Kwenye ujenzi wowote ule hata kibanda umiza marekebisho ni jambo la kawaida na pengine ndiyo sababu Katibu Mkuu akatoa tahadhari na kwamba hakuna makusudi ya kuchelewesha mradi. Hata hivyo taarifa kwamba ujenzi umefikia asilimia 60 inaongeza matumaini. Tuache kuihukumu serikali kwa kuwa makini, tujaribu kuwa na akiba ya maneno.Mkuu umenena,Mabwawa yamejengwa mengi Kidatu,Nyumba ya Mungu,Mtera,Pangani, bila mbwembwe na porojo za kisiasa.
Transparency ilikosekana katika kuwatafuta wakandarasi wa mradi wa bwawa la Nyerere.
Tumeona hata Tanroad anafanya kazi iliomzidi kimo.
Arab contractors ndie main contractor,inamilikiwa na jeshi la Misri haijaonyesha makali ya kazi,sana sana ni doctorate degrees,bilateral relationship ndio hadithi zisizohuzika kwenye mradi wenyewe.
Lakini kwa ndani Waziri Mkuu Majaliwa alietembelea huo mradi mara kwa mara alionekana kutilia shaka utekelezaji wa mradi.
Anapokuja katibu mkuu akasema anajali Safety kwanza katika utekelezaji wa mradi sio maneno ya kupuuzia.
Kuna uwezekano wa kubadiri michoro mara kwa mara ili kwendana na usalama na ubora wa mradi.Kama yapo mambo yalipuuzwa ndio wakati wa kuyaunganisha.Hata lile bwawa maarufu la Ethiopia dam X aka Millennium Dam limefanyiwa mabadiliko mengi mno ili likidhi mahitaji.