1. Hii ni promotion campaign, huwa zina malengo 3
i Kufahamisha walengwa juu ya uwepo wa huduma/bidhaa
ii Kukumbusha, inawezekana aliyefahamishwa anakumbana na bidhaa/huduma shindani nyingine hapa promotion inatumika kumkumbusha mteja
iii Kuhamasisha/Kuvutia/Kushawishi, mtu ambaye ameisha kumbushwa sasa anapewa taarifa za ziada zaìdi ili kumshawishi kutumia bidhaa zaidi
Mzunguko wa malengo hayo 3 ni jitihada za kila za kila siku za mfanyabiashara timamu ambaye ana bidhaa/huduma timamu
Na ndio maana Cocacola mpaka leo hii kila siku ya Mungu wako kwenye Promotion
Muitikio/Impact yake imeanza kuonekana mapema sana baada ya wapinzani wetu ktk biashara hìi kuanza kutengeneza Fabricated Scandals
Hii nilikuwa najibu hoja kuwa hakuna asiyejua Tz na vivutio vyake vya Utalii ?
2.Zaidi ya hapo tuende mbele zaidi, vivutio vilivyopo Tz na idadi ya Watalii wanaozuru Tz mbona inaonyesha Watalii ni wachache ukilinganisha na nchi ambazo vivutio vyake havifiki hata 1/8 ya vivutio vilivyopo Tz
3. Pesa zilizotumika
Wa Tz wanalalamika kwamba, Mama anafubaza 11 billion kuzindua hiyo Royal Tour
Ukweli ni kwamba hizo pesa hazitolewi na Serikali
Lakini hata kama zingekuwa zinatolewa na Serikali unaweza kulinganisha na zile 78 billion tulizozizika pale Chato Airport ?
Ukitaka kujua impact ya 11 billion iliyotumika waulize wakazi wa Arusha
4. DFI
Promotion ya Royal Tour ina lengo la ku promote Makampuni Makubwa ya Utalii na Yasiyo ya Utalii directly. Hii inaitwa Direct Foreign investment
DFI imekuwa kigezo kikubwa cha economic growth kwa nchi nyingi duniani. Nchi kama UAE haina mafuta mengi kama tunavyodhani ukilinganisha na Nigeria. Lakini UAE iko mbele kiuchumi kuliko Nigeria, why ? Because of DFI
Na ndio maana unaona watu wenye akili kama JK alimuomba Mtz (Ms Komwihangiro) aliyekuwa very successful ktk South Africa Investment Centre aje Tz kusukuma gurudumu la DFI mtu mmoja anakuja kumtimua kazi kama house girl
It's very painful kwa watu wanaojua dunia inaendaje
Tutembee kifua mberee sisi ni Matajiriiii
Wawekezaji watatufuata wenyeweee
Nina swali mkuu…
Haya makampuni makubwa ya utalii hapa Tanzania yanamilikiwa na Watanzania ?! Na km jibu ni ndio..je ni kwa asilimia ngapi?!