FID Q asilaumiwe, hana Verbal intelligence

Nikuongezee na Inspector Haroun, pengine akawa mtu mwenye uwezo mkubwa wa kujieleza kuliko hao uliowataja hapo.
 
Hao wooote unaosema wana uwezo wa kujieleza ni watumiaji wa mmea pendwa, kasoro Master J(just maybe)….. unataka kusemaje hapo?
Master ni mtumiaji mzuri wa mmea mzuri tu. Alikiri mwenyewe kwenye interview
 
Kama kweli hiyo «verbal intelligence» ipo, basi itakuwa ni sifa/tabia ya kike aka sifa ya Wasichana na Wanawake, maana wao ndiyo wanawahi kuongea lugha utotoni, na hata ukubwani huwezi kushindana nao kwa mdomo. Mfani ni Dokta Kumbuka na mashoga wengineo wengi redioni ambao wameajiriwa sababu ya wepesi wa midomo yao. Akili zao zipo midomoni.
 
Kwa wote niliwahi kuwashuhudia na kuwasikia hakuna anaye ingia hata chembe kwa Malcolm X kwenye suala zima kujielezea , kufafanua na kutetea hoja .

Jamaa alikuwa anakipaji kikubwa sana akihutubia anajaza watu kushinda hata Rais
 

Kumbe upo ubungo kibangu ww ni jirani yangu kabisa
 
hapo kwa Chid benz umeula wa chuya
 

Unaelimu gani Boss?

Wapi hujaelewa maana ya Verbal Intelligence?

Kuongea ongea ni tofauti na Verbal intelligence,

Kwa mfano wewe unajua kusoma lakini huna akili ya kuchambua kilichoandikwa. Hivyo huwezi itwa una Ujuzi WA kusoma Reading Skills Kwa sababu huwezi kufanya interpretation ya kilichoandikwa.

Hat kasuku anaongea lakini hana verbal intelligence Kwa sababu ya upeo mdogo.

Tofautisha kuongeaongea na Ujuzi wa kuongea.
Nimeshatoa kabisa na sifa za kuwa n verbal intelligence na mambo ya kuzingatia kwenye Uzi lakini bado akili yako haina uwezo wa kuchambua na kutafakari.
 
Fid Q yuko sawa.
Usemaji wa masuala fulani sio lazima msemaji awe na fani husika.
Msemaji ni yule anayepokea maelekezo na yeye kutumia ubunifu fulani kuyawakilisha.
Kwa mfano sio wote wanasemea michezo ni wachezaji au walikuwa wachezaji hapo kabla.
Msemaji hana tofauti na MC, kinachohitajika ni kumlisha vitu muhimu.
Uteuzi wa Steve na wengine kulalamika utamfanya mteuliwa kutumia loop hiyo kuanza majukumu yake.
 
Hao wooote unaosema wana uwezo wa kujieleza ni watumiaji wa mmea pendwa, unataka kusemaje hapo?
Mtu anayetumia bangi huwa yuko makini na anaongea vitu vinavyo eleweka . Huwez mlinganisha na mlevi .

On my side I prefer smoker to drinker.
 
Msimfokee Fid Q.

Nilichogundua Watu wana ushabiki na hawafuatilii yaani wengi mnazani Fid Q ndio katoa maamuzi peke yake mnasahau kuwa kamati ilikaa na kumteuwa Steve.

Je, kamati ni Fid Q pekee?
 
Mwana FA simuoni kwenye list yako!
 

Hii list yako ni coincidence au ina uhusiano na utumiaji wa mmea?
 
Si tuliambiwa huyo jamaa ni intelligent!?.
 
Afande Selle, P funk majani hawa wanajua sana kuelezea kitu kikaeleweka kwa urahisi sana

Nakubaliana na mleta mada
 
Intelligence ya kuongea kwenye hadhara au hata watu 10 ni kama umenisema mm.

Hiki tatizo lipo kwenye uandishi pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…