Let's be serious kama taifa
Mkuu 'Zitto Jr.' hakuna wakati ambao sijawahi kuwa 'serious' ninapojadili mambo yanayohusu waTanzania na nchi yao. Nimeona hili nilitoe mwanzo kabisa; na wakati mara nyingi nikwa nathamini michango yako humu JF, kuwa mmoja wa watu ninaowasoma kwa makini hata kama sikubaliani na baadhi ya unayoandika. be certain that I am very serious when it comes to the welfare of Tanzania and its people. Never doubt that again.
Sina msukumo wa kufaidika kwa njia yoyote juu ya msimamo huu.
Issue ni uthubutu au matokeo?
Kwani bado unamashaka na matokeo ya kuhamia Dodoma? That's fait accompli!
Kuna mambo mengi sana niliyochukizwa na tabia za Magufuli, lakini yapo pia mengine ambayo natamani angeishia kuyafanya bila ya hayo mabovu yaliyoharibu uongozi wake.
"Uthubutu" ni moja ya sifa muhimu sana kwa kiongozi yeyote, hasa kama akiwa 'decisive' katika kufanya maamuzi yake. Mabadiliko ya nchi yoyote hutokana na viongozi wenye uthubutu.
Kwa bahati mbaya sana uthubutu wa Magufuli ulichanganyika na ukichaa wakati mwingine; mfano, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwake!
Dodoma hata airport haijajengwa Bado, ring roads hamna then unasema IMEKAMILIKA? Hivi kwanini nchi tunakosa vipaumbele wamehamia dodoma so what? Kuhamia dodoma Kuna umuhimu kuliko SGR au Nyerere Dam? Hayo Matrillion yaliyotumika kuhamia Dodoma si yangetumika kukamilisha kipande Cha Moro-Dom.
Haya mengine uliyoongeza huku sioni mantiki yake na sina haja ya kuyajibu..., utasubiri umalize kila kitu kwenye jambo moja ndio ufanye lingine? Kama nchi utawezaje kuiendesha namna hiyo!
Upigaji unakujaje sasa? Kwanini wasihujumu Bomba la gesi maana ndio umeme ni 60% unategemea gesi? Yaani wahujumu 40% itasaidia nini? Kwanini tunapenda conspiracy theories? CCM ni majizi najua ila eti hawataki kukamilisha ujenzi eti Ili watoe mikataba kwa makampuni ya kufua umeme mbona haiingii akilini? Kwanini usiseme haukamiliki sababu wanakula Hela za Mradi?? It makes more sense. Yaani wasile matrillion ya Nyerere Dam ila waje kugawana billion vichache vya PAP??
Leo umeamka vibaya, au umekwishaingizwa kichwa kichwa. Watu hawachelewi kugeuka magunia ya chumvi nchi hii.
Kukopa (madeni) siyo dhambi, mradi hela inayokopwa inafanya kazi iliyolengwa. Ni nchi gani isiyokopa kwa shughuli zake mbalimbali?
All in all, sijaona hoja ya kujadili katika majibu yako yote katika mjadala huu. Sitahangaika na hayo mengine.