Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Wafuasi mna imani sana. Hapa sio mambo ya emotional mkuu ni swala la mpunga na kutumia akili.

Mtaani watu kama jpm wapo wengi sana. Akipata kidogo tu anaamini anaweza kufanya kila kitu kwa hicho hicho kidogo mwisho wa siku anapitia wakati mgumu sana mambo yoote yanakwama.

Mfano kama angeanzisha Bwawa pekee sasa hivi tungekuwa tunasubiri Ufunguzi tu. One at a time.
Point ya muhimu sana hii.
Jambo moja likikamilika,linaanza lingine.
 
Mshahara wake akiwa Tanesco ni milion 36 akakuruoushwa na jiwe la msingi kaenda kuwa mwalimu chuo cha Tanesco

Akaja wizarani kama mkurugenzi wa nishati jadilifu sasa Ni katibu mkuu una jambo katika malipo ya escrow huyu bwana analifahamu

Mwisho atarejeshwa ktk nafasi yake
Ndugu goroko77 ,upo MoE!!? Nina kampuni zangu mbili za kusambaza umeme wa REA nataka unisaidie kitu.
 
Ukubwa wa bwawa unapimwa kwa mita za mraba au mita za ujazo?
Kwa ujazo, Ila concern ya mleta mada iliegemea ukubwa kwa mita za mraba.

Hata tukienda kwa ujazo, mtera imejengwa miaka zaidi ya 50 iliyopita Leo tuje kulinganisha na Teknolojia ya sasa?
Ethiopia wamejenga bwawa la mg 6000+ mara tatu zaidi yetu. Tujilinganishe na hao

Hata hivyo nchi yetu bado haipo tayari kwa miradi ya namna hii kwa maana hata likiisha bado itakuwa white elephant project, sisi tumezaliwa kununua
 
JPM namkubali kwenye mambo mawili tu.
Mosi,alikuwa na nia njema ya kuhakikisha hii nchi inapiga hatua kubwa kimaendeleo.
Pili,ni ile kutaka kutujenga Watanzania tujitegemee wenyewe kuleta maendeleo yetu, kwani hakuna shangazi wala mjomba wa kutupa maendekeo.
Tatizo lake ni kujiona kuwa yeye ni mwenye akili kuliko Watanzania wote hivyo kutotaka kusikia na kufuata ushauri wa wengine hasa wataalamu na washauri/wasaidizi wake, kisa tu kawa rais, wakati kumbe ni "below average".
Jamaa alikuwa na ambitions za hatari ila kwenye kuzitekeleza ikawa ndio mtihani
 

Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5​


Nimemsikia amesema bwawa la Julius Nyerere ni mara kumi ya bwawa la Mtera na siyo Bwawa la Julius Nyerere ni mara kumi ya bwawa la Kidatu
 
Hongera sana Bw. Felchesmi Mramba... Kumbe wenye akili kubwa bado wapo.

Kujenga a mega project kama JNHP kwa kasi waitakayo wananchi na wanasiasa ni kujitegea time bombs.

Sijui wengine akili wanaziweka wapi wanapojadili masuala nyeti, muhimu na hatari kwa maendeleo na uhai. Ndiyo tunahitaji umeme wa uhakika lakini tujue kuwa miradi ya mabwawa ya umeme ni hatarishi. Inahitaji muda na umakini!

Pamoja na mambo mengine... nchini Ethiopia Grand Ethiopian Renaissance Dam ujenzi ulianza 2011 na kukamilika 2020. GERD imeanza kazi 2022.

Tujiandae kisaikolojia. JNHP itachukua muda mrefu zaidi.
Kwa hiyo Magufuli alitu danganya aliposema litaisha kabla ya novemba?
 
hakuna hasara wala ubaya kuwa na miradi mingi na mikubwa kwa nchi yenye utajiri kama bongo , ile ni akili kubwa , dawa ni kuzuia ufisadi na kutafuta pesa ya kukamilisha hizo miradi!

ukienda kwa mzungu kuomba pesa swali lake ni moja tu "do you have a plan?" ukimpa plan yako anaicheki akiona plan ina akili anakupa madolari!!
Bahati mbaya sana hiyo miradi ukiipeleka kwa “mzungu” hatataka hata kuisikia hiyo “plan” yako. Hivyo, hadi leo hakuna mzungu anayetaka kutoa madolari yanayohitajika.

Btw hiyo miradi ina feasibility studies na implementation plans za uhakika? Iko kwenye mpango wa muda mrefu wa maendeleo wa taifa?
 
