vibertz
JF-Expert Member
- Mar 15, 2022
- 2,474
- 4,726
Kwenye mpira wa miguu hakuna kitu kizuri kama kupambania timu na hilo ndilo ambalo limeifanya Yanga wafikie hapa walipo ukiachana na mbinu na ufundi wa kocha Gamondi. Viongozi wa Yanga wanaonesha wanataka kitu, wachezaji wanaonesha wapo tayari kupambana kufikia lengo na kila mechi wanacheza kama fainali. Kwa mchezaji yeyote anapopewa nafasi lazima aivujishie jasho timu yake kwa asilimia zake zote. Kocha Gamondi nae yupo kuhakikisha wachezaji wanajituma na kupambana ili kuipa Yanga mafanikio na ndio maana alionekana kutaka kumzaba mshika kibendera ambaye alionekana wazi kutaka kuharibu jitihada za wanajeshi wake wanaopambana kwenye vita.
Timu ya Yanga ndio wapo hivyo kila mechi wanacheza kama fainali japo performance haiwezi kuwa sawasawa kwa kila mchezo ila wapo kupambania matokeo. Kwa upande wa wachezaji wa Simba fighting spirit yao huwa ni pale tu anapokuja mwalimu mpya, makocha wote wapya wanaopewa timu ya Simba hushinda mechi zao na wengine hushinda kwa kishindo kiasi kwamba uwezi kuamini kama ni Simba hii ndio iliyosua sua dhidi ya kocha aliyetangulia.
Benchikha wakati anaanza kuifundisha Simba mashabiki wa Simba waliona kuwa timu sasa ndio hii, na kocha ndio huyu. Watu wakasifia wachezaji wamebadilishwa mno na wakasema wanaona mwanga sasa juu ya Simba yao japo kuna baadhi ya watu wakatoa rai kuwa hii ni spirit kwavile ni kocha mpya tu ila muda ukatoa majibu hadi Benchikha akabakia benchini peke yake.
Hili ndio hilo hilo lililopo sasa kwa Simba ya Mgunda, wachezaji wameamua kujituma na kupambana kwavile ni kocha mwingine na wengine mikataba inaenda ukingoni hivyo lazima kuonesha wanastahili kubaki, ila sio mbaya mashabiki wakajaribu kupatiwa hitaji lao ili wathibitishe kwa uhalisia kuhusu uwezo wa kocha wao wanaomtumainia, wanaompigia chapuo kukabidhiwa timu moja kwa moja. Mgunda apewe timu msimu ujao wote aiongoze Simba