Fight Night: Anthony Joshua ampiga kwa points Joe Parker

Fight Night: Anthony Joshua ampiga kwa points Joe Parker

Ila Joe Parker usipokuwa mwangalifu anakupa ndonga moja kwisha. Imebidi AJ apigane kwa makini bila kufanya makosa
 
skysports-anthony-joshua-joseph-parker_4270328.jpg


MATOKEO: Bondia Anthony Joshua wa Uingereza amefanikiwa kuchukua mkanda wa WBO baada ya kumpiga kwa points bondia Joe Parker wa New Zealand

Majaji katika ngumi hizo walimpa Joshua ushindi wa 118 - 110, 118 - 110, 119 - 109

Joshua sasa anamiliki mikanda ya WBO, IBF, WBA

======================

Hatimaye siku imewadia, mpambano usiotabirika kati ya Anthony Joshua na Joe Parker unatarajia kuvuta washabiki wa ngumi duniani.

Wote wakiwa hawajawahi kupoteza pambano lolote na wakiwa miongoni mwa mabondia bora wa zama hizi wanatarajia kuthibitishia dunia kuwa ni mabondia wasiopigika.

Joe Parker anatarajiwa kubadili kile kilichoshinda wengi akiwemo mkongwe Klitschko kwa kumlambisha sakafu Anthony Joshua.

Lakini Anthony Joshua ambaye kwasasa ndie star wa masumbwi duniani na mwenye washabiki kuliko bondia yeyote duniani anatarajiwa kushinda pambano hili kutokana na rekodi yake.

Anthony Joshua kama leo akishinda atakuwa amechukua mikanda minne kati ya mitano ya ubingwa wa dunia! Mkanda utaobakia wa WBC upo kwa Deontay Wilder.

Kama akichukua na huo atakuwa undisputed heavyweight champion of the world ikiwa ni mara ya kwanza kwa bondia kutoka UK baada ya Lennox Lewis miaka ya mwanzoni ya 2000.


What is your final predictions?

My friend MTAZAMO, thank u so much for updates!
 
AJ akipanda na Wilder , AJ atafia uwanjani

Wilder anatisha ingawa technically si mzuri!

AJ technically ni mzuri kushinda Wilder.

Ila wakipanda ulingoni sidhani kama itakuwa ni boxing match!

It will be a fight. Just not boxing.

Na wote wana power ila Wilder ana power zaidi.

Kwangu huo mpambano naona ni 50-50.

Kwa maana hiyo, nadhani whoever lands the first meaningful punch will win!
 
Wilder anarusha ngumi ovyo ovyo kama bata,AJ anashinda mapema,kwasababu ni fundi wa kurusha ngumi na anautulivu.
 
"l'm the king of the world, I'm the baddest. I need some one to prove me wrong. Some boxers claim to be the kings of the world but they don't want to fight me" Deontay Wilder.
 
AJ vs Wilder itakuwa vita kwelikweli
 
Sijui macho yangu maana naona vijana wametoka kama wanakwenda harusini sijaona mtu ana nunda au jicho limekuwa dogo. October 1 mwaka wa 1975 joe frazier na mohamed ali walikutana manila (thrilla in manila )round ya kumi na tano joe hakurudi ulingoni ali akawa mshindi lakini nae alikuwa hoi timu yake wakawa wanampepea nafsi kama inataka kutoka mara hivi. Kiukweli ule msisimko wa ngumi nzito jana sikuuona.
 
Back
Top Bottom