Bahati mbaya sana hiyo miradi ukiipeleka kwa “mzungu” hatataka hata kuisikia hiyo “plan” yako. Hivyo, hadi leo hakuna mzungu anayetaka kutoa madolari yanayohitajika.

Btw hiyo miradi ina feasibility studies na implementation plans za uhakika? Iko kwenye mpango wa muda mrefu wa maendeleo wa taifa?
unafikiri kwanini hakuna mzungu alie tayari kutoa madolari? think big here ndo utaelewa maana ya kumuita Chuma cha pua Magufuli.

Hivi mkuu unajua Bunge la Ujerumani lilikaa session kibao kuzungumza na kupinga mradi wa Nyerere Dam eti unaharibu mazingira hebu fikiria umbali uliopo kati ya Tanzania na Germany wao inawaharibia mazingira gani? Lini sisi bunge letu limekaa kujadili mambo ya miradi ya nchi ingine? Magufuli will always remain a hero.


yaani ni hivi miradi hii ni ya kibabe na ya kulazimisha ikibidi hata kwa pesa ya ndani maana inafanya nchi kupaa kiuchumi na kupunguza kutegemea mikopo ya wazungu wanayotumia kutukandamiza daima. mzungu akiukataa mradi wako ujue una maslahi kwako lazimisha kuukamilisha and thats why we will always like Magufuli, he was special president

Mama Samia ana elements za Magufuli kuna siku alipinga sana propaganda za wazungu akawaambia sisi sio masikini maana hata kijijini mlo wa mwanakijiji unazidi dola moja (mihogo asali na mayai na maziwa) na wao wanaandika majority tunaishi chini ya dola moja.
 
Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg. Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa.

Amesema bwawa hilo ni kubwa sana hivyo usalama wake unapaswa kuzingatiwa ktk hatua zote za ujenzi wake.

Ametolea mfano kuwa mabwawa ya Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ukubwa wake kila moja ni madogo mara kumi ya lile la Nyerere yalijegwa kwa miaka 5 kila moja.

Ameongeza kuwa bwawa la Nyumba ya Mungu lilijengwa kwa zaidi ya miaka 5.

Source: ITV (Kipindi Maalum).

View attachment 2244046

Bwawa la JNHPP lisipo kamilika kabla ya 2025 CCM haina la kuwaambia watanzania.​

 
Tatizo la kwanza kwenye huo mradi tangu unaanza ni kutanguliwa na siasa nyingi badala ya utaalamu, tatizo la pili ni kukosekana uwazi katika mchakato wake mzima hadi kampuni ya wamisiri ilipoanza kujenga.
Pia Kuna uongo mwingi sana raia wameaminishwa kuhuusu huo mradi.
Sijui habari za "siasa" kwenye mradi huo, ila najua Magufuli hakuwa mwanasiasa. Kwa hiyo sioni siasa pale, ila uhitaji wa mradi huo sioni shaka juu yake.

"Utaalam", hili nalo siwezi kulisemea, kwa vile Magufuli kwa tabia zake zilivyokuwa, inawezekana kabisa kwamba hakutaka kusikia chochote kutoka kwa wataalam, kama ilivyokuwa na COVID-19.
Kama hilo la 'utaalam' ni tatizo, kwa nini huyu Katibu Mkuu asailielezee wakati huu ili lieleweke vyema badala ya kutumia lugha kama hii aliyotumia hapa?
Ni wakati mzuri kabisa wa kuelezea kwa kina matatizo (ya kiutaalam) kama yapo ambayo yataufanya mradi huo usiweze kukamilika kwa wakati uliopangwa kukamilika; watu wataelewa vizuri akifanya hivyo.

"Kukosekana Uwazi." Huyu Katibu Mkuu ndiye anayeongeza tatizo hilo la kukosekana uwazi kwa haya anayoyaweka hadharani sasa. Anafanya ionekane kuwa kuna jambo wanalolifanya ili kuuzima mradi huo huo, kwa wao pia kutokuwa wawazi.

Hakuna shaka yoyote, Magufuli alikuwa ni mwongo, lakini hawa waliopo sasa wanatia mashaka makubwa sana. Sijaona mtu mwenye kusema ukweli toka mkuu mwenyewe hadi hawa wa chini yao.
Uongo hauwezi kuondolewa na uongo mwingine.
Ukweli ni kwamba, 'credibility' ya hawa wa sasa ni mbovu zaidi ya ile ya Magufuli.
 
