Ujinga wa bongo movie hata kama wali plan kuigiza stori aidha ya kweli yenye maudhui mazuri hata kama stori hiyo ilipaswa kuchukua dakika 45 kukamilika, wao watai-extend kwa kujizungusha zungusha ili mradi tu zitoke mbili wapate ulaji (part1&part2)
Kero zitaanza, vitu ambavyo havikua na umuhimu kuvionesha wao wataziongeza ili kufikisha lengo lao. Mfano scene inazungumzia dada wa kazi akimuwekea dawa kwenye chakula mama mwenye nyumba ili ammiliki mumewe.
Basi hapo wanaweza kuonesha situation nzima iliyofanyika jikoni kuanzia kuchambua maharage mpaka stage ya kuiva ili mradi tu muda uende. Mpaka unajiuliza hii ni movie au tutorial ya mapishi?
Unakuta baada ya dakika nyingi kupita unaona binti ameandaa msosi, sasa yule mama mwenye nyumba anamega tu tonge unakuta maandishi eti "watch out part two" goddammit hizo dakika mlizozipoteza kwenye uchemshaji wa maharage kwanini msikate hiyo scene muweke muendelezo?