tpaul
JF-Expert Member
- Feb 3, 2008
- 24,225
- 22,632
Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Kwa hakika, TFF ndio wanaoharibu mpira wa nchi hii kwa kuingiza siasa ndani yake. Kwa mujibu wa sheria za FIFA, ni marufuku mashirikisho ya mpira ambayo ni wanachama wa FIFA, ikiwemo TFF, kuingiza mambo ya siasa kwenye mpira. Kuna matukio kadhaa yanayothibitisha na kubainisha kuwa TFF wameshindwa kuendeleza mpira badala yake wanaendeleza siasa.
Mosi, TFF, kwa sababu wanazozijua wao wenyewe au kwa sababu anazozijua Rais wa TFF, Wallace Karia, wamekuwa mstari wa mbele kuingiza siasa ndani ya mpira kwa makusudi na kwa maslahi binafsi. Kwa kuwa Karia ni kada maarufu wa CCM, amemruhusu mwenyekiti wa chama chake, Rais Samia kujiingiza kwenye mpira ili kujipatia kiki za kisiasa. Kumruhusu Samia kujijenga kisiasa kupitia kampeni ya Goli la Mama, ni ukiukwaji mkubwa sheria za FIFA unaoweza kupelekea shirikisho kufungiwa mara moja.
Pili, Juzi mchezaji wa Namungo ameadhibiwa kwa sababu ya kuonyesha vitendo vya kishirikina wakati Simba walipocheza na timu ya Namungo. Mchezaji mwingine pia aliadhibiwa kwa kumnyanganya mpira ball boy. Adhabu zote mbili kwa mujibu wa kanuni za TFF faini yake haizidi Tsh laki 5! Na kibaya zaidi, timu iliyowaelekeza ball boys kuchelewesha mipira haijachukuliwa hatua yoyote! Hii kama sio siasa ni nini? Inawezekanaje timu au wachezaji watozwe faini ya laki 5 tu kama kweli TFF wanataka kukomesha uhuni kwenye mpira? Haikubaliki. TFF walipendekeza faini ndogo ili ukiukwaji uendelee kwani kwa kufanya hivyo kuna timu zinanufaika na ukiukwaji huo, ikiwemo timu ya Yanga.
Tatu, Kitendo cha TFF kutoza faini ndogo za laki 5 hadi milioni 10 ndicho kinachozipa jeuri timu kukiuka kanuni za mpira. Kwa mfano, Yanga wamepata jeuri ya kuwazuia Simba kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Mkapa kwa kuwa wanafahamu hata kama watapigwa faini, haizidi Tsh milion 10 ambayo haiwaumizi kiuchumi. Ikiwa faini itaongezwa kufika walau Tsh milioni 100, huu use.nge uliofanywa na Yanga na unaofanywa na timu nyinginezo utakoma mara moja.
Aidha, kuweka options mbili kwenye faini - kwamba ama timu ilipe faini au ishushwe daraja, hii sio sawa hata kidogo. Hivi kwa mfano tukisema Yanga ishushwe daraja kwa kuwazuia Simba kufanya mazoezi si watacheza kwenye ligi ya Championship msimu mmoja tu na msimu ujao wanapanda ligi kuu? Sasa hiyo itakuwa imesaidia nini? Ingefaa kama timu zinazokiuka taratibu zingetozwa faini ya Tsh 500M au kufutwa kabisa ikiwa zitashindwa kulipa faini. Hili lingekuwa suluhisho la kudumu kwa timu pumbavu kama Yanga zinazokiuka kanuni kwa makusudi.
Nne, sote tunakumbuka mwaka jana Wallace Karia alitumia jukwaa la TFF kumkandia mpinzani wa chama chake cha CCM, Mh Tundu Antipas Mugway Lissu na kusababisha mtafaruku mkubwa wa kisiasa hapa nchini. Mtu amepewa mamlaka ya kuendeleza mpira lakini anaendeleza siasa badala ya mpira. Hii halikubaliki hata kidogo.
Kwa sababu hizi na nyingine nyingi ambazo sijazitaja kwenye munakasha huu, nawaomba FIFA wawafungie TFF kwa kuwa makosa yao ya kuingiza siasa yamekuwa yakijirudia mara kwa mara na kwa sababu kanuni nyingi za TFF zimetungwa kwa misingi ya kisiasa. Kibaya zaidi, kada wa CCM, Wallace Karia, anatumia jukwaa la mpira kumjenga kisiasa mwenyekiti wa chama chake (CCM) huku akijua fika kwamba FIFA inazuia kuingiza masuala ya siasa kwenye mpira.
FIFA wamezifungua nchi 17 kwa sababu ya kuingiza siasa kwenye mpira. Wembe uliotumika kuzinyoa nchi hizo, naomba wembe huohuo utumike kuwanyoa TFF ili liwe fundisho kwa washenzi wengine wanaoharibu mpira kwa makusudi. Nchi zilizofungiwa ni hizi hapa: The 17 countries FIFA has banned from entering the World Cup since 1950 and why
Nawasilisha.