Field Marshal John Okello ni mwanamapinduzi au missionari

Hilo ndio swali la msingi la kujiuliza, Ambapo jibu lake Utakua ni mwarobaini wa uzi huu.

Nami ni kuulize?
"Unaweza nipa vigezo vya mapinduzi yeyote Kuitwa "MATUKUFU"?"
Nitakujibu ikiwa utanipa tafsiri ya neno "mapinduzi" na tena iwe mapinduzi hayo uliokusudia.
 
Hawataki, mleta mada anataka Sultan arudi.
Hawataki, mleta mada anataka Sultan arudi.
Usinitia maneno kinywani. Ninachotaka uamuzi wa Zanzibari uheshimiwe uliotokana na ushindi wa sanduku la kura. Na hilo limefanyika na kuendelea kufanyika. Dhambi waliofanya ASP(CCM)kwa mauaji 1964 litaendelea kuwaadhibu na mpaka dunia itakapomalizika CCM haiwezi kushinda uchaguzi huru haki na wa kidemokrasia Zanzibar. Hii ina maanisha kizazi kwa kizazi itazidi kuichukia CCM Zanzibar na wataendelea kuiadhibu kwenye sanduku la kura na wao waendelee na mapinduzi Mtakatifu
 
Nitakujibu ikiwa utanipa tafsiri ya neno "mapinduzi" na tena iwe mapinduzi hayo uliokusudia.
Umesema kama okello alikuwa anachukia ufalme angeanza kuondoa wa Uganda na sio was Zanzibar,kwani sultani halali tangu mwanzo aliyetawala zenji alitoka omani?kipi kilimsibu sultani halali baada ya kuwaomba msaada wa kivita kwa hao wa oman kumshinda mreno?kumbe okello alisaidia kuondoa waoman wavamizi na kurudisha visiwa kwa wenyeji sio?
 
Mbona wanzibar mpo wengi bara! Acha ubaguzi
 
hivi huoni watu wameanza kutolewa mpaka machoooo, au mpaka uambiwe mimi ni muislamu au mkristo ???

Unafikiri Dar es Salaam ilikuwa hivyo kabla kuja ukristo hapo???
Kwahiyo aliyemtoa macho muathirika alikuwa mkristo?
 

Ulipoongelea kuhusu watanganyika kuishi miaka kumi Na kupata haki ya kuitwa wazanzibari hivyo kuongeza "UTITIRI WA MAKAFIRI KISIWANI" ulikua ukimaanisha nini?
 
Ulipoongelea kuhusu watanganyika kuishi miaka kumi Na kupata haki ya kuitwa wazanzibari hivyo kuongeza "UTITIRI WA MAKAFIRI KISIWANI" ulikua ukimaanisha nini?
Ni dhana inayo kusumbua. Neno Kafir ni neno la kiarabu lenye maana ya mtu anaepinga uwepo wa mungu. Wengi wahamiaji kutoka Tanganyika wanaolowea Zanzibar wanatoka ukanda wa pwani ambao wengi wao wanaamini uwepo wa mungu. Kwa mujibu wa imani, silka na utamaduni wa wazanzibari hawataki kuwa na "UTITIRI WA MAKAFIRI KISIWANI".Sasa kusema hivyo nimeigusa imani gani zaidi ya Makafiri?
Mbona wanzibar mpo wengi bara! Acha ubaguzi
Ni milki yetu(eneo tuliolitawala)kiasili
Nani mwenyeji wa Zanzibar zaidi kati ya Karume na Muhammed Shamte? Yule hata uraiwa wake uliohojiwa mahakamani na mwenye uraia wa "affidavit" na mwana kindakindaki, vizazi kwa vizazi kuzaliwa visiwani?

Mohammed Shamte,Waziri Mkuu ni mshirazi wa kipemba ndio aliepinduliwa baada ya kushinda kwa sanduku la kura uchaguzi huru na wa haki.Nadhani unaelewa taratibu ya utawala wa nchi/serikali zinazongozwa na Waziri mkuu. Aliepinduliwa ni mwenye serikali nae alikuwa ni Shamte. Baada ya Mapinduzi aliewekwa gerezani(Tanganyika -waandaji wa mapinduzi)kwa miaka kumi alikuwa Shamtena baraza lake la mawziri ( walioshinda uchaguzi majimboni mwao nasi wengine yeyote, kwa vile serikali yake ndio iliopinduliwa.
Kumbuka pia Jamshid alipokimbia mauaji alikimbilia Kenya na baadae Tanganyika. Kwanini asikamatwe alipokuwa dares salaam na kuwekwa ndani kama akina Shamte, badala yake akaandaliwa safari na Nyerere kwenda Uingereza ambako mpaka leo yupo?Wakati wenzake waliosekwa gerezani kwa miaka kumi wote wameshakufa?

Tatizo nchi yenu haina historia na mnalazimisha na nchi nyengine zisiwe na historia kama nyie.Dhamira ya Okello kwa Zanzibar ilikuwa si kuwaondoa waislamu wa Zanzibari wenye asili ya Ghuba,lakini ilikuwa ni kuudhibiti uislamu kwa mauaji. Kutoka maneno yake mwenyewe alinukuliwa "Okello appealed to the black majority, but at same time, as a militant Christian who claimed to hear the voice of God in his head, Okello's appeal on an island whose population was 95% Muslim was limited"

Baadae hata hao ASP wenyewe walipoishtukia dhamira yake hiyo ovu walimfukuza na kumtangaza kama mtu asietakikana visiwani. ASP ilikwenda mbali zaidi na kutamka kuwa jina la Okello lifutwe,lisitamkwe, kutajwa wala kukumbukwa katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar.


 
Kwa style hii wacha tuwatawale
 
Nitakujibu ikiwa utanipa tafsiri ya neno "mapinduzi" na tena iwe mapinduzi hayo uliokusudia.
Mapinduzi tukufu ni hali ya wazalendo wa nchi kufanya mabadiliko ya uongozi dhalimu kwa njia ya mapambano iwe ya kumwaga damu au bila kumwaga damu.
 
Mapinduzi tukufu ni hali ya wazalendo wa nchi kufanya mabadiliko ya uongozi dhalimu kwa njia ya mapambano iwe ya kumwaga damu au bila kumwaga damu.
Wazalendo wa nchi .......John Okello,Eugen,Edington, Mfaranyaki,Kaujore,Washoto nk. Uongozi dhalimu ...Uongozi ulioshinda uchaguzi huru na wa haki kupitia sanduku la kura.Kumwaga damu ..kumwaga damu kwa misingi ya kiimani na kikabila.

Mapinduzi matukufu... umeyatolea tafsiri nzuri sana, sasa ulichotaka kujua kutoka kwangu ni kitu gani? Niseme Mapinduzi matukufu nikama Quran? au utukufu wake ni wakuwaangamiza waislamu?

 
..Haya alikuwa missionary,so whats Your Point??
 
Nchi nzima ya Zanzibar ilipinduliwa na watu sita?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…