bajeti ya ahly ni dola milion 100+ kwa mwaka!
hizo dola mil 50 wala haziwafanyi wao kuwa bora zaidi kutuzidi,
afrika hii timu zijitahidi kufanya scouting, wachezaji wazuri ni wengi sana!
simba na yanga ingekua zinajiendesha kisasa zina uwezo wa kutengeneza mapato zaidi ya 20b kwa mwaka, kiasi ambacho kinatosha kuendesha timu na ikawa na ushindani........
1. kadi za wanachama
2. bidhaa za timu (jezi, skafu, kalenda, kanga, makoti, vyombo vya vyakula vyenye logo zao, etc...... hapa ndio pana pesa ndefu zaidi)
3. gate collection (hapa wanatakiwa kukodisha uwanja, ila wavune vizuri mapato through corporates, migahawa, viingilio, majukwaa unayauza kwa makampuni yajitangaze n.k)
4. media
5. ...
6....
7....
katika nchi kama hii ambayo wapenda mpira ni wengi, ni rahisi sana kuwageuza pesa!
Mkuu umezungumza kama vile ulikuwa kwenye mawazo yangu ila nafikiri Simba wanaweza kuwa matajiri kama wakifanya yafuatayo:-
1: Siku ya simba day wanaweza kuleta timu kubwa mbili au 3 kwa siku tofauti tofauti ambapo kuwepo na tofauti ya siku mbili mbili, wanaweza vuta hela Sana.
2: wanaweza kuanzisha card zao ambazo zinaweza kuwa ni special kwenye kuingia uwanjani,bank, kulipia ada yao ya uanachama, Malipo ya kununua jezi,vikombe nk.
3: kutangaza kila mwaka kwenye Media kuhusu ishu ya kampuni inayotaka kuingia kwenye udhamini na hivyo kufungua milango ya wafanyabiashara kuingia makubaliano. Hapo inahitajika mtu wa marketing afanye Kazi yake.
4: Kuwepo na kadi special za wanachama kuanzia wale wa VIP, VVIP NK ambapo kadi zinaweza anza hata kuanzia million 10, million 5, million 3, million 2, million, laki tano nk. Hapa hela inayopatikana inaweza tumika katika usajili na Mambo mengine madogo madogo.
Hawa waliochangia wanaweza pata faida km ifuatavyo:-
1: kupata tickets bure wao na familia yao Katika kila mechi nje na ndani ya nchi.
2: kupata jezi free
3: kupata hata vinywaji na ikiwezekana vitafunwa, kupata viatu,na mengineyo. Hapa ni kwa wale wa kuanzia million na na kuendelea.
4. Kama timu inaweza fanya Hivi katikati ya msimu,hela inaweza tumika katika uwekezaji.
Pia yapo mengi tu kwa timu kuweka mikakati ikiwemo kujua idadi ya fans wa simba kupitia katika card na kusajili watu wa ndani na nje ya nchi na wao kupata hadhi yao na hata taarifa za Simba, mazoezi ya simba, wachezaji wanaoona wanafaa,nani aingie na nani atoke,waweke mitandao ambayo wanaweza toa maoni yao na viongozi wakasoma,kuwajibu n huko pia hata youtube na other social media ambapo mpunga unaweza kuingia vizuri tu kila mwezi.
Kama kuna watu wanataka hata kumleta mchezaji ghali na atamlipia,au kuna wanaotaka kujitolea mbona very simple?wapo wanaotaka kumpa zawadi mchezaji anaweza fanya hivyo akatoa hela yakr na ikafika kupitia katika mitandao hyo hyo ya kijamii.
Kwa Sasa kuna mambo ya hovyo yanayofanyika kama ifuatavyo:-
1: malumbano ya uongozi na uongozi
2: kocha na wachezaji.
3:hakuna platform ya hawa fans kutoa maoni yao na kubaki kutoa kwenye mitandao ambayo inachochea katika mifarakano kati ya wachezaji, kocha na viongozi.
4: kuvujisha taarifa za wachezaji wanaotakiwa simba kabla ya kumalizana nao na hivyo kufanya timu pinzani au kumuongezea mchezaji gharama za usajili au hata kuingia Katika radar za timu zingine ambazo hazijafanya scouting bali kuisubiri Simba ifanye scouting,itoe wachezaji kwenye mitandao na wao waongeze dau na kwa kuwa simba kwenye hela ni mkono mfupi, inashindwa katika mihimili gharama za mchezaji baada ya kuwa aghali,wanaishia kula kwa macho, AZIZI K walianza nae hadi kwenye mitandao, baadae MANGUNGU akasema deal done na kuonyesha gharama za kumsajili mchezaji, yanga wakaongeza hela, leo amekuwa msaada Sana kwa yanga. Kuna Manzoki nae yuko wapi,ni magazeti, viongozi, na mitandao kila Siku kuipamba simba ila mwisho wa siku wanakuja Kuchukua wachezaji wanaokaa benchi tu na wa gharama nafuu Sana.
Kama wataendelea Hivi basi simba inaweza shuka daraja na kubaki na sifa tu ya kile miaka ya nyuma ilipofikia robo fainali tu.
Pia huyu mwekezaji nae auze hisa zake maana tunasikia kuwa kuna watu wanataka kuweka mpunga wa maana.
Mwisho
Simba sio ya MO bali ni ya mwekezaji pamoja na wanasimba hivyo kunahitajika kuifikisha simba katika mafanikio na sio mtu mmoja tu aendeshe timu bila kuweka ushirikiano na watu wengine maana kidole kimoja hakivunji chawa.