Felchesmi Mramba: Bwawa la JNHPP ni mara 10 ya bwawa la Kidatu lililojengwa kwa miaka 5

Halafu hata kuhamia kwenyewe Dodoma hakujakamilika. Ofisi ndiyo kwanza zinajengwa Mtumba.
 
Kila siku muko kwenye suspicions tu, labda tupate malaika kutoka mbinguni maana kwa duniani hakuna mkamilifu.
 
Nakubaliana na ww kwenye vingi hapo ulivyonadika ila
Katika kitu ambacho nimeona wengi wanakikosea ni kuhusu deni la taifa na nani sijui alikopa sana.
Mwaka Jana niliona gazeti la jamhuri tena likiandikwa na mkongwe kabisa deodatus balile anasema Magufuli aliacha deni la taifa likiwa trillion 78.
Ilikua ni ajabu kwa mtu kama balile kuweka taarifa ile.
 
JK aliacha deni la $42 billion tafuta facts sahihi.

Magufuli alilipunguza mpaka $37 billion na kuli maintain hapo anachukua kwa mkono mmoja analipa kwa mkono mwingine; mpaka alipofariki. Ndio maana nchi ikatolewa kwenye ‘moderate risk, aliyoikuta Magufuli na kuwekwa kwenye ‘low risk’ borrowers.

Deni limeanza kupanda tena na Samia hadi kurudishwa tena kwenye ‘moderate risk’ of defaulting, majuzi tu.

Muwe mntafuta facts za third parties zinazotumiwa sokoni kuangalia debt sustainability za nchi sio porojo za Zitto Kabwe Twitter.
 
JK aliacha deni la $42 billion tafuta facts sahihi.
Acha uongo mkuu, unajua hii ni zaidi ya trillion 100!! Hivi upotoshaji huu ni kwa faida ya nani? Ni lini deni la taifa limewahi fika $42 Billion??
 
Debt sustainability inapimwa kwa Debt as percentage of GDP. So hata udaiwe kama ni taifa maskini ila deni lipo chini ya 50% utakopesheka among other factors of course. So maybe useme JPM alipandisha GDP ila kusema alishusha deni unapotosha mnoo.

 
Let's be serious kama taifa
Mkuu 'Zitto Jr.' hakuna wakati ambao sijawahi kuwa 'serious' ninapojadili mambo yanayohusu waTanzania na nchi yao. Nimeona hili nilitoe mwanzo kabisa; na wakati mara nyingi nikwa nathamini michango yako humu JF, kuwa mmoja wa watu ninaowasoma kwa makini hata kama sikubaliani na baadhi ya unayoandika. be certain that I am very serious when it comes to the welfare of Tanzania and its people. Never doubt that again.
Sina msukumo wa kufaidika kwa njia yoyote juu ya msimamo huu.
Issue ni uthubutu au matokeo?
Kwani bado unamashaka na matokeo ya kuhamia Dodoma? That's fait accompli!
Kuna mambo mengi sana niliyochukizwa na tabia za Magufuli, lakini yapo pia mengine ambayo natamani angeishia kuyafanya bila ya hayo mabovu yaliyoharibu uongozi wake.

"Uthubutu" ni moja ya sifa muhimu sana kwa kiongozi yeyote, hasa kama akiwa 'decisive' katika kufanya maamuzi yake. Mabadiliko ya nchi yoyote hutokana na viongozi wenye uthubutu.

Kwa bahati mbaya sana uthubutu wa Magufuli ulichanganyika na ukichaa wakati mwingine; mfano, ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa kijijini kwake!
Haya mengine uliyoongeza huku sioni mantiki yake na sina haja ya kuyajibu..., utasubiri umalize kila kitu kwenye jambo moja ndio ufanye lingine? Kama nchi utawezaje kuiendesha namna hiyo!
Leo umeamka vibaya, au umekwishaingizwa kichwa kichwa. Watu hawachelewi kugeuka magunia ya chumvi nchi hii.

