Kuna vitu huelewi.
1. TFF walijipa mamlaka ya kuamua kesi za jinai, kitu ambacho kisheria hakipo, hapo hiwezi kwenda FIFA unaenda mahakama za kiraia maana hiyo ni ukiukwaji wa katiba za nchi na sio katiba za FIFA. Lazima uelewe kua hakuna sheria yoyote ya taasisi yoyote ambayo inaweza kua juu ya sheria za nchi. Inapotokea kuna mkanganyiko kinachofuatwa ni sheria za nchi na sio sheeia za hiyo taasisi.
2. Hukumu ya TFF ilikua kinyume na katiba ya nchi, wambura alikua sahihi kwenda mahakama za kiraia na sio za FIFA.
3. Hukumu ya TFF ilishafutwa na mahakama kuu na TFF hawakupeleka hiyo taarifa ya mahakama kuu FIFA, hvyo fifa wameamua juu ya kesi hewa au mashtaka hewa ambayo yalishafutwa na mahakama kuu.
4. TFF wangetafta namna nyingine ya kudeal na wambura ila sio kutumia njia za kihuni na za kipumbavu kama walikua hawamtaki. Kwa hili wamechemka.
5. Wamburs bado ni makamo wa rais wa TFF.