Fikra inayodai Mwanaume hapaswi kuchelewa kupata mtoto tumeipata wapi?

Fikra inayodai Mwanaume hapaswi kuchelewa kupata mtoto tumeipata wapi?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kwamba Mwanaume hupaswi Kuchelewa kuwa na Mtoto na kwamba unatakiwa kuwa na Mtoto kuanzia Umri wa Ujana na kwamba ukiwa na Miaka kuanzia 45 kwenda mbele hadi 50 au 55 hapo ukipata Mtoto wako wa Kwanza utaitwa Mchelewaji wa kuwa na Mtoto na kwamba hutoweza Kumlea vizuri na sijui atakuwa anakuita Babu na siyo Baba kama wanavyoitwa Wengine waliowahi Kuzaa wa Kwao.

Halafu ni waswahili haw hawa ambao leo hii wanakucheka na kukusema vibaya kuwa unachelewa Kuzaa Mtoto / Watoto ila ukiwahi Kuzaa Mtoto / Watoto kama watakavyo (ili uwafurahishe ) na kushindwa Kuwalea vyema hao hao wanaanza Kukukalia Vikao na Kukucheka na kukuambia nani alikuambia uwahi Kuzaa ( kuwa na Familia ) kama uliona huna Uwezo wa Kulea na Kuhudumia?

Ndiyo maana Kutwa ninasema hakuna Watu WANAFIKI duniani kama Watanzania na ukiwasikiliza tu Wao umeumia.
 
Bongo watu wanafanya mambo kwa kuigana sana ila binafsi naamini katika maisha hakuna kuwahi wala kuchelewa utakachokipata basi ndio muda wake umefika.

Ukipata mtoto na umri wa miaka 26 na mimi nikipata mtoto na umri wa miaka 35 wewe utaniona mimi nimechelewa na mimi nitakuona wewe umewahi...ila kuna mwengine yeye kapata mtoto akiwa na miaka 19 atamuona wa miaka 26 kachelewa so hakunaga hoja ya msingi kwenye kuchelew na kuwahi.
 
Bongo watu wanafnya mambi kwa kuigana ila binafsi naamini katika maisha hakuna kuwahi wala kuchelewa utakachokipata basi ndio muda wake umefika.

Ukipata mtoto na umri wa miaka 26 na mimi nikipata mtoto na umri wa miaka 35 wewe utaniona mimi nimechelewa na mimi nitakuona wewe umewahi...ila kuna mwengine yeye kabapata mtoto akiwa na miaka 19 atamuona wa miaka 26 kachelewa so hakunaga hoja ya msingi kwenye kuchelew na kuwahi.
Kula Gwala / Tano Mkuu kwa post iliyoshiba Madini.
 
Ukizaa na miaka 55 utasababisha wajukuuu zako wasimwone babu yao,maana at 75yrs utakuwa zako ahera madukani.
Utafiti unaonesha vizazi vijavyo kuna watu watakuwa wanaona babu zao youtube na kwenye picha,maana vijana wa sasa wanachelewa kuzaa.
 
Nikiwahi huko Kuzaa na nikashindwa Kuwalisha na Kuwahudumia hao Watoto wangu nikikuletea Kwako utawalea au?
 
Ukizaa na miaka 55 utasababisha wajukuuu zako wasimwone babu yao,maana at 75yrs utakuwa zako ahera madukani.
Utafiti unaonesha vizazi vijavyo kuna watu watakuwa wanaona babu zao youtube na kwenye picha,maana vijana wa sasa wanachelewa kuzaa.
Kuna umuhimu gani wa wajukuu kumuona babu yao?
 
Hii mentality itachukua muda sana kututoka "waswahili" Mimi niliwaambia wazee wangu, my life my business, mmenizaa, kunilea na kunikuza inatosha na nawashukuru, mambo ya nitaoa lini, watoto niwe nao wangapi sio jambo lenu, naomba mniheshimu katika hilo.
 
Safi sana Kudadadeki...!!
 
Back
Top Bottom