Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Alikuwa mwanasiasa haswa ila ni mwanasiasa aliyeamini anajua kuliko wote na kushinda hata kwa kulazimisha hoja badala ya nguvu ya hoja.
Sijui habari za "siasa" kwenye mradi huo, ila najua Magufuli hakuwa mwanasiasa. Kwa hiyo sioni siasa pale, ila uhitaji wa mradi huo sioni shaka juu yake.
"Utaalam", hili nalo siwezi kulisemea, kwa vile Magufuli kwa tabia zake zilivyokuwa, inawezekana kabisa kwamba hakutaka kusikia chochote kutoka kwa wataalam, kama ilivyokuwa na COVID-19.
Kama hilo la 'utaalam' ni tatizo, kwa nini huyu Katibu Mkuu asailielezee wakati huu ili lieleweke vyema badala ya kutumia lugha kama hii aliyotumia hapa?
Ni wakati mzuri kabisa wa kuelezea kwa kina matatizo (ya kiutaalam) kama yapo ambayo yataufanya mradi huo usiweze kukamilika kwa wakati uliopangwa kukamilika; watu wataelewa vizuri akifanya hivyo.
"Kukosekana Uwazi." Huyu Katibu Mkuu ndiye anayeongeza tatizo hilo la kukosekana uwazi kwa haya anayoyaweka hadharani sasa. Anafanya ionekane kuwa kuna jambo wanalolifanya ili kuuzima mradi huo huo, kwa wao pia kutokuwa wawazi.
Hakuna shaka yoyote, Magufuli alikuwa ni mwongo, lakini hawa waliopo sasa wanatia mashaka makubwa sana. Sijaona mtu mwenye kusema ukweli toka mkuu mwenyewe hadi hawa wa chini yao.
Uongo hauwezi kuondolewa na uongo mwingine.
Ukweli ni kwamba, 'credibility' ya hawa wa sasa ni mbovu zaidi ya ile ya Magufuli.