Sasa kama sio wajinga mtawafanya nini? mna mahakama ya kuwashitaki? Acha tu kuwashtaki je kuwwsema tu hadharani mna uwezo huo
Si hivi tunawasema mkuu, au unataka tuwaseme vipi?
Kuhusu watafanywa nini, vuta subira kidogo mkuu, usiwe na haraka.
 
Ametolea mfano kuwa mabwawa ya Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ukubwa wake kila moja ni madogo mara kumi ya lile la Nyerere yalijegwa kwa miaka 5 kila moja.
kwa hiyo katibu unataka kutuambia nini watanzania ? tugeukie gesi ya ntwara ama ?
 
Ye angeweza. Ni uthubutu tu. Kwani mangapi yameanzishwa na yamefanyika. Kuna lecturer mmoja aliniambia wakati serikali inaanza mchakato wa makao makuu dom kuwa hautafanikiwa kabisa. Baadae ye nae akawa mpiga tarumbeta. Nadhani hakuamini kilichotokea.
Lakini hufahamu hasara na adha waliyopata waliohamia Dodoma bila maandalizi ya kutosha. Kwanza vifaa vingi vya ofisi viliharibika wakati wa usafirishaji. Pili ofisi hazikuwepo na kujibanza UDOM na baadhi ya Wizara kwenye majengo mengine ya kupanga. Tatu ofisi za muda zilizojengwa Mtumba ni ndogo mno ofisi inayotakiwa kukaa afisa 1 kuna maafisa 4 . Chumba cha maafisa 6 wanakaa hadi 15!! Utadhani darasa!!!

Kati ya 2018 hadi sasa baadhi ya ofisi zilikuwa hazijahama. Kulikuwa na movement kubwa sana kati ya Dar na Dodoma kupeleka majalada na kuyarudisha. Gharama za kuitisha mikutano Dodoma maafisa kutoka Dar ni lazima waende. Kwa ufupi Gharama za uendeshaji zilikuwa kubwa. Si ajabu bado zipo.

Mwisho hakuzingatia social aspect ya kuhamisha watu bila maandalizi. Ndoa nyingi sana ziliyumba. Kwa hiyo kusifu kuwa aliweza kuhamisha sana but with a lot of consequences. Angehamisha lakini kwa utaratibu maalum.
 
Sifa kwa maslahi mapana ya nchi.
Kwenda kustarehe Ulaya na kuanzisha miradi mikubwa kwa nchi, yupi mpenda sifa?.
Alijua ana muda mchache wa kuishi hivyo akagusa kila pahala kwa maslahi ya nchi.
Kumbe alijua kuwa ana muda mchache wa kuishi sasa haya maneno kuwa aliuawa yametoka wapi!!!!🤔🤔🤔
 
Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg. Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa.

Amesema bwawa hilo ni kubwa sana hivyo usalama wake unapaswa kuzingatiwa ktk hatua zote za ujenzi wake.

Ametolea mfano kuwa mabwawa ya Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ukubwa wake kila moja ni madogo mara kumi ya lile la Nyerere yalijegwa kwa miaka 5 kila moja.

Ameongeza kuwa bwawa la Nyumba ya Mungu lilijengwa kwa zaidi ya miaka 5.

Source: ITV (Kipindi Maalum).

View attachment 2244046
Serikali ya kitapeli imejaza matapeli kwenye system
 
Huyu ni Katibu Mkuu wa Wizara husika.

Maana ya lugha hiyo ni kuwaandaa watu wakubali mipango ya kifisadi inayoandaliwa kwenye wizara hiyo.

Kesho utasikia habari za mipango ya dharura inayohitajika kufanywa ili nchi isiwe gizani.

Hawa watu ni wapuuzi sana, wanafikiri waTanzania ni wajinga.

Kabla ya ujenzi kuanza, mkandarasi na wataalam huko Tanesco hawakujua kuwa itahitaji muda mrefu kukamilisha ujenzi huo? Hii miradi inafanywa tu kwa kubahatisha bila ya kuwa na upambanuzi juu yake kuhusu muda utakaohitajika kuikamilisha?

Hayo mabwawa anayotolea mifano yake, yalijengwa kwa muda huo wakitumia teknologia gani? Leo hii hapajakuwepo na maendeleo/mabadiliko yoyote katika ujenzi wa mabawa haya?

Huku kuwadharau waTanzania kiasi hiki kunatokana hasa na nini?

