Financial Education, hata Mabenki hawataki mteja aipate

Financial Education, hata Mabenki hawataki mteja aipate

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2011
Posts
7,872
Reaction score
9,263
Mabenki wanaweza wapatia wateja wao kila aina ya elimu ila sio Financial educaion, hio hawawezi itoa hata kwa bunduki make wanajua itawakosesha wateja wengi sana.

Na ukweli ni kwamba upigwaji kwenye mikopo ni kwa sababu watu hatuna elimu ya kifedha hilo ndio tatizo, hakuna tatizo jingine. Asilimia kubwa ya wakopaji hawana hiyo elimu na Mabenki hawataki kabisa watu waipate.

Mtu anakopa ukianza kumuuliza maswali unaona kabisa hapa kuna shida kubwa sana.

Kuna Project moja tulikuwa tunafanya na NGO moja kubwa sana, sasa ikawa inahusu kufanya kazi na Benki mojawapo kubwa sana Tanzania. Project ilihusu pia kutoa elimu ya kifedha kwa wanavikundi then wawe linked na Benki kwa ajili ya Saving na Loan, Sasa kwenye swala la Financial education hapo Benki wakakataa wakasema itolewe tu Financial linkage education na tuachane na Financial education.

Hawakuweka wazi sababu za kukataa Financial education ila tulijua tu sababu ni itaenda kinyume na siri zao za kukopesha.

Kwenye kukosa elimu ya kifedha hapo ndio Mabenki na hizi taasisi zingine zinazotoa mikopo wanakotajirikia. Ukiona walimu sijui wafanyakazi wanalia lia na mikopo kisa ni Financia education hawakuwa nayo na wangekuwa nayo wangeweza hata kughairi kwenda kukopa pesa.

Mabenki wanaweza toa sana elimu za ujasiriamali ila sio elimu ya kifedha.

Ni elimu inayopaswa kutolewa sana kwenye jamii hasa walimu ambao ni wahanga wakuu wa mikopo, shida nani anatoa hio elimu?
 
Kweli mkuu mtu anakopa pesa ananunua gari anaenda nayo kazini anaipaki kuanzia asubuhi mpaka jioni.

What a waste of money yaani more than 30 million or 20 million unaipaki kuanzia asubuhi tena mkopo hapo bado garage bado mafuta yaani ni uzuzu inatakiwa ukikopa ufanye kitu cha kuingiza hela sio unaenda kuzika pesa na jamii imeshamezeshwa tayari na ni ngumu kuelewa.
 
Last week my phone iliharibika nikaenda duka moja kukopa simu, nilikuta imebandikwa stiker 570k, nikaangalia ile simu sokoni ni 400k, nikasema sio mbaya maana nikikosa simu shughuli zangu zitasimama, nikaanza process zote kwenye kumaliza mpaka jioni naomba statement nakuta natakiwa kulipa 860k, bahati nzuri nilikua sijalipa malipo ya awali nikawaomba samahani kwa usumbufu nikatoka.
 
Kwa mfano ni elimu gani ya fedha ambayo benki hawatoi kwa wateja?
Mfano kuna account' X 'mteja anafungua na wao benki wanakwambia akaunti hii itakuwa inazalisha faida 'Y' baada ya Muda 'Z'

Benki hawawezi kukwambia limitation za akaauti hiyo ambayo zinafanya ukose Ile faida utakayoipata, mathalani unatakiwa utoe pesa mara ngapi kwa mwezi ili usivuruge terms, matokeo yake watu wanakosea terms akaunti haitoi faida na benki hawawaelezi wateja wanapokosea, maana wakifanya hivyo benki itapata hasara kwa kulipa faida zinazozalishwa kwenye akaunti za wateja.
 
Mfano kuna account' X 'mteja anafungua na wao benki wa kwambia akaunti hii itakuwa inazalisha faida 'Y' baada ya Muda 'Z'
Benki hawawezi kukwambia limitation za akaauti hiyo ambayo zinafanya ukose Ile faida utakayoipata, mathalani unatakiwa utoe pesa mara ngapi kwa mwezi ili usivuruge terms, matokeo yake watu wanakosea terms akaunti haitoi faida na benki hawawaelezi wateja wanapokosea, maana wakifanyaje hivo benki itapata hasara kwa kulipa faida zinazozalishwa kwenye akaunti za wateja.
Uongo, ingekuwa kweli hiyo ni fursa ya kupiga pesa kupitia fidia.
Taarifa zipo wazi kwenye maandishi. Ukiwa unafungua akaunti yoyote soma zile terms and condition na soma contract kila kitu kimo mule. Kama kuna kitu hakimo na kikafanyika bila makubaliano hiyo ni fursa kwako.

Unadhani wanaofungua akaunti wote ni vilaza? Kila siku ungesikia kesi mahakamani watu wakidai fidia iwapo kuna ukiukwaji wa taarifa.
 
Kweli mkuu mtu anakopa pesa ananua gari anaenda nayo kazini anaipaki kuanzia asubuh mpaka jioni what a waste of money yaani more than 30 million or 20 million unaipaki kuanzia asubuh tena mkopo hapo bado garage bado mafuta yaani ni uzuzu inatakiwa ukikopa ufanye kitu cha kuingiza hela sio unaenda kuzika pesa na jamii imeshamezeshwa tayari na ni ngumu kuelewa.
Huwezi kuona kwenye Atm, Kuna gharama za miamala!
Zile karatasi zinazotupwa kwenye dust bins benki wameshachaji!!! Laiti kama watu wangejua gharama za kutaka Ile receipt ambayo wanasoma tu balance na kuitupa kwenye bin , wasingeitaka Ile receipt , na benki zingekosa mapato,
 
Mabenki wanaweza wapatia wateja wao kila aina ya elimu ila sio Financia educataion, hio hawawezi itoa hata kwa bunduki make wanajua itawakosesha wateja wengi sana.

