Ndio maana nimekuambia mnatanguliza sana ushabiki badala ya uharisia.
Haya niambie kwann Marekani anaendelea kununua mafuta ya Urusi kwa mlango wa nyuma wakati ameyapiga marufuku?
Kwanza kuhusu Poland ni Ujerumani yenyewe ilitangaza kuwa ita isambazia gesi Poland baada ya Urusi kusitisha usambazaji sasa sijui tukusikilize ww au viongozi wa Ujerumani.
Kuhusu Uchumi Urusi ni moja wapo ya taifa lenye nguvu za kiuchumi barani ulaya na ni taifa la 5 kwa Uchumi mkubwa barani ulaya kati ya nchi zaidi ya therathini na kitu.
Alafu kila taifa duniani lina Umuhimu katika nafasi yake na kutokana na ilicho nacho.
Mfano kwenye sekta ya viwanda nchi kama Japan, China, Marekani,na Ujerumani ni mataifa muhimu sana.
Kwenye sekta ya nishati mataifa kama Urusi, Qtaar, Saudia,UAE,Iran na Venezuela ni mataifa muhimu sana.
Kwenye sekta ya kilimo na usambazaji wa chakula duniani mataifa kama Urusi, Ukraine,India, Thailand na Pakistan ni mataifa muhimu sana.
Kila taifa lina Umuhimu wake.
Ulaya kamwe haotakuja kuacha kutumia nishati ya Urusi ni kuomba mungu atupe uhai tu,watajifanya wamepiga marufuku lakini wanaenda kuinunua kwa mlango wa nyuma.
Hata kwenye suala la Rubo kwenye vyombo vyao vya habari wanakataa lakini nyuma ya pazia wameruhusu makampuni yao kununua kwa Rubo.