Neemawalterr
New Member
- Sep 5, 2022
- 1
- 1
Ni ukweli kabisa usiopingika kwamba serikali na mashirika ya siyo ya kiserikali yamejikita mno katika kuongeza fursa za wanawake ili waweze kujikwamua kiuchumi. Jambo hili ni faida kubwa kwa nchi yetu, kwani takwimu zinasema kampeni hizi zimepunguza umaskini Tanzania kutoka 34.4% kwenda 26.4% kutoka mwaka 2007-2018. Bado kampeni hizi zinaendelea na hivi sasa serikali imeelekeza jicho kwenye kupindua vipingamizi vyote vinavyokwamisha jitihada za kuwawezesha wanawake kama vile, umiliki wa ardhi, kupunguza idadi za mimba na ndoa za utotoni, kupunguza idadi ya mabinti wanaoshindwa kuhitimu masoma yao n.k.
Jitihada hizi zinahitaji pongezi kubwa sana maana tunayaona mabadiliko katika nchi yetu lakini kuna upande ambao unapuuzwa na haupewi nguvu inayohitajika. "FIKRA". Zipo fikra zilizotapakaa na kuonekana jambo la kawaida sana au kama utamaduni wa Tanzania yetu.
Mpenzi msomaji, fikra hizi najua sio ngeni kwako kabisa, hilo nakuhakikishia, na hii inaonyesha ni jinsi gani tatizo hili ni pana sana na linaelekea kuwa kitu cha kawaida kama halitaongelewa na kuwekwa sawa ili mabinti waachane na fikra hizi na kizazi kijacho kisibebe fikra hizi.
Sitaki kuuzunguka mbuyu kwa mda mrefu, jambo hilo ni " MAHUSIANO NA NDOA KUFANYIKA KAMA KITEGA UCHUMI KWA WANAWAKE HASA MABINTI".
Utasikia mabinti wakisema "mimi siwezi kuwa na mwanaume asiweza kunisaidia matatizo yangu, yaani akimaanisha asiyekuwa na fedha. Mabinti wanashauri pia mabinti wenzao kufanya vivyo hivyo.
Jambo hili lipo hata kwa wazazi wetu yani mzazi anamwambia binti yake hakikisha unapata mwanaume wa kueleweka na kueleweka huko wanamaanisha WENYE FEDHA.
Mara nyingi nikiwa naongelea swala la kutafuta fedha na kufanikiwa sana katika maisha na ugumu uliopo katika kufikia malengo na uhuru wa kipato, wanaume walionizunguka utasikia wakisema "afadhali wewe ni mwanamke, huna sana presha ya maisha kama sisi wanaume" au wengine watasema "hauna haja ya kuwaza sana maisha au kupitia magumu sana katika kutengeneza maisha bora kwavile utaolewa tu". Je kuolewa ndo kipato kwa mwanamke?? Kuolewa ndiko kutakaponipa uhuru wa kipato?? Laahasha!!!
Utasikia mke anasema "baba fulani leo wamekuja wageni hawatoshi maana nyumba yako ni ndogo". Katika sentensi hii ni wazi kabisa mwanaume ataanza kufadhaika na kuchekecha akili ni kwa namna gani ataongeza ukubwa wa nyumba yake. Je ni afungue biashara? Au atafute kazi na vibarua vya ziada?. Lakini kwa mwanamke huyu akili yake inakuwa ishajiwekea ya kuwa hausikii na hivyo akili haitawaza ni jinsi gani ya kuongeza kipato ili aweze kuongeza ukubwa wa nyumba yao.
Je wajua kwa nini wanaume huwa wanapambana sana kutafuta fedha? Kwasababu wamejengewa dhana ya kwamba "mwanaume anapaswa kutunza familia, anapaswa kujenga, kulipa mahari, kumtunza mpenzi wake, kusomesha watoto, kununua magari, kuwekeza, kufungua biashara mbalimbali na kuwapa maisha mazuri familia yake". Je dhana hii ikiwekwa pia kwa mwanamke uchumi utapanda kiasi gani?
Ifike mahali sasa na wanawake tujue kwamba tunatakiwa kupambana sawasawa na mwanaume maana majukumu hayo yanatuhusu pia. Tukifanikisha hili hakika uchumi wa nchi utapanda, familia zitakua bora zaidi, maisha yatakua mazuri zaidi.
Kuinua uchumi wa familia, jamii na nchi kiujumla inamwitaji mwanamke na mwanaume kusaidiana, na sio mwanaume kumsaidia mwanamke tu. Kila mtu anapaswa kuweka nguvu ileile katika kutafuta maisha mazuri, kukimbilia fursa zilizopo na kutengeneza fursa ili Tanzania yetu iwe juu.
Iwe hivi, binti atafute maisha akijua anapaswa kujitunza yeye, familia yake na jamii na kijana afanye vivyo kisha upendo uwalete watu hawa pamoja. Hakika familia zenye uwezo wa kifedha zitaongezeka maana itakuwa kama majembe mawili yamekutana kutengeneza "tractor". Watapeana nguvu zaidi, mawazo yenye tija, elimu za fedha, talanta na mipango mikakati yenye ubunifu wa kuendelea kuwasogeza mbele.
Wahenga walisema KIDOLE KIMOJA HAKIVUNJI CHAWA, inapaswa tuwe sambamba katika kutia nguvu kwenye kuukimbia umaskini. Mwanamke waza kununua kiwanja, kujenga, kusomesha watoto, kusaidia ndugu na jamaa, kuwekeza na kukuza mitaji, kumtunza mumeo sawa na mwanaume anavyowaza kumtunza mkewe.
TUWAJIBIKE SOTE, wanawake na wanaume, kujipa sisi na familia zetu maisha mazuri maana hapa ndipo UKUAJI WA UCHUMI WA TAIFA unapoanzia.
Ni kwa jinsi gani tunaweza tengeneza jamii yenye fikra sahihi na tamaduni hii mpya??? Kwanza kabisa kuwepo na kampeni mbalimbali zinazobadili fikra za sasa na kujenga fikra mpya kwamba maisha bora yatafikiwa kwa haraka zaidi kwa kuwepo na jitihada sawa baina ya mwanamke na mwanaume katika kutafuta kipato.
Vilevile kuwapa mabinti motisha mbalimbali na kutambua jitihada za wanawake wapambanaji. Wanawake hawa watafanyika chachu kwa wengine.
Jambo lingine ni kuondoa uwoga wa kufeli na kujaribu kwa mabinti. Wanawake wengi wanakua na hofu ya vipi kama nikifeli itakuaje? Ifike mahali sasa ambapo hatutajali jamii itatuonaje tukifeli au tusipofanikiwa. Wanawake watoke na kwenda kujaribu vitu mbalimbali ili kuweza kuitambua ZAWADI KUBWA waliyojaliwa na mwenyenzi Mungu katika upambanaji na uwezo wa kufanikiwa katika kazi zao.
Tuzidi kutengeneza majukwaa mbalimbali yatakayoweka FIKRA sahihi kwa wanawake.
Tukaijenge Tanzania ya wapambanaji wa jinsia zote. Tanzania yenye wanawake na wanaume wenye uchu sawa wa maendeleo. Wanawake na wanaume watakaoungana kuleta mafanikio yao binafsi, mafaniko ya familia zao, mafanikio ya jamii zao na taifa kiujumla.
Mungu wabariki wanawake, Mungu wabariki wanaume, Mungu ibariki Tanzania yetu.

Upvote
1