FIFA kujenga uwanja wa michezo kwa kila nchi mwanachama barani Afrika. Je unapendekeza mkoa/bei gani?

FIFA kujenga uwanja wa michezo kwa kila nchi mwanachama barani Afrika. Je unapendekeza mkoa/bei gani?

Tupige soga tu, ila Mukulu kashafikiria kama sio Dodoma basi Chattle, Karia atapewa maelekezo tu.

Kama ni siasa zetu basi kijengwe Dodoma na kama ni mpira na biashara ya mashabiki wengi wa mpira basi Dar haina mpinzani na uwanja utakuwa na faida endelevu
 
Kigoma mwambao Wa ziwa Tanganyika watalii waje kuangalia meli kongwe duniani MV liemba na ni mkoa uliochangia sana kutoa vipaji vya soka nchini,tp mazembe,as vital,vital o na intersport zitaweza kuweka kambi zao hata timu za kimataifa pia.
 
Dar maana ndiko wanakoishi watu. Huku mtwara wala hakufai tunaishi manyani
Na uitwe mwalimu julius kamba rage nyerere
 
Kilimanjaro, kwa sababu hamna uwanja mkubwa wa michenzo, pia tutakuza utalii mlima kilimanjaro na mbuga za wanyama
 
Uwanja ujengwe Dar..mikia wanacheza Taifa na Yanga wanakipiga uwanja wa FIFA hakuna janjajanja
 
Morogoro ilikuwa ni sehemu sahihi ya kuweka uwanja huo ukizingatia SGR hilo mbioni kutunguliwa hivyo kuwahusisha usafiri kwa muda muafaka. Unatoka Dar saa 7 mchana saa 8.30 huko Moto alafu baada ya mechi inarudi zako Dar kihulaini. Wapenzi tupewe nafasi ya kupendekeza, nina imani Moto utainuka kidedea, hila changamoto hakuna airport Na hoteli za kueleweka
 
Back
Top Bottom