FIFA na CAF zasimamisha Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nigeria (NFF)

FIFA na CAF zasimamisha Uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Nigeria (NFF)

Jannatul Firdaus

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2026
Posts
446
Reaction score
1,113
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA) likishirikiana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeagiza kusitishwa mara moja kwa mchakato wa uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu la Nigeria (NFF). Uchaguzi huo ulikuwa umepangwa kufanyika Septemba 27, 2026, mjini Lafia, Jimbo la Nasarawa.

Hatua hii imekuja kufuatia mgogoro mkubwa wa uongozi ndani ya shirikisho hilo baada ya kujiuzulu kwa pamoja kwa aliyekuwa Rais wa NFF, Ibrahim Musa Gusau, Katibu Mkuu Mohammed Sanusi, pamoja na wajumbe wa Kamati ya Utendaji.
SaveClip.App_800345961_18489499594102583_7947577329696849361_n.jpg
SaveClip.App_800696322_18489499609102583_6158559658961577926_n.jpg
SaveClip.App_801101462_18489499585102583_6767410602289029625_n.jpg
 
Back
Top Bottom