Na ukweli ni kwamba upigwaji kwenye mikopo ni kwa sababu watu hatuna elimu ya kifedha hilo ndio tatizo, hakuna tatizo jingine. Asilimua kubwa ya wakopaji hawana hio elimu na Mabenki hawataku kabisa watu waipate.

Mtu anakopa ukianza kumuuliza maswali unaona kabisa hapa kuna shida kubwa sana.

Kuna Project moja tulikuwa tunafanya na NGO moja kubwa sana, sasa ikawa inahusu kufanya kazi na Banki moja wapi kubwa sana Tanzania. Project ilihusu pia kutoa elimu ya kifedha kwa wanavikundi then wawe linked na Banki kwa ajili ya Saving na Loan, Sasa kwenye swala la Financial education hapo Benki wakakataa wakasema itolewe tu Financial linkage education na tuachane na Financial education.

Hawakuweka wazi sababu za kukataa Financia education ila tulijua tu sababu ni itaenda kinyume na siri zao za kukopesha.

Kwenye kukosa elimu ya kifedha hapo ndio Mabenki na hizi taasisi zingine zinazo toa mikopo wanako tajirikia. Ukiaona walimu sijui wafanya kazi wanalia lia na mikopo kisa ni Financia education hawakuwa nayo na wangekuwa nayo wange weza hata kughairi kwenda kukopa pesa.

Mabenki wanaweza toa sana elimu za ujasiriamali ila sio elimu ya kifedha.

Ni elimu inayo paswa kutolewa sana kwenye jamii hasa walimu ambao ni wahanga wakuu wa mikopo, shida nani anatoa hio elimu?
Walimu wanapigwa Sana kwa Kweli wanapigwa Hadi wanadata
 
Uongo, ingekuwa kweli hiyo ni fursa ya kupiga pesa kupitia fidia.
Taarifa zipo wazi kwenye maandishi. Ukiwa unafungua akaunti yoyote soma zile terms and condition na soma contract kila kitu kimo mule. Kama kuna kitu hakimo na kikafanyika bila makubaliano hiyo ni fursa kwako.

Unadhani wanaofungua akaunti wote ni vilaza? Kila siku ungesikia kesi mahakamani watu wakidai fidia iwapo kuna ukiukwaji wa taarifa.
Ulishawahi Ona gharama za miamala zimebandikwa kwenye Atms? Atms wanatumia vilaza?
 
Huwezi kuona kwenye Atm, Kuna gharama za miamala!
Zile karatasi zinazotupwa kwenye dust bins benki wameshachaji!!! Laiti kama watu wangejua gharama za kutaka Ile receipt ambayo wanasoma tu balance na kuitupa kwenye bin , wasingeitaka Ile receipt , na benki zingekosa mapato,
Vipi kwa mfano nikiisomea hiyo risiti mtandaoni. Je, bado watakata?
 
Huwezi kuona kwenye Atm, Kuna gharama za miamala!
Zile karatasi zinazotupwa kwenye dust bins benki wameshachaji!!! Laiti kama watu wangejua gharama za kutaka Ile receipt ambayo wanasoma tu balance na kuitupa kwenye bin , wasingeitaka Ile receipt , na benki zingekosa mapato,
Na hata simbanking, hawakwambii kiasi kilichobaki kwenye akaunti. Mpaka uulize ambapo nahisi kuna kiasi utahitaji kulipia, sio kama tigopesa and the like. Au ni akaunti yangu tu jamani
 
Ulishawahi Ona gharama za miamala zimebandikwa kwenye Atms? , Atms wanatumia vilaza?
Hizo gharama za ATM haziji tu, kuna makubaliano uliyakubali. Again nakuambia, lolote bank wanalofanya kwako bila makubaliano ni fursa kwako.

Nikuulize, hiyo ATM ulipewa bila makubaliano? Wakati unafungua akaunt na kuomba huduma ya kadi, ulisani nyaraka zipi? Zilikuwa zinasemaje?
 
Kubwa Zaid Ni viwango vya riba
Viwango vya riba vipo wazi kwenye mkataba boss. Unapewa mpaka rejesho kwa mwezi lipoje na kwa mda gani. Mabadiliko yoyote unapewa kwa maandishi in advance. Binafsi ni mkopaji.
Na pia kueleza adhari za Mikopo ya long yrem na Short term
Hili si jukumu la bank boss. Ni jukumu la mkopaji kujua faida na hasara za mkopo in long run and short run. Bank wanafanya lililo ndani ya uwezo wao tu, sana sana watahitaji wewe ndo uwaeleze matokeo ya huo mkopo in long run and short run kupitia agenda for action au business plan.
Sababu za kukopa zinatofautiana, biashara zinatofautiana. Una biashara ya madini, Bank hawana wataalam wa madini, wao wanaangalia capacity, sasa Imagine bank atafute wataalam wa madini ili ikupe elimu in short run and long run. Kazi ya bank itahama kutoka biashara ya fedha kwenda kwenye biashara ya ushauri na iwe na wataalam kwa kila sekta.
Huku mtaank mnanisumbuwa sna watu Kuja niwashauri Aina Mikopo unakopa
Ni fursa. Fungua consultancy firm
 
Back
Top Bottom