Melubo Letema
JF-Expert Member
- Apr 1, 2020
- 416
- 414
KATIBU Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania, Filbert Bayi anadaiwa kuhusika na ufisadi wa fedha zinazotolewa na Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) kwa ajili ya maendeleo ya mchezo wa riadha hapa nchini.
Taarifa zilizoifikia Tanzania PANORAMA Blog kutoka kwa wadau wa mchezo wa riadha walio karibu wa TOC zimedai kuwa, Bayi ambaye sasa amekuwa kiongozi wa kamati hiyo kwa zaidi ya miaka 20 amekuwa akitia kibindoni kwake fedha zinazotolewa na IOC ikiwa ni pamoja na mradi wa michezo ulio chini ya Olimpafrica.
Katika mlolongo wa tuhuma zilizotolewa, inadaiwa IOC ilitoa fedha za ujenzi wa shule za michezo kwa nchi mbili za Afrika, moja ya nchi zilizonufaika na fedha hizo ni Tanzania lakini shule iliyojengwa ipo Dole, Zanzibar huku Tanzania Bara ikiwa haipo.
Kwamba, IOC imekuwa ikituma wakaguzi kwa ajili ya kukagua mwenendo na maendeleo ya shule hizo lakini kila wanapotua nchini, vibao vya kuitambulisha Shule ya Fibert Bayi hubadilishwa na kuwekewa vibao vingine mpaka wakaguzi hao wanapoondoka ndipo hurudishwa vibao vyake vya awali.
KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC) jana (3/5/2022) iliitisha Tanzania PANORAMA Blog kuhusu hatua yake ya kuripoti habari zinazomuhusisha Katibu Mkuu wa kamati hiyo, Filbert Bayi na ufisadi wa fedha zinazotolewa na Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kwa ajili ya kusaidia na kuendeleza shughuli za michezo hapa nchini.
Sambamba na hilo, TOC iliwatumia waandishi wa habari wa Serikali wa magazeti ya Habari Leo na Daily News kujaribu kuizuia PANORAMA Blog kuendelea kuripoti habari hizo.
Bayi, ambaye jana aliiita PANORAMA Blog ofisini kwake Kibaha kwa ajili ya kujibu maswali iliyomuuliza, ilimkuta akiwa na watu wengine saba aliosema amewaita wamsaidie kujibu maswali hayo kwa sababu ni watu wa karibu yake na wanaofahamu kinachoendelea ndani ya TOC.
Miongoni mwa watu hao, Bayi alimtambulisha Makamu Mwenyekiti wa TOC, Henry Tandau, waandishi wa habari wawili aliosema wanaandikia magazeti ya Daily News na Habari Leo ambao walishirikiana kwa karibu na Tandau kumkingia kifua Bayi.
Akijibu kwa niaba ya Bayi, Tandau ambaye alitumia dakika kadhaa kujigamba kuwa nguli wa uandishi wa habari aliyepata kufanya kazi na waandishi wa habari wanaoheshika nchini na wenye madaraka makubwa Serikalini kwa sasa, aliilaumu PANORAMA Blog kumuuliza maswali hayo Bayi kwa kile alichosema yanaelekeza cha kujibu na yameandaliwa na mtu mmoja na kupelekwa Bungeni, Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na PANORAMA Blog.
BAADA ya kutishia Tanzania PANORAMA Blog kuipeleka mahakamani kwa kuibua kidogo ‘madudu’ ya Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kamati hiyo sasa ikishirikinana na wapambe wake, waandishi wa habari wawili inapanga kujisafisha kwa kutumia vyombo vya habari.
Mkakati wa TOC baada ya kushindwa kujibu maswali na hoja za msingi walizoulizwa na PANORAMA ni kuitisha mkutano waliodai kuwa wa waandishi wote wa habari wenye lengo la kukanusha tuhuma zinazoelekezwa kwao.
Mkutano huo utawahusisha Katibu Mkuu wa TOC, Filbert Bayi na Makamu Mwenyekiti Henry Tandau, Kamati ya Utendaji pamoja na waandishi wa habari hao wawili na ambao TOC imeeleza kuwa itautumia kujibu maswali ya tuhuma za ufisadi zinazoelekezwa kwa Bayi na TOC.
ALIYEKUWA Mweka Hazina wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Charles Nyange amesema aliacha kazi katika kamati hiyo kwa sababu ya kulinda heshima yake na heshima ya taaluma yake.
Nyange ameyasema hayo leo alipozungumza na Tanzania PANORAMA Blog iliyomuuliza sababu zilizomuondoa kwenye utumishi wake huo na iwapo katika kipindi cha utumishi wake ndani ya TOC alipata kukutana na vikwazo vya aina yoyote katika utendaji wake.
Katika majibu yake mafupi, Nyange alisema yeye ni mhasibu kitaaluma hivyo aliamua kuacha kazi kwa hiari yake kwa sababu wanataaluma wenzake wangemshangaa lakini hakuwa tayari kufafanua zaidi wangemshangaa kwa sababu zipi.