FIFA yatuhumiwa kwa kumuwezesha Messi kushinda tuzo ya shirikisho hilo

Kwani fifa wameweka vigezo vya kumpata mchezaji bora kwa kuangalia takwimu au wanatumia kura za makocha na makapteni?
 
Sasa kura na mapenzi binafsi ndo hizo zishaleta shutuma
 
Kwani fifa wameweka vigezo vya kumpata mchezaji bora kwa kuangalia takwimu au wanatumia kura za makocha na makapteni?
wakitumia takwimu wakitumia kura za makocha bado atabeba messi-sababu hata hao makocha hadi wampigie mchezaji fulani ni sababu ya uwezo wa mchezaji ambao unatafasiriwa katika takwimu -kisha takimu zinajitafasiri katika upenzi.Hadi kocha amempenda mchezaji fulani kuwa ni bora maana yake amekubaliana na uwezo wake.
-messi anaongoza magoli La liga
messi anongoza kwa Magoli UEFA
 
Sasa kura na mapenzi binafsi ndo hizo zishaleta shutuma
Shutuma hazikosekani popote panapopigwa kura sababu lazima kutakua na either pande mbili au zaidi zinazokinzana.
Kikubwa ni kumpogeza aliyepewa, hata maandiko (bible) yanasema;- "Kura hukomesha mashindano; Hukata maneno ya wakuu." MITHALI 18 : 18.
 
Nakupa mfano mdogo tu......Giroud anapendwa sana na Didier Deschamps ....je, ndio kusema OG ni bora kuliko strikers wote wa France?Benzema,Lacazette, na wengineo wamepitwa nini na huyu jamaa
 
Ni UHUNI UHUNI UHUNI tu FIFA imejaa Rushwa tu,Ni Upumbavu uliopitiliza unaofanywa na hili genge la wahuni la FIFA,na ukifanyika uchunguzi vizuri kuna Award nyingi sana wamepewa kijanjajanja hao jamaa wawili.
 
Hamna rushwa hapoo hata kura za wa Egyptian zingehesabiwa zisingeweza kumfanya salah achukue tuzo na wasingeeza kumpigia mtu mwingine zaid ya salah kwa hiyo messi ana deserve mzigo washabiki wa VVD acheni wivu... Alafu salah mwenyew kmliza nafasi ya nne
 
Figisu tu!
Africa sisi sijui tynajua nini...!?
[emoji848][emoji848]
 
Kwa bahati mbaya au nzuri sasa hakuna zaidi ya messi kwa kizazi hiki hata hizo kura zinazingua tu....anaeujua hawezi kujificha....
 
Messi hakustahil kuchukua malalamiko ni kuwa kuna watu hawakumpigia kura ila wameona majina yao kweny list ya walio mpigia kura hii ni kamari maana kwa vyovyote vile watu walibet kweny Fifa kuwa either atachukua van dijk au ronaldo lakn fifa wakatwist mambo ili kujipatia faida kwa wale wenye bettings za messi hii mambo ni kamari tu na imeanza 2012 lakn kabla ya hapo Tuzo halali ndo zilikuwa zikitolewa
 
Watanzania bhana ka umpendi Messi isiwe sababu ya kupindisha ukweli. Hivi hiyo kura ya Egypt na Sudan ingemuondolea Messi kushinda hiyo tuzo.
Pili, msipende kuhukumu kisa umesikiliza upande mmoja wa shilingi.
Haya sasa FIFA wamesema kura ya Egypt iliharibika kwa sababu ilisainiwa kwa herufi kubwa na haikusainiwa na katibu wa soka wa Egypt.
Uzuri wa Fifa zile kura wanaziweka wazi.
Hata huyo wa sudani alitakiwa ampeleke malalamiko yake FIFA ili tupate majibu ya kutoka FIFA kuondoa ukakasi ka walivyofanya kwa malalamiko ya Egypt, sio anapiga porojo Kwenye mitandao ya kijamii
 
Daaaaaah usipende kuogozwa na hisia, aliyelalamika( tena Kwenye mitandao ya kijamii sio officially) ni mmoja tu wa Sudan.
Sasa kabla ya kuhukumu ungekua unatamani sana uwasikie FIFA. Kibaya zaidi ni kwamba huyo aliyelalamika Kwenye mtandao hajatutendea haki alitakiwa afanye ka alivyofanya wa Egypt.
Usihukumu kwa kwa sababu ya lawama ulizosikia upande mmoja.
 
Acheni mambo anaongoza la liga( La liga wanateuwa mchezaji wa bora wao) siju UEFA hapa hatafutwi mfungaji bora ingekuwa hicho ndio kigezo basi ni wazimu kumshindanisha mshambuliaji na beki haileti maana. Tofauti kubwa FIFA wanapiga kura makocha na captains wa team za Taifa na UEFA wanapiga kura makocha na captains wa team zilishoshiriki mashindano ya UEFA tu hakuna vigezo vingine. Tuseme maneno yako ni kweli wakati Modric anapewa mwaka jana vigezo gani?
 
Na kujibu zaidi hoja yako ya makocha kupiga kura nadhani wote tunajuwa makocha bora duniani wanafundisha team zinazocheza UEFA CL ndio wakampigia VVD sasa huku FIFA hata kocha wa Comoro anapiga na mara nyingi utakuta anapiga kura kwa ku support nchi ya mchezaji au vigezo vingine personal. mfano mdogo leo ingekuwa Mbwana Samatha yuko katoka list ni lazima kocha wa Tz angemchagua kwa kigezo wa kwetu lakini sio bora. Hoja hapa iweje amtu amchague fulani halafu FIFA waoneshe kamchagua mwingine hilo ndio shida na haina maana kwamba Messi hakustahili inaweza kuwa anastahili ila kura ziendane na zilivyopigwa. mtaani kwako ukipiga kura hata kama unayemtaka hakushinda lakini utajisikia raha kujuwa umechagua sio umepigia fulani halafu unasikia ambaye hujampigia kapata zote 100 utajiuliza kura yangu mbona sikumpigia huyu kapateje 100
 
Hizi tuhuma zingekuwa kwa #CR7,barca-la-puta fans wangeshajaza comments humu.
 
wanawake wana wivu sana .hata izo kura akipewa..haezi mzidi messi..na ile ni individual award,,sasa kuna nyumbu itataka ihusishe na makombe..na personal statistics zinambeba messi.....
Hapo wamejitkeza watatu ... What if wapo wengine wameamua kupotezea tu ...ni ujinga
 
wanawake wana wivu sana .hata izo kura akipewa..haezi mzidi messi..na ile ni individual award,,sasa kuna nyumbu itataka ihusishe na makombe..na personal statistics zinambeba messi.....
Mdau hajazungumzia makombe wala personal stats!!Kazungumzia kuchakachuliwa kwa kura!!!
 
Mashabiki wa barca na messi kwa ujumla,msijitoe ufahamu.Hoja ni kuchakachuliwa kwa kura,sio nani kaperform kuliko nani.Hamna anayepinga messi alikuwa na msimu mzur last season,vivo hivyo kwa VVD,Mbappe,Mane,Ronaldo,Salah,Becker kwa ufupi.Tafuteni njia nyingine ya kulikimbia hili
 
Safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…