Fidia ya Tsh. Bilioni 75 iliyolipwa na Serikali kwa Winshear Gold Corp ingeweza kununua Mashine 83 za CT-Scan

Fidia ya Tsh. Bilioni 75 iliyolipwa na Serikali kwa Winshear Gold Corp ingeweza kununua Mashine 83 za CT-Scan

Uamuzi wa Serikali kuifanyia marekebisho Sheria ya Madini ya mwaka 2010 yaliyofanyika mwaka 2017 na kanuni zake ni chanzo cha Serikali kulipa Sh75 bilioni kwa mwekezaji Winshear Gold iliyemfutia leseni.

Fedha hizo zingeweza kutumika kuboresha sekta kadhaa za maendeleo, lakini zimeishia mikononi mwa mwekezaji kutokana na uamuzi uliofanywa na Serikali miaka michache iliyopita.

Fedha zilizolipwa kwa kampuni hiyo zingeweza kujenga zahanati 267 na vituo vya afya 68.

Kwa upande wa magari ya kubebea wagonjwa, yangeweza kununuliwa 250, moja likigharimu Sh300 milioni na kila mkoa ungeweza kupatiwa magari tisa.
 
Mkuu mbona unawaza miundombinu tu Kila wakati?

Badala ya kusema ingeweza kuajiri walimu kadhaa au kuongeza mishahara ya walimu kiasi kadhaa au tungewapa posho walimu wanaolea taifa hili kiasi kadhaa au tungeboresha miundo ya utumishi wa walimu walau kima cha chini kianzie Milioni Moja n.k

Mawazo ya namna hii ndio tunahitaji baada ya miaka kadhaa utakuwa na taifa bora kabisa lililoelimika.

Pia, utakuwa umeongeza tija kubwa na value ya human labour sio Kila mara majengo tu na magari hizo ni teknolojia zinachakaa lakini ukiwekeza kwa watu Mzee unajenga taifa
 
Serikali kupitia kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali imethibitisha kuilipa kampuni ya Winshear Gold fidia ya Tsh. Bilioni 75 baada ya kukamilika kwa mazungumzo ya kumaliza Mggoro nje ya Mahakama.

Chanzo cha mgogoro huo ni uamuzi wa Serikali wa mwaka 2017 kuifutia kampuni hiyo leseni ya uendeshaji wa mradi wa uchimbaji Dhahabu wa SMP ambapo kampuni hiyo haikukubaliana na uamuzi huo. Mwaka 2020 ilifungua kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Migogoro ya Uwekezaji (ICSID) nchini Uingereza ikiwakilishwa na kampuni ya uwakili ya Lalive.

PESA ILIYOLIPWA INGEWEZA KUTEKELEZA MIRADI IFUATAYO KWA ZAIDI YA ASILILIMIA 100%

Kiasi cha fedha kilicholipwa kwa kampuni ya Winshear Gold ni kikubwa kuliko Bajeti za Wizara hizi za mwaka 2023/24:
  • Utamaduni, Sanaa na Michezo - Tsh. 35,445,041,000
  • Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira - Tsh. Bilioni 54.1
  • Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum - Tsh. Bilioni 74.2
Kwa maana hiyo, Fedha zilizolipwa kwa kampuni hiyo zingewezesha upatikanaji wa moja kati ya huduma hizi muhimu.

1. Zahanati - 267 (Gharama ya Zahanati moja Tsh. Milioni 280).
2. Vituo vya Afya - 65 (Gharama ya Kituo kimoja Tsh. Bilioni. 1.15).
3. Magari ya kubeba Wagonjwa - 250 (Gari moja Tsh. Milioni 300) kila Mkoa ungepata Magari 9.
4. Madarasa - 3,750 (Darasa moja Tsh. Milioni 20).
5. Madawati - Milioni 2.5 (Dawati moja Tsh. 30,000).
6. Vipimo vya CT Scan - 83 (Mashine moja Tsh. Milioni 900).
7. Visima Vifupi vya Maji - 25,000 - 75,000 (Kisima kimoja ni kati ya Tsh. Milioni 1 hadi Milioni 3 kutegemea na eneo).
8. Mkopo wa Elimu ya Juu - Wanafunzi 18,750 (Kila Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza angepata 100% Tsh. Milioni 4).
9. Pembejeo za Kilimo - Mifuko 6,250,000 ya Mbegu za Mahindi 6,250,000 (Mfuko mmoja Tsh. 12,000).
Tumepata mgodi lakini au?
 
Back
Top Bottom