikamilisha?

Hayo mabwawa anayotolea mifano yake, yalijengwa kwa muda huo wakitumia teknologia gani? Leo hii hapajakuwepo na maendeleo/mabadiliko yoyote katika ujenzi wa mabawa haya?

Huku kuwadharau waTanzania kiasi hiki kunatokana hasa na nini?

Hawa watu inatakiwa kuwatafutia njia za kuwatia adabu, kwa sababu sasa wamevuka mipaka kabisa katika kuwaona waTanzania kuwa mabwege.
Vijana wa JK wote wamerudishwa hivyo ngoja nchi itafunwe vizuri
 
Yule boss wa awamu ya 5 alikuwa na nia njema lakini uwezo wake wa kupangilia mambo ulikuwa mdogo Sana. Aliendeshwa na mihemko ya kutaka sifa.

Huwezi kuanzisha miradi mingi ya matrilioni kwa wakati mmoja. Hii ndiyo hasara yake sasa
Upo sahihi tatizo lake alikuwa ni mpenda sifa za hovyo lakini nia yake ilikuwa ni njema sn
 
Anawaandaa mataga kisaikolojia maana hao ndio wa kwanza kupiga kelele itakapoisha miaka 10 halijaisha.
Kwani wewe hupendi bwawa likamilike kwasababu ya mwanzilishi au halina faida baada ya kukamilika?

Naweza kuwa mujinga ila sio katika kiwango hiki
 
Upo sahihi tatizo lake alikuwa ni mpenda sifa za hovyo lakini nia yake ilikuwa ni njema sn
Sifa kwa maslahi mapana ya nchi.
Kwenda kustarehe Ulaya na kuanzisha miradi mikubwa kwa nchi, yupi mpenda sifa?.
Alijua ana muda mchache wa kuishi hivyo akagusa kila pahala kwa maslahi ya nchi.
 
Sifa kwa maslahi mapana ya nchi.
Kwenda kustarehe Ulaya na kuanzisha miradi mikubwa kwa nchi, yupi mpenda sifa?.
Alijua ana muda mchache wa kuishi hivyo akagusa kila pahala kwa maslahi ya nchi.
Hakujua ana muda muchache ila alitamani kuona Tanzania yenye mafanikio , mutu yeyote mwenye familia anajua namna Gani au njia Gani amezitumia kuhakikisha ustawi wa familia yake kama Kuna rough ezicheza halafu upo hapa kumunanga hayati hongera kwako
 
Mama amesha ahidi miradi lazima ikamilike na ataiendeleza,sasa wewe mleta mada unataka kutukatisha tamaa kwa uelewa wako mdogo...
 
Umemuelewa vibaya. Alimaanisha kuwa litakamilika ndani ya muda mfupi kwa sababu serikali inaona umuhimu wa kuuharakisha mradi, lakini kama ingekuwa kufanya kwa utaratibu kama wa mabwawa mengine basi ingechukua muda mrefu
Sasa huoni ni hatari kuharakisha bila sababu za msingi?
 
Tatizo la kwanza kwenye huo mradi tangu unaanza ni kutanguliwa na siasa nyingi badala ya utaalamu, tatizo la pili ni kukosekana uwazi katika mchakato wake mzima hadi kampuni ya wamisiri ilipoanza kujenga.
Pia Kuna uongo mwingi sana raia wameaminishwa kuhuusu huo mradi.
Huyu ni Katibu Mkuu wa Wizara husika.

Maana ya lugha hiyo ni kuwaandaa watu wakubali mipango ya kifisadi inayoandaliwa kwenye wizara hiyo.

Kesho utasikia habari za mipango ya dharura inayohitajika kufanywa ili nchi isiwe gizani.

Hawa watu ni wapuuzi sana, wanafikiri waTanzania ni wajinga.

Kabla ya ujenzi kuanza, mkandarasi na wataalam huko Tanesco hawakujua kuwa itahitaji muda mrefu kukamilisha ujenzi huo? Hii miradi inafanywa tu kwa kubahatisha bila ya kuwa na upambanuzi juu yake kuhusu muda utakaohitajika kuikamilisha?

