FIFA kujenga uwanja wa michezo kwa kila nchi mwanachama barani Afrika. Je unapendekeza mkoa/bei gani?

FIFA kujenga uwanja wa michezo kwa kila nchi mwanachama barani Afrika. Je unapendekeza mkoa/bei gani?

kabla ya kufikiria mkoa gani ujengwe waangali ni mkoa upi ambao washabiki wake wanaweza kujaza uwanja mfululizo bila kujali gharama jibu hakuna zaidi ya Dar es salaam ni heri ujengwe mkoa wa Pwani
 
Kote hakufai bali inapaswa ukajengwe Lindi!

Uwanja ukishajengwa Lindi uwe unatumika kwa mechi za kimataifa! Na baada ya hapo tuwaache Wazee wa Lindi wawe ndio wanaendesha shoo kwa kutumia utaalamu wao ule ule wanaojua wenyewe kwa mechi za Ligi Kuu Tanzania! Nakumbuka enzi hizo Lindi kulikuwa na timu ya Kariakoo Lindi!!! Mbele ya Kariakoo Lindi, hakukuwa na cha Yanga wala Simba, ukinusa Uwanja wa Ilulu Lindi, lazima ule kibano, na pona yako ni suluhu!

Kwenye Ligi Kuu 1999, hakuna timu hata moja ya Ligi Kuu iliwahi kutoka na point zote Uwanja wa Ilulu Lindi! Ni timu moja tu, Yanga ndio angalau iliwahi kuambulia Point 1 pale Ilulu! Na ingawaje Timu ya Kariakoo ilikuwa ni dhaifu, waliweza kushiriki na kuchukua Kombe la Hedex East Africa kwa sababu kila aliyegusa Lindi, alikula kibano!

Hivi sasa, nasikia Timu ya Namungo nayo, iliyopo Ruangwa Mkoani Lindi, nayo inatembeza kibano kwa kila timu inayonusa uwanja wao wa nyumbani!! Leo hii Namungo, timu mpya kabisa katika Ligi Kuu, tena ikitoka kwenye wilaya iliyo sawa na kijiji, kwenye msimamo wa Ligi Kuu inashika nafasi ya 6 ikiwa imewaacha vigogo kadhaa nyuma yake!!

Ni kwanini basi Wazee wa Lindi wasipewe mikoba ya kusimami mechi zetu za kimataifa mara wakishapewa uwanja wenye hadhi za kimataifa?! Tutawaambia: Hatuwaingii! Fanyeni yale yale mliyokuwa mnayafanya wakati wa Timu ya Kariakoo!

Hapa chini ni msimamo wa Ligi Kuu Bara mwaka 1999.
Kariakoo.png


Mnyama Kariakoo kashinda mechi 14 na 13 zote HOME! Mechi yake ya kwanza na Simba, K/koo akachezea 3-1 pale Shamba la Bibi! Kariakoo wakawaambia Simba, "...sawa bhana, si mtakuja home!" Na kweli, July 10, 1999 kwenye mechi ya pili, Simba haooo Ilulu Lindi, na hiki ndicho kilitokea:-
Simba!.png


Dakika ya 51, Mnyama akaweka gamba kwapani, akasepa zake kabla mechi haijaisha 😂😂😂!!! Ila Simba malofa sana! Wenzake badala ya kupoteza nauli hadi Linid, wao walikuwa wala hawajisumbui kwenda huko!! Ukafanye nini wakati unajua utagongwa tu!!!

Wale Waarabu wa Misri wanaotuonea, hapo watakuwa wanaenda Ilulu na wenyewe lazima wakaweke gozi kwapani wakaonje chungu ya wanayowafanyia wenzao!!!
 
KIGOMA,itapendeza zaidi,tukiangalia kwa miaka ijayo itakuwa ni mji mkubwa unaokuwa upande wa Magharibi ya Tanzania. Ni rahisi Taifa stars kucheza mechi za kirafiki au mashindano yanayohusu na kushirikisha nchi za DRC,Burundi,Rwanda hata Zambia na Uganda.
Mkoa wa Kigoma una vijana wenye vipaji(yafaa hata kuanzisha "Football academy").
 
Back
Top Bottom