Hawa watu inatakiwa kuwatafutia njia za kuwatia adabu, kwa sababu sasa wamevuka mipaka kabisa katika kuwaona waTanzania kuwa mabwege.
Punguza hasira mkuu, umeme wa nchi 60% unazalishwa kwa gesi so unaposema JNHPP Inacheleweshwa kisa ufisadi haingii akilini, kwanini ufisadi usifanyike kwenye Bomba la gesi ambako ndio expensive kufanya maintenance na kufua umeme??

Issue kubwa ni kwamba Miradi mingi Ina overlaps, SGR hapo hapo Bwawa hili, Bado sensa inakuja, hapo Bado Mabilion tunalipa riba Kila mwezi ya madeni ya taifa ya nje. Ukitaka kufanikiwa fanya jambo moja kwa ufanisi ila kuanza mambo mengi kwa mkupuo kisa kuonekana Unaleta mabadiliko lazima yachelewe.

Unadhani trillion 1 na kitu tunayoingiza kwa mwezi inaweza facilitate Miradi yote mikubwa, wagebill, na interest rates Kila mwezi??
 
Katibu mkuu wizara ya Nishati ndg. Felchesmi Mramba amesema bwawa la Julius Nyerere halitakamilika hivi karibuni kama ilivyoaminishwa na baadhi ya wanasiasa.

Amesema bwawa hilo ni kubwa sana hivyo usalama wake unapaswa kuzingatiwa ktk hatua zote za ujenzi wake.

Ametolea mfano kuwa mabwawa ya Mtera, Kidatu na Kihansi ambayo ukubwa wake kila moja ni madogo mara kumi ya lile la Nyerere yalijegwa kwa miaka 5 kila moja.

Ameongeza kuwa bwawa la Nyumba ya Mungu lilijengwa kwa zaidi ya miaka 5.

Source: ITV (Kipindi Maalum).

View attachment 2244046
Nafikiri huyu dingi ana cha kujifunza kwenye maneno yake mwenyewe.

1. Kasema bwawa la mtera lilikamilika baada ya miaka mitano.

2. Kasema bwala hili ni kubwa mara 10 zaidi ya Mtera.

3. Kasema hivi sasa wamefikia asilimia 60 ya ujenzi wake.

4. Ukitumia mlinganisho wake ina maana asilimia 60 ya mara 10 zaidi ni sawa hadi sasa zimejengwa Mtera kama 6 hivyo bado nne.

5. Swali ni je uwiano wa muda wa ujenzi wa mtera na hizi asilimia 60 unafanana?

6. Je teknolojia iliyotumika miaka ya 70 ndio hii ya leo?

7. Mkandarasi alipoomba zabuni hakuainisha muda wa kukamilisha mradi?

8. Mkataba wao na mkandarasi unasemaje kama miradi ikichelewa kukamilika?

9. Au anatuandaa kisaikolojia ili wairejeshe Symbion Power?

10. Anyway kila afanyalo mwanadamu atatoa hesabu mbele za Muumba.
 
Ye angeweza. Ni uthubutu tu. Kwani mangapi yameanzishwa na yamefanyika. Kuna lecturer mmoja aliniambia wakati serikali inaanza mchakato wa makao makuu dom kuwa hautafanikiwa kabisa. Baadae ye nae akawa mpiga tarumbeta. Nadhani hakuamini kilichotokea.
Walikurupuka tu hata Dodoma Bado mambo mengi hakuna, airport yenyewe ndio kwanza inajengwa hizo gharama zote ndio zimekula Hela ya kufanya hiyo Miradi mikubwa. Pato la trillion 1.5 huwezi fanya Miradi ya combined 20+ Trillion kwa mkupuo.

Kingine, unaweza kufanya hayo kama utakopa huku na kule ila wakati wa kulipa Inakua changamoto maana unakuta Pato la taifa linazidiwa na madeni!!! So lazima tu utapata shida in the long run.

Tuacheni siasa kwenye uchumi, kama mmeamua SGR then iwe SGR mnafunga mikanda mnafuta maposho, mnafuta mbio za mwenge, mnakata bajeti za safari, mnafuta sensa hadi uchumi utengemea sio mnafanya Kila kitu kwa mkupuo lazima mfeli.
 
Sema walioachiwa ndo hawana akili. Boss aliipeleka nchi uchumi wa kati ndani ya muda mfupi, niamini mimi angeliendelea kuwepo ingekamilika ndani ya muda wake. Waliobakia ndo AKILI KISODA KUMUDU HEKAHEKA HIZO.
Unafahamu utaratibu na factors zinazofanya nchi kuwa uchumi wa kati? Maana unavyoongea utadhani JPM alikuta ni zero yeye akaipaisha hapo ilipo.
 
Back
Top Bottom