Filamu ya Royal tour ni janja ya mabeberu kujipatia pesa kupitia sekta ya utalii



Nina swali mkuu…

Haya makampuni makubwa ya utalii hapa Tanzania yanamilikiwa na Watanzania ?! Na km jibu ni ndio..je ni kwa asilimia ngapi?!
 
Kwani kujitangaza lazima tushoot royal tour?
Ni mojawapo ya ubunifu mzee, CBS ni television iayoangaliwa bara la america na europe, kwa hiyo hapo coverage inakuwa kubwa, na Mama kuenda mwenyewe kuizindua na kukutana namanguli wa utalii ni bonge la mileage.Kaka post covid usipopambana hutoboi, sekta ya utalii ni nyeti na competitive sana hivyo ubunifu kama huu kaupiga mwingi sana. Badilisha mindset kiongozi, otherwise utabaki na vivutio vyako like white elephant.
 
Nina swali mkuu…

Haya makampuni makubwa ya utalii hapa Tanzania yanamilikiwa na Watanzania ?! Na km jibu ni ndio..je ni kwa asilimia ngapi?!
Kama watanzania hawamiliki ulitaka tuendelee hivi? Vijana hawana ajira watu wanatafuta jinsi gani ya kupanua wigo wa fursa za ajira. Sisi tunapata watalii wastani wa 2million kwa mwaka lakn kuna nchi Kama mkuu amesema hapo juu misri wanapata hadi 30 million ya watalii kwa mwaka. Mnataka tubakie hapa? Munaogopa dunia? Pambana na dunia kwa akili na wewe upate. Mnakua na rigid minds. Mabeberu mabeberu so what tujifungie wasije?
Unadhani wawekezaji wautalii ndo watakuja tu?
Na watanzania Wana makapuni ya utalii.
Tusiwe na akili za kimasini tutabaki hivi hivi na kuporomoka zaidi.
 
Haya nenda kajikatie kakipande kako kule Chato upate kuzikwa na yule jamaa kutoka Burundi.
 


Kwahio unampa beberu nyama unabaki na mifupa ili mradi kijana wakutoa nyama kwenye mifupa apate ajira….hii akili kweli
 

Kweli hata wajinga huzeeka. Kwa mda mmoja wewe ni mjinga na mpumbavu kweli kweli. Biashara ni matangazo we huoni nchi nyingi zinatangaza utalii wao we huoni makampuni makubwa yene mauzo makubwa bado yanaendelea kutangaza huduma na bidhaa zao Tanzania [emoji1241] bado utalii wetu haujafanikiwa tuna vyanzo vingi sana vya utalii hivyo bado hatuna watalii wa kutosha na ndio maana tunafanya jitihada za kuendelea kujitangaza haimaanishi mukesh ambani akinywa maji ya uhai basi ndo management ya maji hayo waache matangazo ya hio bidhaa bali wataendelea kutangaza zaidi na zaidi, Mbona mambo yapo wazi kibiashara wajinga nyie au mnata nini maana kila linalofanyika nyie mnalinanga.
 
Na kwanini uzinduzi ufanyikie Marekani badala ya Tanzania ambapo tungepata wageni wengi maana hoteli, fedha za kigeni na wageni wangeweza kutembelea mbunga zetu?
 
Chifu Hagaya ageuka kituko duniani. Eti ni mcheza filamu. Ujinga mtupu na hasara kwa Taifa.
 
Rais wa nchi hawezi kukaa wiki nzima nchini Marekani kwa maigizo ya kisanii ya Royal Tour.

Royal Tour ni chaka ya yaliyojificha nyuma yake. Lipo jambo zito kuhusu Royal Tour nchini Marekani.

Kwa kadiri tunavyoendelea kutizama yanayojiri, tutajua vingi zaidi.

Kwa vyovyote vile, Tanzania itabaki salama.
 
Hii Nchi ina vichwa ngumu sana, hivi wakati watalii nje huko wanaambiwa Mlima Kilimanjaro na hifadhi ya Serengeti vipo Kenya ilikuwa sahihi au? . Je Rais hapo amefanya mazingaombwe au viini macho gani kutangaza raslimali za Tanzania kwa maslahi ya Watanzania?.
 

Huna akili na hauko exposed hata kwa level ya Kitongoji unachoishi. Pole
 
Watu ni wajinga sana. Ni mtu gani asiyejua kuhusu coca cola umeshawahi kuona hawajitangazi.

Nchi ilikuwa inaongozwa na mchungi.

Kwa ivo kwa ujinga wako consumption behavior ya coca cola unaifananisha na lasting experience ya utalii let’s say serengeti au zanzibar kwamba itakua repetetive? I bet hujawahi kutembelea popote kutalii bongo
 
Huna akili na hauko exposed hata kwa level ya Kitongoji unachoishi. Pole
Naona upo exposed kuwaona wengine hamnazo ila wewe upo vizuri. Ndiyo maana nimeandika kuna vichwa vigumu nadhani hiki ni kichwa kigumu ambacho ni exposed one. Hongera
 
.....ameshakaa sasa eheee...
 
Ila yule mzungu kamchukulia poa sana rais wetu sijui kwa sababu ni mwanamke maana hata akipiga nae picha anajiachia tu, alitaka hadi rais wetu akaogelee nae na kuruka nae sijui sarakasi dah!

Safari hii tumepatikana.
 
Ila yule mzungu kamchukulia poa sana rais wetu sijui kwa sababu ni mwanamke maana hata akipiga nae picha anajiachia tu, alitaka hadi rais wetu akaogelee nae na kuruka nae sijui sarakasi dah!

Safari hii tumepatikana.
Jamani huyu Bwana Peter Greenberg alitangulia filamu za Royal Tour huko Jordan (akiongozana na mfalme Abdallah), Israeli (na Netanyahu), Newzealand (na waziri mkuu Clark), Mexiko na Rwanda (pamoja na maraisi Calderon na Kagame). Hao wote waliiona kama nafasi nzuri kupigia debe utalii wa nchi zao, labda pamoja na hamu ya kubadilisha kidogo kawaida za mkuuwa nchi.....
Ni fomati iliyobuniwa na huyu Greenberg; sidhani kiongozi yeyote aliyeshiriki alipata senti moja . Kinyume, nikisikia gharama, inaonekana Greenebrg alihamasisha serikali husika kugharamia safari ndani za nchi. Ikivuta watalii, bila shaka inafaa kuwekeza pesa hivyo.
Yale makelele kuhusu filamu ya Tanzania / Samia inatoka wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…