Fishes & Marine life special thread.

Paedocypris: huyu ni samaki mkubwa tu katika jamii yao, wala sio dagaa. Anashikilia rekodi ya samaki mdogo duniani. Kwenye picha hiyo; huyo kakomaa kabisa kuendeleza kizazi chao
 

Katika pande mbili za mazingira ya bahari ; Kutisha na kuvutia. Hili ni eneo samaki wengi wasio tishio kwa samaki wengine na kwa binadamu ndio makazi yao. Hapa kauli mbiu yao ni AMANI ITAWALE KWA WOTE
 

Ribbon eel; hawa ni jamii ya wale hatari ingawa hawa sio hatari na wanafugwa kwa baadhi ya watu. Mara nyingi hujifungua mdomo pale waonapo tishio ili aonekane hatari ila kiuhalisia ni tofauti.
 

Sea snail inasemekana ni moja ya samaki wenye utajiri mwingi wa afya kwa mwanadamu.
 

Nguva/mermaid?? Hapana! Wenzetu walimpa jina la Dogong. Huyu ni mnyama kabisa 100% anaishi kwa kula majani yanayojiotea huko chini ya bahari. Wanyama hawa wanapatikana pia katika maji baridi mfano ziwani. Ni kati ya viumbe vilivyo katika hatari kubwa ya kupotea duniani.

Amini ya kwamba dogong ni wana kama kaundugu na wenzao wa nchi kavu, Tembo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…