Hongera sana Bw. Felchesmi Mramba... Kumbe wenye akili kubwa bado wapo.
Kujenga a mega project kama JNHP kwa kasi waitakayo wananchi na wanasiasa ni kujitegea time bombs.
Sijui wengine akili wanaziweka wapi wanapojadili masuala nyeti, muhimu na hatari kwa maendeleo na uhai. Ndiyo tunahitaji umeme wa uhakika lakini tujue kuwa miradi ya mabwawa ya umeme ni hatarishi. Inahitaji muda na umakini!
Pamoja na mambo mengine... nchini Ethiopia Grand Ethiopian Renaissance Dam ujenzi ulianza 2011 na kukamilika 2020. GERD imeanza kazi 2022.
Tujiandae kisaikolojia. JNHP itachukua muda mrefu zaidi.
Usilinganishe mradi wa Ethiopia Renaissance Dam na huu wa Tanzania. Ethiopia walipitia kwenye upinzani wa Bwawa kutojengwa kwa muda mrefu. Misri walitishia kupiga bomu huo mradi. Kuna wakati ulisimama.
Vita ya wenyewe kwa wenyewe ilikuwa changa moto kubwa kumaliza mradi kwa wakati. Wakati wa vita ilochukua karibu mwaka na miezi saba.
Kujaza maji kwenye bwawa, Ethiopia inapata mvua mara moja tu kwa mwaka tofauti na Tanzania. Hivyo kujazwa kwa bwawa imechukua muda mrefu zaidi. Mvua Ethiopia unyesha kipindi cha mwezi wa July hadi sept. Kisha hakuna mvua tena mpaka mwaka utaofuata miezi kama hiyo. Hivyo mnakaa mwaka mzima ili kuona mvua tena.
Tusitafute visingizio vya kushindwa kumaliza mradi muda muafaka kwa kujaribu kubalance na miradi mingine. Hivi kweli mkandarasi wa kampuni husika na wataalamu wetu ni wajinga hawakujua kuwa mradi huu wa Nyerere utachukua muda mrefu walipoingia mkataba?
Ati leo ndo Katibu Mkuu aje na hizo sababu? kwa nini kumekuwa na visingizio vingi vikitafutwa, mara winchi ya kunyanyua sijui nini ni ngumu kuipata, mara mvua, ili mradi kutafuta utetezi.
Leo Katibu anafananisha ujenzi wa mabwawa ya Mtera na Nyumba ya Mungu ati yalichukua miaka mingi. Ni ujinga wa kutupwa. Hivi anataka kusema sisi watanzania hatujui kutafakari na niwajinga? Wakati wa ujenzi wa hayo mabwawa technolojia ya wakati huo na sasa ilikuwa tofauti.
Hata kiwango cha uchumi wakati huo na sasa vilikuwa tofauti.
Na kwanini Tanzania tunapenda kutetea na kuhidhinisha matatizo kwa kutafuta sababu ili tu kuwadanganya wananchi. Kwanini tusiwe wakweli.
Katika Tanzania wanasiasa ndo wasemaji wakuu hata katika mambo ya kisayansi. Pia kwa kutafuta ulaji wanasayansi na wataalamu wetu wanaweka ujuzi na utaalamu wao pembeni ili tu kuwafurahisha wanasiasa.
Hata wanahabari, sijaona alie jitokeza kuleta habari toka pande zote. Mfano kuhoji kampuni ya ujenzi wa bwawa. Kumhoji mtaalamu wa serikali msimamizi wa mradi. Na pia kuhoji wataalamu kadhaa wa mambo ya ujenzi wa umeme nchini na hata nje. Kuhoji viongozi wa serikali iliyopita na wasiasa kwa nini tuliaminishwa vingine na leo tunaaminishwa vingine. Walau tukawa na habari yenye ulalo wa ukweli.
Sijawahi kuona nchi yenye ushabiki wa ovyo usioangalia maslahi mapana ya nchi. Watanzania tunajisifia sana kuwa tumeendelea kielimu na mengineyo lakini tu kama makondoo. Tunapelekeshwa tu na kupokea kisha kushangilia kila litakalosemwa.
Maswali ya waandishi wa habari wa Tanzania mengi ni yakujipendekeza. Kujichekesha. Hatuna waandishi wenye maswali ya kufikirisha, maswali ya mitego au hata ya kukera tu. Waandishi wanauliza swali unaona huyu anajiuma uma, hawajiamini. Natamani ningekuwa mwandishi wa habari!