Tetesi: FIFA yadaiwa kuitaka Yanga kujieleza kwa tuhuma za kuichangia pesa za Uchaguzi CCM

Tetesi: FIFA yadaiwa kuitaka Yanga kujieleza kwa tuhuma za kuichangia pesa za Uchaguzi CCM

Mkuu Hersi alitamka wazi kwamba "klabu ya Yanga inatoa mchango wa Tsh 100M kwa Chama Cha Mapinduzi ".

Hiyo kauli inaonesha wazi kwamba ni azimio la klabu na sio kauli yake binafsi maana Rais wa klabu ndiyo mwakilishi wa juu wa masuala ya klabu.
Azimio la klabu haliwi hewani lina rekodi,bila shaka una rekodi za azimio hilo la klabu na pesa kutolewa akaunti ya yanga kwenda ccm
 
FIFA walichukulie hatua hili suala. Lakini kwa upande wa yanga tunaweza kumkana hersi. Hakuna kikao cha timu, wala nyaraka ya malipo kutoka yanga ilihidhinisha iyo pesa. Nitafurahi FIFA wakichukua hatua maana itakomesha kuchanganya mpira na siasa, lakini nitasikitika sana mtu mmoja(hersi) kutusababishia kifungo kwa sababu ya uchawa wake.
 
Kwani Hersi akimsajili Mkude huwa mnafanya naye kikao kwanza? Je, Mkude haichezei Yanga?
 
Kwa mujibu wa chanzo, Shirikisho la soka duniani FIFA limeitaka klabu ya Yanga inayoshiriki ligi kuu soka Tanzania bara kujieleza juu ya tuhuma za kushiriki Siasa kwa kukichangia pesa za uchaguzi chama cha mapinduzi CCM mwaka huu 2025.

Tamko hili la FIFA kwenda kwa Yanga ni matokeo ya malalamiko ya Chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA kwa FIFA, ambapo waliomba FIFA kuichukulia hatua Yanga kwa kitendo hicho, huku CHADEMA wakiahidi kutoa ushirikiano kwa FIFA watakapohitaji ushahidi.

Zaidi soma
Itakuwa FIFA ya kutoka Katavi au labda mitaa fulani ya kariakoo
 
Viongozi wanaweza kumkana na kumshughulikia kwa sababu hakuna kikao wala risiti ya malipo ya iyo hela. Tatizo viongozi wanaomzunguka wana ujasiri huo?
Hao viongozi walipaswa kumkana pale pale na kumshughulikia, ingeleta maana na ushahidi kuwa Yanga hawakuhusika ni tamko lake binafsi. Ila kukaa kimya hadi sasa ni kosa kubwa sana na inahitimisha kuwa wapo pamoja na raisi.
 
Wamechelewa kuchukua hatua lakini bado muda upo
 
Back
Top Bottom