Kukopa (madeni) siyo dhambi, mradi hela inayokopwa inafanya kazi iliyolengwa. Ni nchi gani isiyokopa kwa shughuli zake mbalimbali?

All in all, sijaona hoja ya kujadili katika majibu yako yote katika mjadala huu. Sitahangaika na hayo mengine.
 

Nenda sasa kasome full original report source ya huyo mwandishi ata kwenywe website ya World Bank. Mimi nakuwekea tu sehemu ya extracts.



Ni hivi Magufuli alikuta deni kubwa la JK alikuwa anaalishusha miaka yote toka aingie madarakani kila mwaka.

Ndio sababu ya nchi kutolewa kuwa moderate risk defaulters hadi kuwa ‘low risk’ defaulters na kuachiwa kukopa private banks.

Mwambie Samia akakope bank nje ya nchi kama atapewa mkopo sasa hivi wakati nchi imeondolewa hadhi ya low risk.

Halafu debt sustainability aingalii GDP tu kuna vitu vingi vya mapato ya serikali pia yanazingatiwa kama amount ya malipo, inflation, rates (nominal and interests), na mambo mengine ya risks assessment za finance.

Magufuli aliikuta nchi ipo kwenye moderate risks kwa zaidi ya miaka 10 kwa lugha nyingine kipindi chote cha uraisi wa J.K akaishusha mpaka low risk.

Hakuna mtu aliekopa Tanzania kwa haraka na huku akishindwa kulipa madeni yake na kuicha nchi pabaya kama Jakaya Kikwete soma hiyo report yote vizuri.

Hawa watu waliopo sasa hivi serikalini ni genge la wahuni tu wazushi na waongo.
 
Serikali kuhamia Dodoma kumekuwa na faida gani kwa nchi? Zingatia kwamba magogoni shughuli nyingi zimekuwa zikiendelea huko na mawaziri wanafanyia mikutano yao mikoa mbalimbali ya nchi.
 
Kama kulikuwa na ulazima mkubwa hivyo wa kujenga hilo bwawa na kuachana na gesi basi angemaliza kwanza bwawa kabla ya kuanza SGR na serikali kuhamia Dodoma.
 
Huelewei uchumi wa kati tulifikaje, wewe ndio akili kisoda.
Sema walioachiwa ndo hawana akili. Boss aliipeleka nchi uchumi wa kati ndani ya muda mfupi, niamini mimi angeliendelea kuwepo ingekamilika ndani ya muda wake. Waliobakia ndo AKILI KISODA KUMUDU HEKAHEKA HIZO.
 
Hakuna tatizo lolote kununua gesi yetu kutoka kwa mwekezaji ikiwa ni rahisi kuliko gesi kutoka nje na mwekezaji analipa kodi, anatoa ajira na angesababisha ukanda wa kusini kushamiri ajira.
 
Serikali kuhamia Dodoma kumekuwa na faida gani kwa nchi? Zingatia kwamba magogoni shughuli nyingi zimekuwa zikiendelea huko na mawaziri wanafanyia mikutano yao mikoa mbalimbali ya nchi.
Kuwe au kusiwe na faida hilo ni jambo tofauti wakati huu, lakini ukweli ni kwamba serikali imeshahamia Dodoma.

Kama Samia au kiongozi mwingine yeyote akitaka kuirudisha Dar es Salaam, hapo itabidi afikiri mara mbili mbili juu ya 'implication' ya tendo hilo.

Lakini hili la "faida", kwani uamzi wa kuhamia huko umeanza jana au juzi? Hili lilishakuwa limeamriwa toka siku nyingi, lilisubiri tu utekelezaji, hadi alipotokea kichaa mmoja akafanya kweli!

Kwa hiyo mjadala wa faida hilo ni swala tofauti kabisa.
 
Siasa za maskini kujitegemea wenyewe kuleta maendeleo ni porojo tu. Yeye mwenyewe alikuwa anakopa na kuchukua misaada kutoka kwa aliowaita mabeberu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…