Fisi aliyeuliwa amekutwa na chapa ya jina kwenye paja lake

SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS
View attachment 3244143
Askari wa Mamlaka ya Wanyamapori kwa kushirikiana na TANAPA na Jeshi la Polisi wamefanikiwa kumuua fisi mmoja katika Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, baada ya kuingia katika makazi ya wananchi. Cha kushangaza, fisi huyo alikutwa na maandishi kwenye paja lake la kushoto, yakisomeka MALLA N 7, ingawa maana yake haijafahamika.

Operesheni hiyo maalumu imeanzishwa kufuatia matukio ya fisi kushambulia watoto nyakati za usiku, ambapo baadhi yao wamepoteza maisha. Fisi huyo aliuliwa katika kijiji cha Kimali, Kata ya Nyamalapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti wanyama hao hatari.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Anna Gidarya, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwamigagani, Kata ya Mwalushu, amewataka wote wanaomiliki nyara za serikali kinyume cha sheria kuzisalimisha kwa wahusika wa uhifadhi haraka iwezekanavyo ili kuepuka hatua kali za kisheria.

Tangu operesheni hiyo ianze, jumla ya fisi 16 wamekwisha kuuawa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Itilima na kikosi kazi cha askari wa TAWA, TANAPA na Jeshi la Polisi.
Basi tuseme itilima hoyeee,mnaupiga mwingi.Ila tu baada msituambie mmempoteza mwanachama wenu.Msimu wa chafuzi huu tena.
 
Mkuu kila kiumbe kina moyo, as long as kina moyo unaweza kukiita na kikaja na ukakifanyia fakraa (kuingiza roho nyingine ndani yake ili kuvaa ule mwili wa mnyama) na kuanzia hapo unakitawala!
😲😲😲😲
 
Aisseee alafu wanapenda fisi sana😂
 
Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Anna Gidarya, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwamigagani, Kata ya Mwalushu, amewataka wote wanaomiliki nyara za serikali kinyume cha sheria kuzisalimisha kwa wahusika wa uhifadhi haraka iwezekanavyo ili kuepuka hatua kali za kisheria.

🤣 akimaanisha nyara hizo ni pamoja na fisi wanaofugwa?
HATARI NA NUSU!
 
SOURCE: GLOBAL PUBLISHERS
View attachment 3244143
Askari wa Mamlaka ya Wanyamapori kwa kushirikiana na TANAPA na Jeshi la Polisi wamefanikiwa kumuua fisi mmoja katika Wilaya ya Itilima, mkoani Simiyu, baada ya kuingia katika makazi ya wananchi. Cha kushangaza, fisi huyo alikutwa na maandishi kwenye paja lake la kushoto, yakisomeka MALLA N 7, ingawa maana yake haijafahamika.

Operesheni hiyo maalumu imeanzishwa kufuatia matukio ya fisi kushambulia watoto nyakati za usiku, ambapo baadhi yao wamepoteza maisha. Fisi huyo aliuliwa katika kijiji cha Kimali, Kata ya Nyamalapa, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kudhibiti wanyama hao hatari.

Mkuu wa Wilaya ya Itilima, Anna Gidarya, akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Mwamigagani, Kata ya Mwalushu, amewataka wote wanaomiliki nyara za serikali kinyume cha sheria kuzisalimisha kwa wahusika wa uhifadhi haraka iwezekanavyo ili kuepuka hatua kali za kisheria.

Tangu operesheni hiyo ianze, jumla ya fisi 16 wamekwisha kuuawa katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Itilima na kikosi kazi cha askari wa TAWA, TANAPA na Jeshi la Polisi.
Wakiambiwa wasukuma ni majinga washamba hawaelewi. Ni aibu karne hii jamii inafuga fisi, mnyama mchafu km huyo.
 
Back
Top Bottom