Hayo mabwawa anayotolea mifano yake, yalijengwa kwa muda huo wakitumia teknologia gani? Leo hii hapajakuwepo na maendeleo/mabadiliko yoyote katika ujenzi wa mabawa haya?

Huku kuwadharau waTanzania kiasi hiki kunatokana hasa na nini?

Hawa watu inatakiwa kuwatafutia njia za kuwatia adabu, kwa sababu sasa wamevuka mipaka kabisa katika kuwaona waTanzania kuwa mabwege.
 
Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg. Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa.

Amesema bwawa hilo ni kubwa sana hivyo usalama wake unapaswa kuzingatiwa ktk hatua zote za ujenzi wake.

Ametolea mfano kuwa mabwawa ya Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ukubwa wake kila moja ni madogo mara kumi ya lile la Nyerere yalijegwa kwa miaka 5 kila moja.

Ameongeza kuwa bwawa la Nyumba ya Mungu lilijengwa kwa zaidi ya miaka 5.

Source: ITV (Kipindi Maalum).

View attachment 2244046
Huyu naye asitufanye watanganyika wapumbafu ama wajinga kama yeye..hajui kuwa tekinolojia imebadilika sana kwa sasa.

#MaendeleoHayanaChama
 
Yule boss wa awamu ya 5 alikuwa na nia njema lakini uwezo wake wa kupangilia mambo ulikuwa mdogo Sana. Aliendeshwa na mihemko ya kutaka sifa.

Huwezi kuanzisha miradi mingi ya matrilioni kwa wakati mmoja. Hii ndiyo hasara yake sasa
Hapana. Nchi yetu ina matatizo makubwa sana na ni kichaa tu atakayeshangilia au kusifu haya yanayotokea. Ilikuwaje mtu mmoja awe na nguvu ya kuanzisha miradi complex namna hiyo bila kupata ushauri? Kwa nini hawa wanaopiga kelele sasa hivi hawakutoa hiyo tahadhari kipindi hicho, including aliyekuwa makamu wa rais? Kwanini baada ya haya yote kutokea tunaona ni kama hakuna makosa yaliyofanyika na tukabadilisha mfumo kwa haraka sana ili yasitokee tena na badala yake tunajivuta? Hatuoni kwamba hata sasa hivi kuna makosa makubwa kabisa yanaweza kuwa yanafanyika na tusijue sasa hivi kwa sababu mfumo wetu ni mbovu?
 
Yule boss wa awamu ya 5 alikuwa na nia njema lakini uwezo wake wa kupangilia mambo ulikuwa mdogo Sana. Aliendeshwa na mihemko ya kutaka sifa.

Huwezi kuanzisha miradi mingi ya matrilioni kwa wakati mmoja. Hii ndiyo hasara yake sasa
Mwisho wa siku yoote inafeli. Alitaka kuonesha yeye anaweza kuliko watangulizi wake
 
Ye angeweza. Ni uthubutu tu. Kwani mangapi yameanzishwa na yamefanyika. Kuna lecturer mmoja aliniambia wakati serikali inaanza mchakato wa makao makuu dom kuwa hautafanikiwa kabisa. Baadae ye nae akawa mpiga tarumbeta. Nadhani hakuamini kilichotokea.
Wafuasi mna imani sana. Hapa sio mambo ya emotional mkuu ni swala la mpunga na kutumia akili.

Mtaani watu kama jpm wapo wengi sana. Akipata kidogo tu anaamini anaweza kufanya kila kitu kwa hicho hicho kidogo mwisho wa siku anapitia wakati mgumu sana mambo yoote yanakwama.

Mfano kama angeanzisha Bwawa pekee sasa hivi tungekuwa tunasubiri Ufunguzi tu. One at a time.
 
Ndiyo maana Magufuli aliwatumbua.

Mama amewarudisha na matatizo ya Tanesco yamerudi pia
 
Mshahara wake akiwa Tanesco ni milion 36 akakuruoushwa na jiwe la msingi kaenda kuwa mwalimu chuo cha Tanesco

Akaja wizarani kama mkurugenzi wa nishati jadilifu sasa Ni katibu mkuu una jambo katika malipo ya escrow huyu bwana analifahamu

Mwisho atarejeshwa ktk nafasi yake
 
Back
Top Bottom