Ficha IP Adress yako kwa kutumia VPN (Android users)

habari wakuu,ninaomba maelekezo hatua kwa hatua namna ya kutumia hii VPN kwenye simu,nilidownload app moja ya kuangalia Mpira inaitwa live nettv sasa kuanzia juzi kuna channel hazifunguki,nikatuma Ujumbe kwenye page yao fb wakanielekeza nitumie VPN.
 
not physically existing as such but
made by software to appear to do
so. Sorry mkuu nlikuwa banned
 
Wenye professional zao
 
Maelezo mazuri yametolewa kuhusu VPN.
Lakini nina swali kuhusu VPN iliyokuwa kwenye simu
moja kwa moja ukiondoa APPS kibao zilizokuwepo Play Store na kwingineko
ambazo unadownload na kuinstall kwenye simu yako.

Je naweza kutumia VPN iliko kwenye simu? Na kama ndio najazaje?
Au VPN iliyoko ni tofauti na hizi APP za VPN?
Naomba ufafanuzi mzuri ili nielewe. Naambatanisha na Picha ya VPN ktk simu yangu.
 
Watalamu jibuni swali hili mtakuwa mumetusaidiwa wengi sanaaa
 
Poa
 
cyberghost unaweza tumia kwa kupata bando za bure kweli
 
cyberghost unaweza tumia kwa kupata bando za bure kweli
 
Vpn Wanasema Kuwa Inalinda Taarifa Za Mtumiaji Ili Asiweze Kudukuliwa Na Wana Usalama Na Wahalifu,,sasa Nachohitaji Kujua,,ni Hiki, Mwanzoni nilikua natumia pc yangu bila vpn,,naperuzi mitandaon na kufanya mamb yote bila vpn inamaana hapa kama taarifa zangu wadukuzi walikuwa wanazipata vzuri tu,,Na sasa nimedownload cyberghost vpn swal lang ni je,,inauwezo wa kudaka taarifa zangu za nyuma zote ambazo zilikuwa ziko wazi na kuzificha ,,,au inaanzia kufanyia kazi taarifa zinazoingia mara baada ya kuinstall na kuanza kuitumia yan taarifa mpya,,?
 
Wanakuja
 
Jibu nimeshapigia mstari
 
Kama hautumii VPN haina maana kuwa taarifa zako zinaweza kudukuliwa. Unapotumia web au application yoyote inayotumia SSL/https taarifa zako ziko salama kwa vile zipo encrypted kwa hiyo VPN haiongezi chochote kwa upande huo.

VPN inasaidia kuficha ni site gani unazotumia kutoka kwa ISP wako i.e ISP wako anaona tu kuwa kuna connection kwenda VPN servers haoni kama unafungua JF au FB.

Pia kwa kiasi fulani inaficha upo wapi kwa upande wa site unayofungua kwa hiyo kama VPN server ipo marekani ukifungua Netflix wao wanaona kuwa IP yako ni ya Marekani.Hapa kuna tatizo la kuwa ukikosea tu hata mara moja kuacess hiyo site bila VPN wanajua ukweli uko wapi, na sio rahisi kutokosea kwa matumizi ya kawaida hata warusi waliokua wanasambaza habari feki FB walitereza mara kadhaa na kufichua walipokuwepo kweli.

Ni muhimu kuelewa kuwa unapotumia VPN maana yake unamwamini anayeendesha hiyo VPN na taarifa zako zote maana ni middleman kwenye mawasiliano yako, ni impossible kujua ni nani anaendesha hiyo VPN na lengo lake ni nini. Kwa mfano Facebook walinunua kampuni ya VPN na kuiendesha kisiri ili kujua watu wanatumia Apps na mitandao gani.

Pia VPN app nyingi ni feki au zinakusanya taarifa zako na kuziuza kwa third parties kwa ajili ya kukulenga na matangazo, fikiria VPN itakuwaje bure wakati inahitaji resources na servers nyingi kuiendesha? "If you are not the customer, you are the product".
 
Unaposeti VPN kwa kutumia setting kuna sehemu ya Name na Server address naomba msaada hapo. Au unajaza tu jina lolote
 
Nahitaji pia kujua hapa
 
Unaposeti VPN kwa kutumia setting kuna sehemu ya Name na Server address naomba msaada hapo. Au unajaza tu jina lolote
Unajaza settings za VPN server yako, so kama umenunua VPN service sehemu watakupa hizo settings kama wanasupport VPN bila App.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…