Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata watoe miezi miwili huu sio muda wetu wa kulipa.tutamlipa WAKATI wa dirisha la usajili.View attachment 3109287
Katika uamuzi wa hivi karibuni kutoka kwa Mahakama ya Usuluhishi wa Migogoro ya FIFA (FIFA Dispute Resolution Chamber), Yanga SC, moja ya klabu maarufu za mpira wa miguu nchini Tanzania, imetakiwa kumlipa mchezaji wa zamani wa Bechem United, Augustine Okrah, kiasi cha dola za Kimarekani 24,400 sawa na Tsh 66,612,000.00/= kama fidia ya mshahara ambao haukulipwa wakati wa kipindi chake na klabu hiyo.View attachment 3109288
Mzozo huu unahusiana na kuondoka kwa Okrah kutoka Yanga SC, maarufu kama Wana Jangwani, baada ya mkataba wake kuvunjika kwa njia isiyofaa, hali iliyopelekea Okrah na timu yake kuwasilisha malalamiko kwa FIFA. Baada ya uchunguzi wa kina, FIFA iliamua kuwa Yanga ilikiuka makubaliano ya mkataba na hivyo ikaamuru malipo hayo kufanyika.
Zaidi ya malipo hayo ya dola 24,400, Yanga pia imepigwa faini ya dola 3,000 sawa na Tsh 8,190,000.00/= kwa FIFA, na inatakiwa kulipa ndani ya siku 30 tangu tarehe ya kuarifiwa kwa uamuzi huo. FIFA imetoa onyo kali kwa Yanga, ikisema kuwa iwapo hawatalipa kiasi hicho kwa wakati, klabu hiyo itakabiliwa na adhabu zaidi, ikiwa ni pamoja na marufuku ya kusajili wachezaji wapya kitaifa na kimataifa hadi watakapomaliza malipo yao.
Hii si mara ya kwanza kwa Yanga SC kujikuta katikati ya mvutano wa kisheria na wachezaji wake. Msimu uliopita, Okrah aliitumikia Simba SC, mahasimu wakubwa wa Yanga, kabla ya kurejea ligi kuu ya Ghana akiwa na Bechem United, lakini alijiunga tena na Yanga mnamo Januari 2024 kabla ya mkataba wake kuvunjika ghafla.
Kwa mujibu wa uamuzi wa FIFA, endapo Yanga watashindwa kulipa kiasi kilichopangwa ndani ya siku 45, watafungiwa kusajili wachezaji kwa vipindi vitatu vya usajili mfululizo, hali itakayoathiri vibaya mipango yao ya kujipanga kwa mashindano yajayo ya kitaifa na kimataifa.
Tupe kifungu mkuuHata watoe miezi miwili huu sio muda wetu wa kulipa.tutamlipa WAKATI wa dirisha la usajili.
😂😂😂Hili timu Kila mwaka lazima lipekwe FIFA Kwa madeni na ni tangu zamani hata kabla ya Hersi ni hivi hivi.Linaaibisha Sana ligi yeti.
Na matambiko ya supu ya vibuduTimu la ovyo badala ya kulipa wachezaji linatumia fedha hizo kununua mechi!
Aisee😂😂Na matambiko ya supu ya vibudu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Timu la matapeli, kazi kutapeli tu lipeni hela za watu matapeli wakubwa nyie. Mnaliabisha soka letu.
Mmeanza kubwataa, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Inawezekana pana mtu ananufaika na hizi faini wanazolipa mambo ya Afrika magumu sana..
Ni Rais Karia, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Namnukuu manara aliwahi kusema." Viongozi wa yanga pale walipo kwenye nguo zao za ndani kunanuka kinyesi."
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hili timu Kila mwaka lazima lipekwe FIFA Kwa madeni na ni tangu zamani hata kabla ya Hersi ni hivi hivi.Linaaibisha Sana ligi yeti.
Nimechungulia sana hapo sio bure haiwezekani watu faini wanachukulia kitu cha kawaida na kesho tena watafanya hivyo hivyo..Mmeanza kubwataa, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Pole sana Yanga jamani!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] lipeni madeni ya watu bhana.Nimechungulia sana hapo sio bure haiwezekani watu faini wanachukulia kitu cha kawaida na kesho tena watafanya hivyo hivyo..
Dawa ya deni kulipa😂[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] lipeni madeni ya watu bhana.